Tuwakumbuke waandishi wetu wa Riwaya

Song of Lawino
Trial of Brother Jero
Things Fall Apart
Three Suitors One Husband
Is it Possible?
Masimulizi ya Alfu Lela Ulela
Kuli

na hivi mnavikumbuka?
Safari ya Bulicheka
Someni Bila Shida
 
Song of Lawino
Trial of Brother Jero
Things Fall Apart
Three Suitors One Husband
Is it Possible?
Masimulizi ya Alfu Lela Ulela
Kuli

na hivi mnavikumbuka?
Safari ya Bulicheka
Someni Bila Shida

Mine boy,
Hekaya za abunuwasi
 
Mimi niliwahi kuagiza vitabu vya Alfu Leila U Leila na vile vya Bwana Msa, kutoka kampuni za uchapishaji Nairobi Kenya.

Labda mnaweza kujaribu uko.
 
Mkuu katika watunzi ambao walikuwa sipendi kusoma vitabu vyao basi huo niliye mkoza hapo juu, alikuwa mmoja wapo... Sababu alikuwa ananakilii neno kwa neno kutoka kwenye vitabu vingine vya kiingereza.
 
Mkuu katika watunzi ambao walikuwa sipendi kusoma vitabu vyao basi huo niliye mkoza hapo juu, alikuwa mmoja wapo... Sababu alikuwa ananakilii neno kwa neno kutoka kwenye vitabu vingine vya kiingereza.

Ni kweli, vile vya baadaye alipoanza kuandika mambo ya upelelezi na ujambazi alikuwa ananakili. Lakini vya mapenzi alivyotoa mwanzo vilikuwa vizuri tu hasa kama hicho cha kivumbi uwanjani na je kweli unanipenda.

Kulikuwa na mwandishi pia aliitwa Nico ye mbajo, ulimsoma huyo?
 
Mimi niliwahi kuagiza vitabu vya Alfu Leila U Leila na vile vya Bwana Msa, kutoka kampuni za uchapishaji Nairobi Kenya.

Labda mnaweza kujaribu uko.

Vipo Dar, mtaa wa samora. Hata bulicheka na abunuwasi
 
1. Salam toka kuzimu
2. na ile hadithi ya baba naye anataka kuna mtu anaikumbuka
:smile-big:
 
duh.. kweli ndio mtu unajiona mzee hivi hivi!

Siku hazigandi,

Vitabu vyote hivyo vinavyotajwa hapo ninavyo huko nyumbani ila sijui kama bado viko salama. Ni pamoja na vitabu vya James Hadley Chase, Nick Carter, Denise Robins, Agatha Christie ma vinginevyo vingi vya riwaya za kiswahili na kiingereza. Ngoja niwakumbushe riwaya hii:


Bulicheka alikwa mwalimu wa shule ya Kilakala. Siku moja akamwambia mke wake Lizabeta, tufunge safari tuweze kuiona dunia. Lizabeta akajibu, ukitaka kufunga safari uone dunia nzima, nenda peke yako, mimi siendi. ......

Zaidi ya david Mailu, hapo afrika ya mashariki kulikuwa na mwandishi mwingine kutoka uganda ambaye naye alikuwa akiandika vitabu erotic sana. Character wake mmoja alikuwa akiitwa Matama; kwa bahati mbaya sasa hivi sikumbuki jina la mwandishi huyo tena.
 

Niliwahi kusoma kimoja cha huyo mganda, unfortunately nimesahau jina la mwandishi. Kilikuwa kizuri.

baadhi ya vitabu vya Nick Carter ndio vilikuwa vinatoa stori za willy gamba kwenye vitabu vya Musiba.

Kulikuwa na kitabu cha Denise Robins kinaitwa "two loves", ilikuwa ni story sana nzuri ya mapenzi-ambapo bondia pamoja promoter wake walimuoa mrembo mmoja bila wao kukijijua kwa siku kadhaa..., ila sikubahatika kuviona vitabu vyake vingine.

Je yule mtaalam, Harold Robbins ulivisoma vitabu vyake?

Vitabu vya Agatha Christie James Hardley chase sasa hivi vipo madukani ila vijana wa sasa hawavisomi, wanasoma stori za shigongo, poor them!
 
Sultani akakubali.
Akamchinja mbuzi,
naye mbuzi akanywa maji,
nayo yakazima moto,
moto ukaichoma fimbo,
nayo ikampiga mbwa
mbwa akamuuma kalume-kenge
naya kalume-kenge akaenda shule
 
1. Mazungumzo ya Alfu-lela-ulela, au Siku elfu na moja.

Kimefasiriwa kwa Kiswahili na Edwin W. Brenn na kuhaririwa na F. Johnson

2. Lila na Fila - Kiimbila
3. Ubeberu Utashindwa - Kiimbila
 
Riwaya ya KULI Shafi Adam Shafi


shida mtunzi ndyanao balisidya

Duh! mkuu umenikumbusha form four pale kibasila, 1997!!
Kwenye hicho kitabu kuna sehemu muhusika mkuu anaeitwa chonya alikuwa akitoa msaada kwa mtoto aliyegonwa na gari. Chonya alisema, "I am taking this boy to the hospito, if police men come tell him me chonya of chilonywa", kwa lafudhi ya kigogo. Katika mtihani mmoja wa kiswahili kulikuwa na swali lililotaka wanafunzi wamchore chonya, kwa maana ya kutoa wasifu wa chonya. Basi kuna mwanafunzi mmoja aliamua kumchora kwa kutumia pencel, hakuelewa swali!
Tuliosoma vitabu vya zamani tulifaidi sana, sijui wakati huu mambo yakoje!



......... Mbona vya Eric mie vinanishinda !? :smile-big:

Unakusudia eric shigongo???!!! Lakini shigongo ni mwandishi wa juzi juzi tu!!! Mi nadhani mtoa mada alikusudia tuwakumbuke waandishi wa zamani!!

Hivi hawa watoto wa siku hizi wanasoma vitabu gani?

Watoto wa siku hizi wanahifadhi nyimbo katika vichwa vyao, muda mwingi headphone masikioni mwao, wanajaza ujinga.

duh.. kweli ndio mtu unajiona mzee hivi hivi!

Mzee ukiona hivyo ujue ndo utu uzima unakufuata, mda si mrefu utaitwa babu na kutembelea mkongojo.
 

Duh! mkuu umenikumbusha mbali kidogo!!! Nilisoma kitabu cha usiku wa balaa, nakumbuka nikiwa standard 4 mwaka 1990, kabla ya akina mzee ole kuingizwa katika gazeti la sani. Usiku wa balaa ilikuwa ni hadithi ya kutisha sana, nakumbuka jinsi nilikuwa nikipatwa na hofu na moyo kunienda mbio wakati wa usiku nilipokuwa nikisoma kitabu hicho.

Kwa upande wa vitabu vya kipelelezi, mie nilikuwa navipenda vitabu vya mpelelezi joram kiango. kwa kweli zamani tulifaidi sana na tulikuwa tunapenda kusoma.
 



CHACHAGE
Makuadi wa Soko Huria

Gabriel Ruhumbika
1. Janga Sugu la Wazawa
2. Miradi Bubu ya Wazalendo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…