ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,141
- 951
Wandugu tujihadhari sana, pale Mlimani City kuna viashiria vya kuaminika kabisa kwa wahudumu (Tellers) wa baadhi ya Benki za pale Mlimani City ambao hawana uaminifu kabisa ni vibaka kama sio majambazi kamili!!!, Ukichukua fedha nyingi wanatoa taarifa kwa Majambazi..huwa wanalanda landa katika eneo hilo..... Matukio mengi ya uporaji yanatengenezwa na wao... Kuna ndugu kanisimulia kisa cha kufuatiliwa na amenisimulia kisa cha kusikitisha cha kufuatiliwa na majambazi wenye silaha baada ya kuchukua fedha za Mkopo kwenye Benki ya NMB Mlimani City pale. Ilimlazimu wajisalimishe kwenye lindo fulani na majambzi wakaishia kupiga risaisi hewani na kutawaniyka ..mpaka sasa hajui Majambazi hao walijuaje amechukua hela nyingi..Mnakumbuka visa vya watanzania wenzetu kuuwawa hapo Mlimani City na kula yule Sister wa Kanisa la Ubungo Makoka nae aliuwawa pale Ubungo wakati fulani baada ya kutoka hapo Mlimani City -
TUWE MAKINI SANA
TUWE MAKINI SANA