Kikubwa tufikie hatua tukubali kuwa hapa JF tupo watu wa aina tofauti tofauti na siku zote mtu usiemjua usijiwekee expectations kuwa huyu yupo hivi ama vile.
Hapa tupo watu wa aina tofauti sana kuanzia umri, tabia, nia na malengo ya kuwepo, wasomi, wasiosoma na aina nyingine tofauti kabisa.
Kuna wengine humu ndani sio watu huwezi kuamini. Yaani sio binadamu kama ID zinavyoonyesha na jinsi tunavyo interact nao.
Chamuhimu ni kufuata wewe kilichokuleta.
Kama umefata papuchi wewe mwanaume alafu ukakutana na mwanamke aliefata nae mambo hayo mkazinguana huna haki ya kumsema mwenzako vibaya maana na wewe ndio wale wale tu.
Mtu unajisifu umetongoza wanawake kibao JF alafu unaanza kutaja tabia zao kwa kuwachafua bila kujiangalia wewe kama usingekuwa mchafu ungezijuaje hizo tabia chafu za hao wanawake?
Ungekuwa sio mhuni na mzinzi ungetongoza vipi hao wanawake wote na kujua tabia zao.
Nasikiaga mnasema 'nyani haoni kundule' sielewagi maana yake!
Sent using
Jamii Forums mobile app