Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam haya ndiyo yatakayokutia doa hapa Mbezi Luis Stend ya daladala

Annie X6

JF-Expert Member
Mar 16, 2023
405
751
Niende kwenye hoja Moja Kwa moja.

Hii stend itakuja kusababisha mauaji na viongoz kuanza kujitetea kwa kuleta sababu na matetezi.

Hizi ngaz kiunganishi cha vituo viwili vya daladala. Watakuja kufa watu. Mungu aepushie mbali. Mh charamila mkuu wetu wa DSM una viongozi wasiojali utu wa watu.

Kwa hakika ni suala la utambuzi tu. Lawama zielekee kwa.

1. Afisa mipango wa manispaa ya Ubungo.

2. Afsa usalama wa ukanda huu.

3. Mkuu wa wilaya hii.

Yaani Mh mkuu wa mkoa Hawa watu wanakutia aibu.

Kero zilizopo hapa ni
1. Kuzuia njia, hapa wamejaa wachuuzi... No sawa wanafanya jambo zuri tuu kutafuta riziki.. lkn sio kwa mpangilio.

2. Kuna msongamano sio mkubwa TU it's a huge group. Wamo wagonjwa, wajawazito, watoto wadogo, wazee lkn ghafla wakitokea watu wajiji wanapowafurumusha wachuuzi ni kuangshana na kuswagga meno. Hii haikubaliki hata kidg na si ustaarabu.

3. Yapo makundi makubwa yenye madhumuni tofauti hutumia ngazi zile. Wapo wanaokwenda kupanda daladala TU, na wapo wanaouza, wapo wanaonunua TU. Ni kero kubwa sana hapa. Na Kwa watu walioshuhudia DSM ya miaka ya enz hizo, ni zaidi ya mtaa wa Kongo.

Ushauri kwa
1. Viongozi angalieni hili. Anzisheni ngazi zingine hata zikiwa tatu kwa ujumla. Wekeni permanent security kwa mf askari.

2. Watuamiaji kama hununui kitu epuka kutumia ngaz zile. Utaumizwa.

Manispaa. Kitengo cha ustawi wa jamii ubungo manispaa wale wenzetu wenye mahitaji maalum (ulemavu) wasaidieni watoke pale. Wataumizwa wapate ulemavu mengine.

Wasomi na wanajamii wasamalia wema. Mnapoanzisha foundation hembu hapa naona kuna gape. Hawa wanatakiwa wapate misaada.

Mwisho anzisheni malipo ya kupita kule japo 200 Ili kupunguza wapitaji wasio na ulazima. Na Ndg Mkuu wa mkoa wa DSM hapa mbezi Luis stend ya daladala stend za kupanda na kushuka. Haya ndiyo yatakayokutia doa

Ni maoni yangu kama mwananchi
 
Umesahau kueleza kuwa ni pahali ambapo watu wasio na makazi ndipo hulala hapo, sijui walio plan kujenga hicho kivuko ndivyo walivyokusudia ama lah, kwa kifupi panatisha kama ulivyo eleza.
 
Umeongea point sana, ila umeboronga hapo unaposema ulipishe watu kutumia ngazi Hiyo siyo solution,yani Sasa unataka watu wawe kama wakimbizi kwenye nchi Yao.

NB pale kwenye ngazi kinachosababisha folen ni wale wakina mama wanafanya biashara ndogondogo Huwa wanakaa katikati ya njia hivo unakuta mtu ananunua kitu anasimama njiana hivo kusababisha folen hasa mida ya jioni na alfajiri.

Solutions; uongozi husika wakae waongee nao wawatafutie eneo karbu na hapo coz wapo kwenye utafutaji
 
Umeongea point sana, ila umeboronga hapo unaposema ulipishe watu kutumia ngazi Hiyo siyo solution,yani Sasa unataka watu wawe kama wakimbizi kwenye nchi Yao...
Nia Yao wauze..paleoale
 
Back
Top Bottom