Tuwe makini sana na benki za Mlimani City - DSM

Tuwe makini sana na benki za Mlimani City - DSM

Hua nikichukua kiasi kikubwa nikishaingia kwenye gari nazigawanya faster nyingine naziweka hadi sehemu za siri. Kisha nabakisha kiasi kidogo na kuweka kwenye libahasha la bank kwenye siti ya mbele bila kificho.

Akijipendekeza jambazi ataambulia kapesa kiduuchu tofauti na matarajio yake. Maana akishaona mfuko tu anachukua na kutimka

Weeee cku hizi wanaua tu kabla hata haujaulizwa hela iko wapi! Huyo mshikaji aliyetoka hapo NMB mlimani city aliuliwa then ndo wakachukua mapene kwenye gari.
 
Mtawasingizia mateller but in reality teller awapo kwenye cube huwa hana kitu chochote cha kumsaidia kuwasiliana na mtu alie nje au ndani ya banking hall!

Katika benki teller ni mtu alie busy saana kuliko wafanyakazi wote ndani ya benki.

Teller huyu...
 
Mateller ndo wanatoa mchongo mzima!...6 months ago nilienda kudeposit postal bank POSTA teller akaanza kuniletea story ooh rudi na hizo hela uje kesho upate special rate afu anafosi fulani nikamwambia umetega mijambazi yako nje alihamaki mpaka nikamhisi ki2... Mateller hapana aisee!
 
Wewe nadhani ni banker. Sisi wateja tunawaona hao mateller wakiwa na smart phones zao kwenye cubicles na mara nyingine wanapiga na kupokea simu. Kuna apps za kupiga picha kwa siri ambapo mpigaji anaweza kutransfer hiyo picha faster! We ukiona wachukua mzigo, na teller anajidai kushikashika smart phone yake, ama wale security guards wanazungukia sehemu unayohudumiwa, CHUKUA TAHADHARI, kwani YAWEZEKANA ukawa mhanga!

Huo mchezo uko mpaka bureau de change! Wale masecurity ni balaa, wakishashtukia umefanya exchange in huge amount anaenda kupiga cmu nje fasta kabla hujatoka! Mi week iliyopita niko na braza angu bureau security anapiga cmu tulimkunja shati!
 
Naomba kwa anayejua gharama za askari au yale magari ya kusindikiza pesa
ni shilingi ngapi atuwekee tujipime kama inawezekana kuwatumia
ila kiukweli mimi huwa nao nawaogopa. fikiria kama hizo pesa umechukua
na unaleta nyumbani kwa mambo muhimu hao nao si wanaweza kukurudia baadae?

Mimi ninachofanyaga ni yule ninayetakiwa kumlipa
namwomba akaunti yake namwingizia fedha,Hata kama ni benki tofauti ipo huduma ya kuhamisha.
namletea pay in slip. Afu anakupa hicho ulicholipia.

Cha ajabu majambazi siku hizi hata 3M wanaona ni dili
sijui bei za risasi zimeshuka,mtu anakuzukia kukunyanganya
mauzo ya vocha huku wana bodaboda na bastola,ni ajabu
lakini inatokea.Tuchukue tahadhari.

Mkuu kwa taarifa tu bei Risasi Ni cHini ya buku
 
Mtawasingizia mateller but in reality teller awapo kwenye cube huwa hana kitu chochote cha kumsaidia kuwasiliana na mtu alie nje au ndani ya banking hall!

Katika benki teller ni mtu alie busy saana kuliko wafanyakazi wote ndani ya benki.

Mara nyingi saaana nimeshuhudia kwa macho yangu teller anatuma na kujibu sms akiwa kwenye kiboksi chake cha kazi!! Na siyo benki moja; ni benki tofauti kama tatu........
 
Jamani mnaongea upuuzi, benki makini inafuata taratibu za kazi, bankteller akiingia kibandani anatakiwa akabidhi simu yake , mkoba ,wallet kwa supervisor na vinafungiwa hadi anapoenda lunch au jioni anapotoka, mm nafanya stanbic mbeya branch na hii inakuwa adhered strictly, shida inakuja lapses zinakuwa kwenye physical security na walinzi, unakuta watu wanasindikizana bank hadi watatu wkt mwenye transactions ni mmoja ukiwauliza ooh nimemsindikiza mwenzangu, banking hall sio pa kwenda kupumzika, sasa kwa show offs za mlimani city MTU anabeba ukoo Mzima anaingia nao bank for what purpose? jiulizeni ni kwa nini mlimani city pekee na sio pengine, huwa naingia NBC na crdb mlimani city kuna unakuta watu wamekaa tu hawaeleweki , hao ndio spotters wenyewe, ukitoka nae anatoka anawapigia wenzake wanakutight, punguzeni kujazana mlimani city
 
Bank teller wewe, tena wa CRDB au NBC Mlimani city
 
Sorry niko Stanbic mbeya branch ila ni mteja wa crdb for my personal account @ mandule
 
Leo ndio nimejua ukweli, nilidhani jamiiforum ni home of great thinkers lkn kumbe ni otherwise
 
Kuna uzi hapa jf ulishaizungumzia hii kitu sana na kutaja mlimani city na millenium tower kijtonyama kama sehemu hatari za kuchukulia pesa benki. Jitahidini jamani kwenda kuchukulia kwenye matawi mengine mengi salama yaliyotapakaa dsm msijali gharama za kufika huko kwani roho haiuzwi. Hapo mlimani city inaonekana majambazi na vibaka wamepiga kambi sana ni wakati sasa wa vyombo vya dola kutumia wataalamu wao kuvunja hayo magenge.
 
Hua nikichukua kiasi kikubwa nikishaingia kwenye gari nazigawanya faster nyingine naziweka hadi sehemu za siri. Kisha nabakisha kiasi kidogo na kuweka kwenye libahasha la bank kwenye siti ya mbele bila kificho.

Akijipendekeza jambazi ataambulia kapesa kiduuchu tofauti na matarajio yake. Maana akishaona mfuko tu anachukua na kutimka
Hiyo mbinu yako coco kabisa what if wakikikuzimisha kwa shaba!
 
Mkuu kwa taarifa tu bei Risasi Ni cHini ya buku
Kiongozi sikulijua hilo,ni vema serikali iangalie mambo kama haya
na kuchukua hatua,pale iliposemekana watu wanatumia mafuta ya
taa kuchanganya na petrol ili wapate faida kubwa,
serikali ilipandisha bei ya mafuta ya taa,na hii ilileta athali kubwa
hasa kwa watu wa vijijini,sasa kama hilo liliwezekana,

kwa nini bei ya risasi ambayo si muhimu kwa raia wa kawaida
kama mafuta ya taa isipandishwe bei ili kuepusha matumizi
holera ya silaha? Naamini taasisi za serikali
hazitaathirika kwa kupanda bei ya risasi
kwani bidhaa za serikali hazilipiwi kodi.
 
Leo ndio nimejua ukweli, nilidhani jamiiforum ni home of great thinkers lkn kumbe ni otherwise
Mkuu ninapata mashaka
kama wewe siyo jambazi?
kwa andiko lako hili unataka kusema uzi huu hauna maana?

Nashawishika kukuita jambazi kwani
umeona huyu anaharibu michongo yenu siyo?

Naomba uwaambie na wenzio,hizi fedha zinazowafanya mtutoe roho,
sisi tunazitolea jasho,na hamtakaa mzifaidi salama.
mtaishia kuwa vichaa na kuokota makopo kwani damu ya mtu
ina tabia ya kudai kisasi mbele za Mungu.
 
Back
Top Bottom