Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,340
- 51,891
TWENDE MBELE TURUDI NYUMA, WANAWAKE WALITESEKA SANA
Anaandika, Robert Heriel
Licha ya kuwa Mimi ni mfuasi mzuri wa mfumo dume lakini nachukizwa na tabia ya utesaji, unyanyasaji na uzalilishaji wa Wanawake. Mfumo Dume ni Amani, haki, upendo na heshima Kwa dunia yetu.
Acha Wanawake wafanye watakavyo, Acha wawapeleke mputamputa wanaume wapumbavu, Acha wafurahie Uhuru wao. Waliteseka Sana. Hata kama zipo changamoto za Uhuru wao lakini ni akheri changamoto hizo kuliko Mateso waliyoyapata Mama zao.
Wanawake waliteswa na mababu zetu, walichapika, walifanywa Kama Punda.
Yaani unakuta Mwanaume anampiga Mkewe Kama Ngoma, ati kisa yeye ni mume au mwanaume. Haipendezi! Huo ni ukatili, na Dalili ya unyama.
Uchunguzi wangu ambao kimsingi siku zote haupendelei wala kusema uongo, ulibaini kuwa Wanawake waliowengi WA miaka ya 80 Kurudi nyuma 90% hawajawahi kufurahia Ndoa wala mahusiano.
Ubaba ni ubabe ndio hata Taikon ninakubali hivyo. Lakini uwe Ubabe wenye akili sasa, ubabe katika mambo ya Msingi. Taikon ni Muumini wa HAKI, najua haki ndio huleta Amani na Furaha!
Uchoyo ni miongoni mwa Mateso waliyoyapata wanawake. Hata hivi leo wapo wanaume ni machoyo, mabinafsi na yenye kujipendelea. Nani alikuambia Mkeo hapendi Paja la kuku Kama wewe, unakuta mwanaume mchoyo, vitu vyote vizuri awekewe yeye tuu. Akiulizwa, ati yeye ndio anatafuta pesa. Acha uchoyo Bata wewe. Kutafuta pesa sio kisingizio cha kujipendelea, Weka utaratibu wa kugawana vitu vizuri katika familia yako.
Wanawake ni viumbe wanaojifunza kutoka Kwa Wanaume, hiyo iweke akilini. Ukiwa mbinafsi Mkeo lazima Naye awe mbinafsi. Wanawake kisaikolojia wao wapo chini yetu hivyo hutegemea upendeleo kutoka kwetu.
Wanawake ni Lastborn hivyo hupenda kudeka na kupendelewa. Kutompa mwanamke Haki ya U-lastborn ni moja ya Mateso Kwa mwanamke.
Mwanaume popote Ulipo tambua kuwa wewe ni Firstborn hata kama Mkeo amekuzidi umri au kipato au Jambo lolote lakini Nature inakutambua hivyo.
Ni kweli Wanawake ni dhaifu Hilo wala halina Ubishi, lakini udhaifu wao hauondoi lolote katika thamani Yao.
Wanaume wengi hutumia vipato vyao kuwanyanyasa wanawake, kuwaonea na kuwatesa. Wanawake wengi kutokana na umasikini wao au kwenye familia watokazo hujikuta wakivumilia Mateso hayo. Chepuka uwezavyo lakini unashindwaje kujificha mpaka Mkeo akajua?
Ni kweli wanaume hatuwezi kuwa na Mwanamke mmoja hilo ni kweli. Lakini tutumie akili kusudi kulinda mioyo ya Wake Zetu. Wanaumia Sana.
Oooh! Wanawake hawaeleweki. Oooh! Wanawake ni chombo cha STAREHE. Ni kweli Wanawake hawaeleweki, na ni kweli ni chombo cha STAREHE. Sasa ndio uwatese na kuwanyanyasa?
Taikon ninajua kuwa, Matokeo ya wanawake kuwanyanyasa wanaume pale wawapo na vipato ni matokeo ya wao kunyanyaswa na Wanaume.
Binti ambaye Baba yake hakuwahi kumtesa Mama yake, ni nadra Sana kumkuta binti huyo akimnyanyasa mwanaume hata akiwa na kipato. Kinachofanya Wanawake wanyanyase Wanaume ni kutokana na tabia walizoziona Kwa Baba Yao alivyokuwa anamfanyia Mama Yao.
Maneno Kama, Ninawalisha tuu hapa, mnajaza Choo, wewe mwanamke ni Masikini Kama huko kwenu,
Kama nisingekuoa wewe ungekuwa hivi, ulikuja umekondeana sasa umenona unaanza kuleta kiburi,
Usiniletee tabia zenu za hovyo hapa, na maneno ya Dharau Kama hayo.
Maneno hayaishi, ukimwambia mtu neno Baya jua hatalisahau KAMWE!
Mwanaume ndiye anayeweza kumbadilisha mwanamke tabia. Tabia hizi mbofumbofu za wanawake Sisi Wanaume ndio tumesababisha.
Mwanaume kujiamulia kuoa vile atakavyo, kisa yeye ni mwanaume, hajali hisia za mkewe, walah! Yeye anachojua ni kufuata matamanio yake. Huo ni Ubinafsi.
Hujakaa na Mkeo mkajadili kuwa unataka kuongeza mke unajiamulia tuu. Hiyo sio HAKI na Mwanaume siku zote anayejitambua lazima azingatie HAKI.
Haya Mumechuma Mali, imetokea mnataka kutengana, kitu gani kinakufanya upate shida kumgawia hiyo mwanamke sehemu ya Mali mlizochuma? Kitu gani Kama sio ushetani.
Mkeo kama anakujua wewe ni mtu wa HAKI kamwe hawezi kuchukua kimabavu Mali ambayo hutompa wewe mwenyewe.
Unamdhulumu mwanamke Mali, unamfukuza licha ya kuishi na wewe miaka nenda Rudi, kisa alikuwa hafanyi kazi za kuzalisha, Ila alikuwa anaitunza familia yako na kukuhudumia mumewe ili ukazalishe lakini wewe hilo unaona kwako sio Mchango. Unafukuza. Hayawani mkubwa weee!
Taikon Kama Mwanaume mfuata mfumo Dume. Anapenda kuwaambia vijana wa kileo. HAKI na upendo ndio msingi wa Maisha.
Huwezi ukamdhulumu Mkeo ukabaki salama.
Na huwezi ukamdhulumu Mumeo ukabaki salama.
Mpe mtu haki zake.
Kama mmeshindwana, kaaeni muongee mnaachanaje, pigeni Hesabu Kwa Haki.
Mke achukue 40% au 30% au kadiri ya mlivyoishi na muda mliokuwa pamoja.
Au mume achukue 40 au 30 ikiwa mke atabaki na watoto.
Kuendekeza ubinafsi na Kupenda penda Mali kutakufanya usiwe na Amani na furaha hasa ukiwaonea watu wako wa muhimu katika maisha yako.
Zingatia, Haki ni Haki.
Mkeo akiwa mwema mlipe Mema.
Mkeo akiwa Mbaya basi mlipe Mabaya.
Jitahidi uwe hakimu mzuri katika maisha.
Baya moja lisiondoe Mema elfu moja.
Na jema moja lisifute mabaya elfu moja.
Haki bin Haki
Kuna Wale Wadada wa mjini wanaofunga ndoa kwaajili ya Mali alafu baada ya miaka mitatu wanavunja ndoa ili mgawane Mali. Hao usiwachekee. Haki bin haki. Ubaya ubaya, wema Kwa wema
Usikubali Mkeo au mumeo muliyewahi kuishi Kwa furaha mwenye Mchango mkubwa katika maisha yako, akakususia Mali mlizochuma pamoja, hazitakusaidia.
Usione shida kupata kidogo Kwa Yule aliyekufanya ukapata vingi.
Yule Mtibeli,
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam