Human nature ni complex sana. Nikisoma post hizi za watu nawaza,tunaishi nchi moja wote? Tunaangalia bunge hili hili? Tunajua watu wamegawana pesa, zimetoka wapi? NADHANI WOTE TUNAKUBALIANA PESA ZIMEGAWANYWA. Tuanze hapo sasa Escrow akaunt kama ya umma, kwa nini wamechukua? Kama si za umma , waliogawana hizo pesa wana business gani na IPTL? Hasa hawa viongozi wetu wameuza bidhaa gani hadi wapewe hizo pesa. Mimi si ccm wala UKAWA ni mtanzania ninayenunua umeme 10000/- napata unit 8. Napita kwenye barabara yenye mashimo tangu march , nilienda hospitali nikaambiwa hakuna dawa, ndugu yangu alilazwa hakiwekewa shuka kwa sababu hakuna dawa. IPTL kwa nini wasingetulipia deni MSD? mi nauliza hilo tu.