Tulisema hili la Escrow mapema. Akaunti nyingi zilizopokea hela zilikuwa ni mpya, nyingine hazikuwa hata na vitabu vya hundi. Hatuliachi. Ni jambo la kusikitisha sana kuona hata benki zinazomilikiwa na madhehebu ya dini sasa zimekuwa sehemu ya kusambaza fedha zilizoibwa. Fisadi anapoachia ngazi bila kufikishwa mbele ya sheria ni sawa na kupewa mapumziko kwenda kutumia alichofisadi. Kuachia ngazi tu haitoshi.