Kumbukizi muhimu za kashfa ya ESCROW; Kikwete asema fedha za ESCROW ni mali ya IPTL na sio za Serikali

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Wadau.
MZEE KIKWETE ALISEMA FEDHA ZA ESCROW NI MALI YA IPTL NA SIO ZA SERIKALI.
TUESDAY DECEMBER 23 2014.
Rais Jakaya Kikwete amesema fedha zilizochotwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow hazikuwa zinafikia Sh306 bilioni, bali ni Sh202 bilioni na zilikuwa mali ya Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL.
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete amesema fedha zilizochotwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow hazikuwa zinafikia Sh306 bilioni, bali ni Sh202 bilioni na zilikuwa mali ya Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL.
Akijibu swali alilojiuliza mwenyewe katika hotuba yake ya zaidi ya saa mbili kuwa: “Fedha hizi mwenyewe nani, umma au IPTL?” Rais Kikwete alisema kumekuwapo na maneno mengi, kila mtu anasema yake na wenzangu Wakwere tunasema ‘tunazoza sana’ akimaanisha waongea sana.
Alisema, “Kimsingi fedha hizi ni za IPTL, katika swali pesa za nani, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alipoulizwa na Kamati ya Bunge alisema humu yawezekana zipo za umma pia zipo za IPTL.
NB: Waliokula Fedha za Escrow Ni WAHUJUMU Uchumi. Na Watazitapika tu kwani ni Mali ya Serikali.
Tunatekeleza
 

Attachments

  • kikwete_jakaya.jpg
    kikwete_jakaya.jpg
    16.1 KB · Views: 1
Back
Top Bottom