Mlimani City walikuwa wanajiamini na nini hadi kumgomea Magufuli hivi? Inamilikiwa na nani?

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,779
18,746
Anaandika Boniface Jacob ambaye alikuwa Meya wa Ubungo na Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema, aisee inaonekana wafanyabishara wote wa ndani na wa kigeni walikuwa wakimuogopa Magufuli isipokuwa mmiliki wa Mlimani City kama anavyoandika Boniface Jacob hapa.

================

ZAMA ZILE ZA GIZA kumbi nyingi sana Dar es Salaam ziligoma Kupokea Pesa za Chadema Kwa ajili ya Kukodi Kumbi za Kufanyia mikutano ya Kamati kuu 2016 Kuelekea Operation Ukuta Giraffe Hotel wao Katikati ya Kikao Walifuatwa na Magari ya Polisi, Wakaturudishia pesa zetu tuondoke.

Basi tukavunja Kikao wakiwa wameshapika Chakula cha Wajumbe na Break fast, Ila wakarudisha pesa zote Tiffany Diamond, Wao Siku ya Kikao cha Kamati kuu,Waligoma Kufungua Ukumbi Kufuatia Vitisho walivyo pokea kutoka Serikalini, Wakaturudishia pesa zetu, tukatafuta Kumbi Nyingine.

2017 Double Tree Hotel wao Walipokea pesa za Chadema Kwa ajili ya Kikao cha Kamati Kuu Siku 3 ila Baada tuh ya Kikao cha Siku ya Kwanza Kesho yake wakaomba tusi rudi tena pale Hotelini Kwao
Kufuatia Vitisho walivyopokea kutoka Serikalini.

Siku Moja Week end baada ya Vikao pia tukaenda Hotel Moja Masaki Kupumzika na Kupata Chakula na Kinywaji Wao Wahudumu Walikatazwa kabisa Kuja kutusikiliza Mezani Kwetu,Tulipo kuwa wakali Meneja alituambia Maboss zake Wahindi Wametuona tukiwa tunaingia Wameogopa sana Ukaondoka.

Wamiliki wa Kumbi moja tuh ya Mlimani City hadi Leo hatujui kwanini Walikuwa wanajiamini sana Mara zote Walipokea pesa na Wakatupatia Ukumbi Chadema,Serikali ilipofika kuwatisha Walikuwa Wanatoa akaunti namba za Benki,Serikali iweke pesa zote za Kuwa rudisha Chadema.

Mwaka 2019 Ukumbi Wa Mlimani City pakiwa pamepambwa na bendera za Chadema,Serikali Walifika tena Kuwatisha ili tunyimwe Ukumbi, Jamaa wa Katoa Akaunti ya Benki Waingize pesa ili wao wavunje Mkataba na Chadema Kwahasira Serikali ilirudi Mida ya Saa 5 Usiku ikiwa na Polisi wengi.

Polisi wakazingira Ukumbi Mlimani City, Usiku Ule Wajumbe wa Mkutano Mkuu waliokuwa Dar es Salaam tukahamasishana Kuja Mlimani City Wanachadema Walipojaa, Polisi Walitoka nje ya eneo la ukumbi kwahasira walipiga Mabomu wakaondoa Bendera zote za Barabarani pamoja Mgambo wa Jiji.

Kwa Mabomu yale nilifikiri sasa Wamiliki wa Ukumbi Wa Mlimani City Wataingia Uoga, Siku Nyingine hatutopewa tena Ukumbi Tulienda tena 2020 kukakodi Ukumbi tulijua watagomea, Walaah hata hawakuuliza Maswali, Walipokea pesa wa Katoa Ukumbi, Tukampitisha Lissu kama Mgombea Urais.

Nimeitoa Twitter

Capture.PNG
 
Wanasiasa wanajuana, wanatuchanganya tu raia, siasa za Chadema ni za wachumia tumbo, wanatingishaga tu kibiriti wapate maslahi yao, uzuri walimkuta Ngosha acheki na Kima, uso wa mbuzi, Mbowe ni mtu wa maslahi,mbwa Koko, yupo pale kufanikisha deals zake, Ngosha alikuwa anajua kuwa Mbowe ni Mwanasiasa uchwala.

Sent from my WAS-TL10 using JamiiForums mobile app
CCM na Chadema wote wanaimba Mungu fundi, kamaliza ugomvi..
 
Anaandika Boniface Jacob ambaye alikuwa Meya wa Ubungo na Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema, aisee inaonekana wafanyabishara wote wa ndani ...
Hoja mfilisi pambanen kujenga chama muungwe mkono mtabaki mnasema mtu kashaondoka huku mkiendelea kutawaliwa na ccm iliyojaa ufisadi!

Mmebakiza vioja siyo hoja siyo mwenyekiti wenu wala nyie nyote kwasasa hamna hoja hoja ni matusi dhidi ya mwendazake
 
Anaandika Boniface Jacob ambaye alikuwa Meya wa Ubungo na Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema, aisee inaonekana wafanyabishara wote wa ndani...
Aisee poleni sana wadau wa Uhuru, demokrasia na maendeleo

Ndio maan tunasema Samia anaupiga mwingi.

Kuzuia shughuli za chadema ni kuiumiza jamii nzima ya kitanzania.

Ona wafanya biashara walivyokuwa wakiteseka sana kwa sababu za ajabu ajabu
 
Wanasiasa wanajuana, wanatuchanganya tu raia, siasa za Chadema ni za wachumia tumbo, wanatingishaga tu kibiriti wapate maslahi yao, uzuri walimkuta Ngosha acheki na Kima, uso wa mbuzi, Mbowe ni mtu wa maslahi,mbwa Koko, yupo pale kufanikisha deals zake, Ngosha alikuwa anajua kuwa Mbowe ni Mwanasiasa uchwala.

Sent from my WAS-TL10 using JamiiForums mobile app
wewe ndio mchumia tumbo. Kama huoni hilo lilikuwa tatizo basi wewe una roho mbaya roho za kimaskini
 
Back
Top Bottom