Tuwe makini na pombe, zinaua

Smart Contract

JF-Expert Member
Sep 24, 2014
1,018
2,407
Wasaalam, mnamo mwaka jana X Mass nilikunywa sana mpaka ikanipelekea kupata ulcers hivyo 25/12 na 1/1 ziinikuta kitandani naugumia maumivu nikajiapiza naachana na mipombe kali. Lakini nilivyopata nafuuu nikarudi tena.

Mwaka huu juzi 25/12 na 1/1 nazenyewe nimezilia kitandani the same case kama mwaka uliopita lakini nilipopata nafuuu nikaendelea tena.

Ila kilichonitisha juzi kati kaja balozi wa mtaa anachangisha rambirambi, nikatoa ila sikumuuliza chanzo cha kifo baadae niko kijiweni ndo washikaji wanasema huyu mtu alikufa kwa sababu ya pombe kali hawajamalizia hiyo story napewa taarifa mshikaji kuna mwingine tena huyu nimewahi kunywa nae mtaani kwangu kwa zamani naambiwa na yeye amekata moto kwa sababu ya vikali. Wakuu nimeogopa yaani bapa lote nilokunywa lilikata.

Kwa moyo wa dhati mi nimeamua kupunguza hii mikali japo bia siziwezi ila napunguza hii mikali taifa bado linanitegemea.

Na nyie nawaasa kama unapenda mikali hakikisha unakula vizuri japo hata huyo aliyekata moto alikuwa vizuri kiuchumi na hela ya kula hawezi kosa lakini ndo hivyo tena.
 
Kunywa pombe (kali) hapa Bongo ni hatari sana. Kuna breweries bubu kibao huko mtaani kama hawa jamaa waliokamatwa mwaka jana huko huko Dar.

Unaambiwa baadhi ya ingredients wanazotumia ni pamoja na maji ya betri na dawa za kuulia wadudu. Hapo kuna figo na ini litakalosalimika kweli?

TBL tayari wameshasema kuwa wanapunguza uzalishaji wa Konyagi kwa sababu soko limejaa Konyagi feki. K-Vant pia. Na mamlaka ni kama vile zimezidiwa au hazina nia ya kufuatilia. Au si ajabu ni project za wakubwa. Hatari sana!

IMG-20231230-WA0077.jpg
IMG-20231230-WA0079.jpg
IMG-20231230-WA0080.jpg
IMG-20231230-WA0081.jpg
IMG-20231230-WA0083.jpg
IMG-20231230-WA0082.jpg
IMG-20231230-WA0084.jpg
IMG-20231230-WA0085.jpg
 
Na nyie nawaasa kama unapenda mikali hakikisha unakula vizuri japo hata huyo aliyekata moto alikuwa vizuri kiuchumi na hela ya kula hawezi kosa lakini ndo hivyo tena.
Kuna jamaa alifariki Mwaka Jana Mwezi wa kwanza kisa visungura, sasa hivi ametulia zake kwenye udongo amepiga usingizi mrefu sana anakoroma huku anakula udongo na kuliwa na mchwa
 
Jamaa yangu alitapika damu kwenda hospital ni vidonda vikali vya tumbo!
Akaapa kwamba anacha pombe kali😂😂😂 ndo kaongeza mwendo...

Chakula anakula kwenye vibakuli!!

Dokta jirani tumemsafirisha mwezi uliopita kwenda huko Kanda ya kati,pombe kali ilimtoa uhai. Kaacha watoto na mjane mnono sana
 
Kunywa pombe hapa Bongo ni hatari. Unaambiwa baadhi ya ingredients wanazotumia ni pamoja na maji ya betri na dawa za kuulia wadudu. Hapo kuna figo na ini litakalosalimika kweli?

View attachment 2868102View attachment 2868103View attachment 2868104View attachment 2868105View attachment 2868106View attachment 2868107View attachment 2868108View attachment 2868109
Dah bora Local zetu tu, gharama ya kufoji bia ya local inaweza ikawa alfu tatu kwa bia moja, wakati bia orijino inauzwa elfu mbili, nani atengeneze fake sasa wakati hakuna upungufu wa bia local, all year around .
 
Jamaa yangu alitapika damu kwenda hospital ni vidonda vikali vya tumbo!
Akaapa kwamba anacha pombe kali😂😂😂 ndo kaongeza mwendo...

Chakula anakula kwenye vibakuli!!

Dokta jirani tumemsafirisha mwezi uliopita kwenda huko Kanda ya kati,pombe kali ilimtoa uhai. Kaacha watoto na mjane mnono sana
Noma sana pombe kali ni kali kweli
 
Wasaalam, mnamo mwaka jana X Mass nilikunywa sana mpaka ikanipelekea kupata ulcers hivyo 25/12 na 1/1 ziinikuta kitandani naugumia maumivu nikajiapiza naachana na mipombe kali. Lakini nilivyopata nafuuu nikarudi tena.

Mwaka huu juzi 25/12 na 1/1 nazenyewe nimezilia kitandani the same case kama mwaka uliopita lakini nilipopata nafuuu nikaendelea tena.

Ila kilichonitisha juzi kati kaja balozi wa mtaa anachangisha rambirambi, nikatoa ila sikumuuliza chanzo cha kifo baadae niko kijiweni ndo washikaji wanasema huyu mtu alikufa kwa sababu ya pombe kali hawajamalizia hiyo story napewa taarifa mshikaji kuna mwingine tena huyu nimewahi kunywa nae mtaani kwangu kwa zamani naambiwa na yeye amekata moto kwa sababu ya vikali. Wakuu nimeogopa yaani bapa lote nilokunywa lilikata.

Kwa moyo wa dhati mi nimeamua kupunguza hii mikali japo bia siziwezi ila napunguza hii mikali taifa bado linanitegemea.

Na nyie nawaasa kama unapenda mikali hakikisha unakula vizuri japo hata huyo aliyekata moto alikuwa vizuri kiuchumi na hela ya kula hawezi kosa lakini ndo hivyo tena.
Mimi pia Kuna ndugu yetu alifariki sababu ya unywaji pombe na alikua bado kijana mdogo
 
Back
Top Bottom