Tuwasamehe wanaume wanaochukia wanawake humu

Tuwasamehe wanaume wanaochukia wanawake humu

Status
Not open for further replies.
Wengi wameumizwa kihisia
Aidha walitelekezwa na mama zao wakiwa watoto,ama waliumizwa na wapenzi wao waliowapenda na kuwaamini.

Wamejeruhiwa so wametengeneza chuki na kila mwanamke ama jinsia ya kike .Ni wagonjwa wa kiakil bila kujijua.Wasamehe na uwaombee huenda wakapona siku moja.

Wanadhihak wanawake na kuwadharau wanasahau ni kupitia hayo maumbile ya mwanamke walikuja duniani.Hata uyatukane maumbile ya mwanamke vipi ama umdhalilidhe vipi atabaki kuwa mwanamke na msaidizi wa muumba katika uumbaji.

Mungu alimuumba mwanamke ili akasaidie kazi ya uumbaji na jukumu hilo haliwezi badilika kamwe na umuhimu wa mwanamke utabaki enzi na dahari.

Wengi utawatambua kwa comments na mabandiko yao hapa jf,wanastahili kuonewa huruma na ikibidi kupatiwa msaada wa kisaikologia.

Sihitaji kuwataja wanajijua and nashauri its about time watafute msaada wa matibabu,tuna wataalamu wengi wa magonjwa hayo kwenye hospital zetu zote kubwa nchini Tanzania.

Mwisho niwape moyo wasichana na wanawake wenzangu msivunjike moyo.we we ni kiumbe wa pekee na uliletwa duniani kama mwanamke kwa sababu.Una nguvu kama malkia esta,kama Eva/hawa,Mariamu mama yake Yesu,Malkia wa Sheba na wanawake wote mashujaa wa enzi na enzi.Wewe ni dhahabu maneno hata kwenye kanga yapo.Hakuna mtu wala maneno machafu ya mtu ya kukushusha isipokuwa wewe mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Happy New year dear

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ndio maana nilishawahi kushauri PM zifungwe tu,lol...kwa kweli saa nyingine yanayoendelea humu mpaka unajiuliza kuna watu au mazimwi tu ndio yanatype? 😀😀😀😀,nina mapungufu yangu ila huku kuna watu huku wako heartless.....wamefanya watu genuine kukosa chance ya kuform relationship humu,kila mtu anakaa juu juu tu,kuhofiwa kutundikwa hapa jamvini… 😀😀😀
Nikushauri tu Becky, ukiwa humu Jamii Forums learn to lower your expectations hata umuone mtu yuko vipi au anasifiwa vipi.
Umeenda mbali sana umewasiliana naye PM au kwenye E-Mail, nje ya hapo kama unataka mpenzi bora uende kwa Mwakasege.
 
Mwanzoni ninavyijiunga na huu mtandao nilikuwa sichukuliia maisha ya hapa jukwaani kivileee. Lakini bahati mbaya nikaja kujua kwamba kumbe kuna watu hapa Jamii Forums ndiyo wamefika na kila jambo wanalolisema huwa wanalimaanisha. Sasa asilimia 70% ya wengi wa wanaochukiwa humu ndani na kudhalilishana ni wale waliojitakia wenyewe kwa kukosa umakini au kuendekeza tabia za uswahili uswahili. Nasema ni heri mtu aje atukane wanaume wote tu au wanawake wote, lakini siyo aje aanze kukusakama wewe peke yako. Mara zote matusi ya hapa jukwaani huwa yanaanzia huko PM hasahasa baada ya kutongozana au kukutana uso kwa uso.
Nakazia tuu...humu kuna watu kuumizwa ni haki tuu kwao asee,.kuna watu waswahili saaana si wanaume si wanawake tena nikisema uswahili ntakuwa nakosea ni WASHAMBA na MALIMBUKENI wa maisha acha wavune walichopanda,.
 
Wanawake ni mama zetu, shangazi zetu, dada zetu, wake zetu, watoto wetu na wajukuu zetu. Tuwapende tu hakuna namna bado sifikiri itatokea vita kuu ya dunia ya kijinsia yaani wanawake na wanaume. Tupendane tu, ukiwa mwanamke ukinipenda usisite kuja PM
[emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni ile mweshimiwa tupunguze Kuunda Tume ni hasara na majibu ya Hayana tija.
Hayaa nimesikia maonini yako ntayafanyia kazi kuunda Tume kuyachunguza.
Kazi kweli kweli,

Dada kaleta Uzi kuwatetea na kusaidia kuheshimisha Wanawake kadunda Watu wanazidi kuwapaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi huwa sipendi kabisa kuwa ongelea wanawake vbaya kwa sababu " katika vijiutafiti vyangu nilivyo vifanya nimebaini kwamba hata sisi wanaume huwa tuna changia kuwa haribia maisha yao nakuwaingiza katika aina ya maisha ambayo hayastahiki wao kuwa nayo

Katika umri huu nilionao ambao naweza kusema ni wa-wastani " nimeshaona wanawake wengi sana wakipitia tabu na majuto ambazo nyingine zilisababishwa na sisi wanaume iwe ama kwa makusudi au bahati mbaya..

Nimeshaona " mabinti wakipewa mimba halafu wakaishiwa kutelekezwa " nimeshaona " vibinti vidogo vikiolewa na wazee " nimeshasikia mabinti wadogo wakibakwa " nimeshaona wakikatishwa masomo na kunyimwa haki yao ya msingi ya kuelimika nkwa chagizo tu la Jamii yetu wanaume kuamini kwamba mwanamke hafai kuelimishwa " tutapoteza pesa "

Nimeshaona wanaume tukitumia pesa kwa minajili ya kuwa honga marafiki wa wake zetu/gf zetu ili wawasaliti marafiki zao natupate kushiriki nao kingono

Achilia mbali rushwa za ngono vyuoni na makazini " (ijapo kuwa kuna wanawake ambao nao huwa wanataka rushwa hiyo toka kwa wanaume ) lakini wahanga wakuu katika hili huwa ni wanawake "

Sehemu kubwa pia ya watawala wa huu ulimwengu ni wanaume " mara nyingi " tunapo leta machafuko duniani " Huwa tunawaingiza wanawake na watoto Katika tabu kubwa na mateso " wakati hata hawakuwepo wakati machafuko hayo yanapangwa kufanyika na kama walikuwepo basi ni wachache " ..so bado hatuwezi kukwepa hizo lawama ".

Hizi ndio sababu ambazo huwa zinanifanya nisi wakashifu Wanawake kwa sababu huwa natambua kwamba " sisi huwa tunachangia sana " kuwafanya wawe watu wa hovyo " mpka kufikia hatua ya kuwaona kuwa hawafai "


Licha ya hivyo pia " nyinyi wanawake " mnapaswa kukaa chini na kujiuliza kwanini kila siku msemwe nyinyi tu " msiwe mnachukia kusemwa tu " hamuwezi kuwa mnasemwa bila sababu " je mlishawahi kutafuta suluhisho la hayo matatizo yanayo fanya msemwe " nakuonekana kuwa hamfai " !!!?

Au mnaishia kulalamika ili muonekane kwamba mnaonewa " huku mkisahau ule msamiati unaosema kwamba lisemwalo lipo "



Sent using Jamii Forums mobile app

Msalimie shemeji mkuu
 
Sisi wenye wanawake single mother hizi komenti zinatuumiza sana mkuu wakuu hawajui Tu
Aahh " kuwa na mwanamke single mother sio laana " mama yangu alilelewa na baba wa kambo " na mpaka leo hii huwa anamuona ni shujaa wake " ....

so kama mama yangu anautambua mchango wa baba yake wa kambo " mimi ninani hasaa ni shindwe kuutambua mchango wa mwanamke ambaye ni kama single mother "

Ina maana jamii yetu haina kabisa wanawake ma-single mother ambao wana hekima utii na busara ..sitaki kuamini kuhusu hilo ... kuna wanawake wengine wamekuwa ma- single mother baada ya kubakwa wakashika mimba _ na wengine ni wajane waliofiwa na waume zao " ... sio kila single mother aliwahi kuwa malaya ndio akapata mtoto "



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rebbeca,tuwe wakweli dada angu,una mtoto wako wa kiume Ana miaka 27,anakwambia mama nataka kuoa,then anakuletea mwanamke tayari Ana watoto wawili ambao sio wa mwanao???lazima uwe surprised na kuhoji,

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanawake akili zetu tunazijua wenyewe unakuta mama anasomesha wanae wa kike shule za gharama Ila hataki watoto wake wa kiume waoe wanawake wasomi au wenye pesa kuwazidi watoto wake Dunia haishi vituko kikubwa tuvumiliane tu.
 
We single mother wa hum Jf ulichomfanya huyo kijana wa watu Mungu atalipa. Sio vizuri umemfanya mtoto wa mwanamke mwenzio kawa kama kichaa anaweweseka tu

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Hawajui single mother hawanaga muda wa kudeal na bs. Akikutapika utalia lia kama hawa tunaowaona huku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ecclestiastes 9:5 - 'The Dead Know Nothing'

Badala ya kukaa na kutafakar ni mabadiliko gan myafanye ili yawape Heshima humu........ Bado mnaendelea kujifariji ?

Ukiwa Singo mama, ni singo.mama tu..ukiwa Hujaolewa na Umri umeenda itabakia ivo tu..... Ukiwa Unatabia alizosema ndugu GuDume unazo tuu.
...after all mtu hawezi kutoka kusikojulikana kuja kusemea Tabia zako ambazo wewe mwenyewe hujawah kuzidsclose au kuzifanya.

Ivo basi,ni wazi kua Yanayosemwa humu yapo na uanatendeka sio visa vya kubuni wala kusadikika.

Msipende kusifiwa upande mzuri tu..ifike mahali, angalieni huo upande mnaouchukia kisha muutumie kama Fursa ya nyinyi kufanyaa mabadiliko..


Basi angekua ni mmoja basi tutasema anachuki nanyinyi za kibinafsi..LAKINI NI WENGI SANA, nakila siku yanakuja mapya....

Inamaana wote hao wanawachukia ??? Wamelelewa vibaya ???

Endelea kujifariji nakutiana upofu ambao utazidi kuwafanya msiondoe badiliko la mioyo yenu. Na kwanmaana iyo Tegemeen hayo kila siku kwakua watu ni walewale namaisha niyale yale

...mbona masingo mama wengi wanaolewa????? Nikwann Wahumu tu ndo msemwe???

Kuna singo maza mmoja, kaniPM minamba yake kwa ID hii, sijakaa kidogo ID ingine inaniPM kwenye ID yangu ingine tena anajitongozesha uko na namba akaaacha mbaya zaidi anasema " Mimi najua una mtu ila utanipa pesa kidogo kisha tutombanee"

Huyu wa aina hiii unamuweka kundi gani??? Dem una ID nyingi, unazunguka humu kutafuta Ujinga tuuuu mpaka unajigonga mara mbili kwa mtu??? ( mpaka sasa anajua sijajua, ila ukimya wangu umeshampa jibu).



SIKILIZENI, HATA MKIJIFANYA HAMUELEWI ,OOHOOOO SIJUI NN, UKWELI UTABAKI KUA UKWELI NA UTASEMWA TU INGAWA UTASEMWA NA WATU WACHACHE WASOTAFUTWA KUPENDWA !!!

INTERESTING......soma unielewe….

issue sio single mazas,

issue ni wewe kila siku ukiona topic ya wanawake...iwe single mazas,wasioolewa etc lazima uingie na kuponda...

Kama kigezo ni heshima mtu akiolewa kabla hajazaa,wengine sio kigezo..usilazimishe watu kufanana...

ni kweli humu masingle mazas wanalaumiwa na watu wengi wanawaponda,

ila kwa mtu makini atakua kashagundua kuwa kuna maprofile yako peculiar....

ikija kusigina wanawake,lazima huyu mtu yumo….

mpaka imekua common,tukiona topic inaponda wanawake,tuna expect Fulani lazima ataandika tu mashudu yake kwenye hii topic..

na inakua kweli...


(Halafu nilikukutaza kujibu posts zangu,sijibugi posts zako, (I will appreciate kama hautajibu tena topic yangu)
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom