Tuwakumbuke waandishi wetu wa Riwaya

Musiba na willy Gamba "wake" alitukamata sana wengine miaka ile,mpaka eti tukawa tunamtengeneza willy gamba vichwani mwetu kwamba ni kijana fulani mtanashati hivi..shushushu hatari mwenye uwezo wa hali ya juu wa sanaa za mapigano.Nakumbuka willy gamba na ushujaa wake kwenye vitabu vya Elvis Musiba kama:

Njama
kikosi cha kisasi
Hofu
etc

LOL! Kufa na Kupona = Live and Let Die ?
 
Mpenzi, Kitanda cha mauti - KAJUBI MUKAJANGA
Makuadi wa Soko huria - SEITHY CHACHAGE
Gamba la Nyoka - Euphrase Kezilahabi
Nyota ya Rehema - Mohamed S. Mohamed
Doa Jeupe - Comrade Companero
Miradi Bubu ya Wazalendo - Gabriel Ruhumbuka
Mukwava wa Uhehe - Mugyabuso Mulokozi
Kumbatio la Mwenye Makosa - Mzee Mwanakijiji
 
Aisee ni kweli kuwakumbuka lakini cha kusikitisha ni kwa nini baadhi ya vitabu vilifungiwa au kuondolewa kwenye mtaala? kimtindo naona kama sio sawa... naomba mnisaidie wakati tunawakumbuka tutafakari na hilo jamani AU?
 
Vitabu ambavyo viko katika hazina yangu. TUTARUDI NA ROHO ZETU?, ROHO YA PAKA, SALAMU TOKA KUZIMU, MALAIKA WA SHETANI, PESA ZAKO ZINANUKA, LAZIMA UFE JORAM, DIMBWI LA DAMU vya BEN MTOBWA..NJAMA, KIKOMO, KIKOSI CHA KISASI vya ELVIS MUSIBA pia ninacho MASHIMO YA MFALME SULEIMAN. Na KIJASHO CHEMBAMBA, JOGOO LA SHAMBA NA MSAKO WA HAYANI vya EDIE GANZEL. Watunzi wote wazuri wamesha fariki.

mkubwa tuazime jamani!ntakupm
 
Hapa ningependa kumtambua Mtunzi na mfanya biashara maarufu sana kule kanda ya Ziwa.
Elistablus Elvis Musiba. yeye alitunga vitabu hivi
1. Kikosi cha kisasi
2. Njama
3. Kikomo
4. Hujuma.
 
Mzimu wa Watu wa Kale, Kisiwa cha Giningi, Duniani Kuna Watu, Siri ya Sifuri, Mke Mmoja Watume Watatu, Mwana wa Yungi Hulewa, By Muhammed Said Abdulla

Umenikumbusha mbaaali sana kuhusu mtunzi huyu Ammi Moh'd.

Hakika asiyesoma vitabu vake basi amekosa mengi sana. Siku zote nilikuwa namfananisha na Marhum Shaaban Roberts.
 
Umenikumbusha mbaaali sana kuhusu mtunzi huyu Ammi Moh'd.

Hakika asiyesoma vitabu vake basi amekosa mengi sana. Siku zote nilikuwa namfananisha na Marhum Shaaban Roberts.

His books are splendid and heartwarming...!
 
Mkuu hivyo vitabu vyote nilivisoma ndugu yangu... Mimi nilikuwa msomaji mzuri sana wa riwaya, na kwa bahati nzuri nilipokuwa shule ya msingi nilikuwa ndio mtunza maktaba ya shule, na Alhamdulillah shule niliyo soma ilikuwa na vitabu vingi sana, nadhani robo ya vitabu viliishia home kwangu... ah ah ah ah.

Nadhani tabia ya usomaji vitabu nimerithi kwa mzee wangu. Home kulikuwa na Novel za aina nyingi sana, nami nilikuwa siishi kumsumbua anisomee...! Na si vitabu tu hata nikiokota vijarida uko nje basi ilikuwa lazima nikipeleke home aidha mama au baba wapate kunisomea.... Hii ilipelekea nipelekwe shule ya vidudu kabla ya umri wangu kufika na ikasababisha mimi kujua kusoma haraka sana.

Kumbe ndiyo maana ile shule ina upungufu wa Vitabu !!Unaonaje ukivirudisha Mkuu? aha aha aha. utani tu
 
Wakati titi la Nyati, hukamuliwa kwa shaka.
Wakati mwana Banati, waendao wana shaka.

Wakuu wenye kukumbuka ,tafadhali naomba mniwekee beti mbili tatu za Shairi hili
 
Shaaban Robert
1. Adili na nduguze
2. Kusadikika
3. Kufikirika
4. Maisha yangu na baada ya miaka 50

JOMSSI(John Msimbe Simon Simbamwene)
vitabu vingi tu vya kamanda shupavu Inspecta Fog

TV zimeua kabisa utamaduni wa kupenda kusoma, zama hizo tukishindana idadi ya novel ulizosoma mfano nakumbuka nikiwa form three, Tanga School back in 1993, nilisoma novel kubwa about 600 pages in less that 4 days, novel yenyewe ikiitwa Kane and Abel.

Siku hizi wenetu wanashindana kwa idadi ya movie walizoona katika TV na video plus kama unaweza kuchezea playstation na other video games, badili ya kucheza soka uwanjani siku hizi inachezewa kwenye video!!!

kweli wakati umebadilika!!!!
 
.... KIJASHO CHEMBAMBA ! ................... Eddi Ganzel
Kabla sijaanza kusoma 'novel' za kiingereza k.m. James Hadley Chase na Nick Carter, huyu mwandishi mzalendo alikuwa ananivutia sana na hadithi zake hasa zile zilizokuwa zikitoka gazetini (sikumbuki ni gazeti gani). Kuna hadithi yake ilikuwa inasimulia kachero mmoja aliyekuwa anapambana na kundi la majambazi yaliyokuwa yanaitwa 'Vinyamkela'. Nilikuwa najificha chumbani ili nisome hizo hadithi bila bughdha, na mara nyingi tu nilikuwa natafutwa sionekani, hasa wakati wa chakula, kumbe nasoma hadithi za kusisimua za 'Vinyamkela'. R.I.P. Eddie Ganzel, you really made my days!
 
Dadi Athumani katunga vitabu vitamu kama 1. MAPUTO 2. OPERESHENI VIPUSA. Msisahau vitabu kama: Mirathi ya Hatari, Njozi Iliyopotea,Pandu, Akuanzae Mmalize, Mbigili Tupu,Bwana na Bibi Myombekere, Kamlete,Akibisha Mlipue, Mashimo ya Mfalme Suleiman, Najisikia kuua tena, Mashetani, Nchi ya Wazuvendi, Miradi Bubu ya Wazalendo, Janga sugu la Wazawa, Harusi, Asali Chungu,Sitaki Sijavunja ungo, Kuli, Kasri la Mwinyi Fuadi, n.k.
 
Kwa kweli leo nimejisikia furaha sana, kukumbuka na mimi enzi ninakua maana nami ni mpenzi wa vitabu. Nyumbani tulikuwa wa vitabu vingi vya hadithi na vilivyonigusa ni mfano Nyota ya Rehema, Kasri ya Mwinyi Fuad na pia hadithi za Ben Mtobwa. Pamoja na gazeti la sani enzi hizo.....

Nakumbuka pia hadithi za alfu lela ulela, niliona mara ya mwisho Walter Bgoya ametoa machapisho mapya ya hizi hadithi nadhani waliokuwa wanaulizia wanaweza kupata ila sijui ikiwa wana duka maalumu wanakouzia vitabu vyao.

Katika moja ya interview zake pia anaongelea ugumu wa uchapishaji wa vitabu Tanzania na kukosa kwa wanunuzi. Wakati ninakua maktaba pale nilikuwa ninaishi walikuwa na vitabu vingi pia mara moja kwa wiki walikuwa na ukumbi ambako mmoja wa wafanyakazi alikuwa anasoma hadithi kwa watoto wa chekechea na shule za msingi.

Huu utaratibu sijui kama bado unaendelea.
 
Back
Top Bottom