Tuwe makini sana na benki za Mlimani City - DSM

Tuwe makini sana na benki za Mlimani City - DSM

Ndo ushamba huo haujawesha mnabeba mihela mingi ya nini ili mpate sifa!! Cheque book za kazi gani kama unafanya malipo si utumie kiasi kidogo na kama unachukua more than 10 m kwa mf hata kama benki yako haimo humo mcity si ufanye transfer,acheni ushamba wa kubeba mihela,nawaruhusu wanaobeba mishahara tu nanyi chukueni Police escort alaah!
haya...
 
Mkuu hapo kwa walinzi umenena,Kuna ile mitambo ya cctv
wale wanaokaa kwenye chumba chenye tv wanaona kila kitu
na wale ni rahisi kuwasiliana na majambazi maana wao
hawako busy kama mateller,lakini wanaona kila kitu
aliyepewa hela nyingi au ndogo wanaona.

Kuna umuhimu wa wamiliki wa mabenki
kuimulika idara hii,kwani ipo kwa ajili ya
ulinzi lakini inaweza kutumika vinginevyo
nadhani tunaikumbuka story ya kasusula.

Manager wa branch anaweza akawa mwizi teller naye mwizi mlinzi naye mwizi....wote syo wa kuwaamini
 
Mtawasingizia mateller but in reality teller awapo kwenye cube huwa hana kitu chochote cha kumsaidia kuwasiliana na mtu alie nje au ndani ya banking hall!

Katika benki teller ni mtu alie busy saana kuliko wafanyakazi wote ndani ya benki.

Wana smart phones na wanachat muda wote.
 
Hua nikichukua kiasi kikubwa nikishaingia kwenye gari nazigawanya faster nyingine naziweka hadi sehemu za siri. Kisha nabakisha kiasi kidogo na kuweka kwenye libahasha la bank kwenye siti ya mbele bila kificho.

Akijipendekeza jambazi ataambulia kapesa kiduuchu tofauti na matarajio yake. Maana akishaona mfuko tu anachukua na kutimka

Eti akijipendekeza ahahah kwanza anakishushia mvua ya risasi akutoe ubongo
 
Eneo lile lipo Targeted sana.
Na matukio mengi sana yanaripotiwa pale.Na hii ni kwa wenye kutumia silaha,sasa sipati picha wale wanaozimwa kimya kimya kwa bastola za kuwekewa shingoni.

Ipo siku watajulikana tu,maana majambazo woote wakikamatwa wanaenda kuteswa kama mbwa mwizi,wanataka mnyororo woote.Na ndio maana utashangaa mtu anavamiwa tu kwenye nyumba na kukutwa na silaha.Sio kwamba polisi ndio walinusa issue,ila ni kwamba kuna mtu jela kamtaja mwenzie.Au mtu waliedhulumiana akaona bora nona na iwe noooooma
 
Kuna jamaa yangua likoswa koswa hapo baada ya kuchukua mzigo nahisi kuna watu wanatoa info za wateja wanapobeba mzigo mkubwa
 
Dadangu kanisurika mwaka Jana hapo! Ni mabank tellers!
Halijakukuta utabisha!
 
Kuna watu wako pale mliman hawana kazi zaidi kuzunguka zunguka tu, hao ndio wanapanga dili zote
 
wandugu tujihadhari sana, pale mlimani city kuna viashiria vya kuaminika kabisa kwa wahudumu (tellers) wa baadhi ya benki za pale mlimani city ambao hawana uaminifu kabisa ni vibaka kama sio majambazi kamili!!!, ukichukua fedha nyingi wanatoa taarifa kwa majambazi..huwa wanalanda landa katika eneo hilo..... Matukio mengi ya uporaji yanatengenezwa na wao... Kuna ndugu kanisimulia kisa cha kufuatiliwa na amenisimulia kisa cha kusikitisha cha kufuatiliwa na majambazi wenye silaha baada ya kuchukua fedha za mkopo kwenye benki ya nmb mlimani city pale. Ilimlazimu wajisalimishe kwenye lindo fulani na majambzi wakaishia kupiga risaisi hewani na kutawaniyka ..mpaka sasa hajui majambazi hao walijuaje amechukua hela nyingi..mnakumbuka visa vya watanzania wenzetu kuuwawa hapo mlimani city na kula yule sister wa kanisa la ubungo makoka nae aliuwawa pale ubungo wakati fulani baada ya kutoka hapo mlimani city -

tuwe makini sana
haha benkizote

use simba banking.tigopesa.mpesa..nk
 
hao washikaji unawachukua wanini? wakubebe utakapo dondoka kwa pressure baada ya kuibiwa au? maan sidhani kama wana msaada wowote kwakuwa majambazi wanakuja na bunduki washikaji zako watakuja wamebeba galaxy na iPhone tu

Ha ha ha ha haa washikaji viduki
 
ilishawahi kunitokea mimi palepale mlimani city mwaka jana,nilichukua kiwango kikubwa tu cha pesa pale NMB,kabla sijatoka nje nilihisi kulikuwa na watu walikuwa wananifuatilia,nilirudi haraka na nikazi deposit kwenye account yangu ya CRDB palepale.Tuwe makini jamani, unaweza poteza uhai

Miezi miwili iliyopita kuna ndugu yangu nae walimchomea naada ya kuchukua fedha nyingi ila yy aligundua fika mlinzi ndio alimchomea
 
Hameni bank za kuchukulia pesa sio lazima mcity. Kuna matawi udsm au mjini kabisa
 
ukichukua pesa zaidi ya milioni tatu unashauriwa uchukue escort ya polisi.

tumieni cheki na miamala ya simu ktk malipo.
 
Bank za mlimani city ma Teller wanashirikiana na majambazi
 
Mtawasingizia mateller but in reality teller awapo kwenye cube huwa hana kitu chochote cha kumsaidia kuwasiliana na mtu alie nje au ndani ya banking hall!

Katika benki teller ni mtu alie busy saana kuliko wafanyakazi wote ndani ya benki.

Mbona tunawaona wakipiga simu na kupokea?..sasa hapo Si ndipo wanapowapigia?..
 
Back
Top Bottom