OleWako
Member
- Sep 7, 2021
- 6
- 9
Ukipanda daladala unaweza kugundua jambo lilelile kila siku: kila daladala inapofika kituo chenye watu wengi mlango umeshazibwa na watu ambao hawawezi kusubiri kupambana kwa vile viti vichache. Mara nyingi watu wanapandaga hata kabla ya watu wote kushuka.
Aidha makondakta wanachangia kuongeza kero wakirudisha change mbele ya mlango kusababisha watu wanaosubiri change kuziba mlango. Hivi vitendo ni kero kwa watu wanaoshuka lakini pia inawachelewesha watu wote wanaotumia daladala pamoja na kuwa hasara kwa wazee, wagonjwa, wajauzito, nk. ambao hawana nguvu ya kupambana kupanda daladala.
Suluhisho ni rahisi: tuache ubinafsi na tuongeze utulivu.
Tuwape watu nafasi ya kutosha kushuka na kutoka halafu tukipanda tuheshimu wenzetu. Mwisho wa siku ni faida ya sisi wote; wanaoshuka wanaweza kushuka chap na bila kero na wanaopanda wanaweza kuwahi kupanda kuliko wakipanda kwenye ile fujo inayotokea mlango ukizibwa.