Tutofautishe bei ya mazao, wingi wa mavuno na kuuza mazao nje ya nchi

don-mike

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
435
843
Nnaona kuna upotoshwaji wa hali ya juu wa hali ya chakula nchini. Si kawaida yangu kuanzisha thread, ila hili imebidi nianzishie thread.

Kwanza kabisa ni declare interest, mimi ni mdau wa kilimo kwa miaka mingi, hivyo nnachoandika hapa ni kutokana na uzoefu wangu kwenye kilimo.

HOJA KUU
Watu wengi wanachanya bei za mazao kuwa juu na upatikanaji wa mazao nchini. Wengi wamejawa na hofu ya kutokea njaa, watu kukosa chakula hasa vijijini, etc....kubwa zaidi ni watu wa mjini kuogopa kununua chakula kwa bei ya juu.

Ikumbukwe mazao yanayolalamikiwa sana hapa ni mahindi na mpunga. Kwa kuwepo field, sioni kama kunaweza tokea njaa yoyote Tanzania, sababu watu walilima, na watu wanaendelea kuvuna.

Swala la kupanda bei lina pande mbili, kubwa ikiwa gharama kubwa za mbolea na mazao kiduchu yaliyotokana na wengu walioshindwa nunua mbolea.

Wengi mtawaza kwamba serikali izuie kuuza nje ili bei za vyakula zishuke, hiyo itakuwa kumuua mkulima at the expense ya walaji. Ikumbukwe mwaka jana mwishoni serikali ilinunua kwa wingi mahindi kwa wakulima na bado hawajaanza toa stock kwenye maghala yao. Hivyo mkulima aendelee uza kwa bei inayomlipa, popote kwenye soko, serikali ina stock ya kutosha kuuza ndani, muda ukifika itoe stock yake.
 
Thats true..Watu waseme ukweli tu kuwa bei zipo juu serikali ifanye mpango mazao yashuke but hiyo itamuumiza sana mkulima aliyenunua mbolea 120k afu aje kuuza mahindi 40k itakuwa si haki acha vita ya ukraine ituumize wote....Mfuteni mkulima machozi atoke kwenye kilio cha samaki basi daah
 
Alhamdulilah Ingawa mavuno yalikua hafifu mwaka huu lakini sikosi gunia 20 za mahindi msimu huu, ninayaweka store nasubiri angalau ifike 120000 kwa gunia, acheni tu mwaka huu tupige neema wakulima, tumeteseka sana
 
Kabisa aisee.....hawa watu wamezoea umiza wakulima....this time waziri Bashe is brave enough....kama walikuwa wanataka bei ndogo, wangeuza mbolea bei ndogo.....50kgs mbole ilifika hadi 150k Songea, hapo mtu anataka uziwa unga kilo sh 1,000/= wapi na wapi
 
Subiri kuanzia oktoba utakapo nunua unga kwa sh 3000 ndio uje na hii mada
Mafuta yamefika Sh 3,000/= na maisha yanaenda, huku vijijini tunanunua mafuta Tsh 4,000/= kwenye vidumu na maisha yanaenda, sasa nyinyi mnataka nunua unga bei che...."alikwambi nani" in Bwege voice.
 
Nnaona kuna upotoshwaji wa hali ya juu wa hali ya chakula nchini. Si kawaida yangu kuanzisha thread, ila hili imebidi nianzishie thread.

Kwanza kabisa ni declare interest, mimi ni mdau wa kilimo kwa miaka mingi, hivyo nnachoandika hapa ni kutokana na uzoefu wangu kwenye kilimo.

HOJA KUU
Watu wengi wanachanya bei za mazao kuwa juu na upatikanaji wa mazao nchini. Wengi wamejawa na hofu ya kutokea njaa, watu kukosa chakula hasa vijijini, etc....kubwa zaidi ni watu wa mjini kuogopa kununua chakula kwa bei ya juu.

Ikumbukwe mazao yanayolalamikiwa sana hapa ni mahindi na mpunga. Kwa kuwepo field, sioni kama kunaweza tokea njaa yoyote Tanzania, sababu watu walilima, na watu wanaendelea kuvuna.

Swala la kupanda bei lina pande mbili, kubwa ikiwa gharama kubwa za mbolea na mazao kiduchu yaliyotokana na wengu walioshindwa nunua mbolea.

Wengi mtawaza kwamba serikali izuie kuuza nje ili bei za vyakula zishuke, hiyo itakuwa kumuua mkulima at the expense ya walaji. Ikumbukwe mwaka jana mwishoni serikali ilinunua kwa wingi mahindi kwa wakulima na bado hawajaanza toa stock kwenye maghala yao. Hivyo mkulima aendelee uza kwa bei inayomlipa, popote kwenye soko, serikali ina stock ya kutosha kuuza ndani, muda ukifika itoe stock yake.
Kwanza mwaka huu mahindi yatapungua ukilinganisha na miaka mingine sababu za Ukame ila mpunga utaongezeka japo sio kwa kiwango kama cha mwaka Jana..

Hivyo kutokana na njaa kali kwenye Nchi za jirani inalazimu ku push Bei juu sababu exports imeruhisiwa..👇👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220719-153106.png
    Screenshot_20220719-153106.png
    90.8 KB · Views: 5
  • Screenshot_20220719-153949.png
    Screenshot_20220719-153949.png
    107.4 KB · Views: 7
  • Screenshot_20220719-153451.png
    Screenshot_20220719-153451.png
    93.7 KB · Views: 6
  • Screenshot_20220719-153552.png
    Screenshot_20220719-153552.png
    165.2 KB · Views: 6
Yani kwa mara ya kwanza kwa miaka mingi mkulima naye ananufaika. Tanzania yetu wakulima wengi huuzia mazao shambani, wafanyabiashara wananunua, wanasubilia bei ipande wauze kwa faida, mwaka huu bei wanauzaga wafanya biashara, ndio bei anayouzia mkulima shambani.
Kwanza mwaka huu mahindi yatapungua ukilinganisha na miaka mingine sababu za Ukame ila mpunga utaongezeka japo sio kwa kiwango kama cha mwaka Jana..

Hivyo kutokana na njaa kali kwenye Nchi za jirani inalazimu ku push Bei juu sababu exports imeruhisiwa..👇👇
 
Yani kwa mara ya kwanza kwa miaka mingi mkulima naye ananufaika. Tanzania yetu wakulima wengi huuzia mazao shambani, wafanyabiashara wananunua, wanasubilia bei ipande wauze kwa faida, mwaka huu bei wanauzaga wafanya biashara, ndio bei anayouzia mkulima shambani.
Bado kuna mafala wanaocheza BAO mjini wanataka eti mipaka ifungwe..
 
Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya watu mjini wanaishi kwa udalali, sasa hao ndio kila siku wana bundle za kutosha, wakiamka wanachochea mipaka ifungwe wao wapate unafuu wa maisha kwa kumgalagaza mkulima. Ukiangalia sana kwenye mzunguko wa maisha, budget ya chakula ni ndogo sana, acha chakula kipande mkulima naye anufaieka, watabana budget ya bundle maisha yaende.
 
Nnaona kuna upotoshwaji wa hali ya juu wa hali ya chakula nchini. Si kawaida yangu kuanzisha thread, ila hili imebidi nianzishie thread.

Kwanza kabisa ni declare interest, mimi ni mdau wa kilimo kwa miaka mingi, hivyo nnachoandika hapa ni kutokana na uzoefu wangu kwenye kilimo.

HOJA KUU
Watu wengi wanachanya bei za mazao kuwa juu na upatikanaji wa mazao nchini. Wengi wamejawa na hofu ya kutokea njaa, watu kukosa chakula hasa vijijini, etc....kubwa zaidi ni watu wa mjini kuogopa kununua chakula kwa bei ya juu.

Ikumbukwe mazao yanayolalamikiwa sana hapa ni mahindi na mpunga. Kwa kuwepo field, sioni kama kunaweza tokea njaa yoyote Tanzania, sababu watu walilima, na watu wanaendelea kuvuna.

Swala la kupanda bei lina pande mbili, kubwa ikiwa gharama kubwa za mbolea na mazao kiduchu yaliyotokana na wengu walioshindwa nunua mbolea.

Wengi mtawaza kwamba serikali izuie kuuza nje ili bei za vyakula zishuke, hiyo itakuwa kumuua mkulima at the expense ya walaji. Ikumbukwe mwaka jana mwishoni serikali ilinunua kwa wingi mahindi kwa wakulima na bado hawajaanza toa stock kwenye maghala yao. Hivyo mkulima aendelee uza kwa bei inayomlipa, popote kwenye soko, serikali ina stock ya kutosha kuuza ndani, muda ukifika itoe stock yake.
Kusema "watu walilima na wanaendelea kuvuna" una maana gani?

Ni mkoa gani huo mvua imenyesha vizuri wakalima na sasa wanavuna?

Ukame uliotamalaki nchini wewe hauuoni?
Si chakula tu, hata maji ni shida na kuna ukame wa kutisha!

Tafiti zako kuhusu mnyororo wa kilimo, stock za nafaka za serikali, hofu ya wakazi wa mjini kuhusu njaa ni dhaifu sana na hakuna uhalisia wowote.

Sasa hivi kutokana na ukame na njaa inayolikabili taifa, kuna mazao yanatolewa mjini na kwenda kuuzwa vijijini kwa bei ya faida.

Na serikali isipoliangalia jambo hili kwa jicho la3, basi kwa mara ya kwanza tangia uhuru, watu wanaweza kufa kwa njaa mwaka huu kutokana na hali halisi.

Kile chakula cha mgao wa kisanii wa kilo mbili hadi 10 kwa kaya zenye njaa hautakidhi chochote kutokana na ukubwa wa tatizo.
 
Kiufupi ni kwamba hii serikali inaendesha nchi kwa siasa hakuna kingine
 
Madaba Songea ntavuna mwezi wa nane week ya kwanza, bado mazao yanakaukia shambani.....usiongee nadharia.....tulio field tunaongea fact....huo ukame leo hii upo wilaya gani...? Mwaka gani mvua zimenyesha sawa nchi nzima? Always kuna sehemu chache kila mwaka wanalia shida....
 
Sibishi kama Madaba Songea mvua inanyesha na mnavuna.

Embu fanya utafiti basi kwa mikoa mingine nchini mwaka huu ina hali gani?

Karibia 80% ya mikoa yote nchini mwaka huu ni njaa kali kutokana na ukame uliosababishwa na mvua za masika kuto kunyesha sawa sawa.
 
Mavuno kitaifa ni machache, ndio maana bei ipo juu, na bei ipo juu shambani sio kwa madalali, sababu ya bei juu ya mbolea, madawa, mafuta, etc...... mazao yapo ya kutosha mashambani, kilimo cha mtanzania ni hiki hiki kila siku, mvua zinakuja kwa ratiba inazozijua zenyewe, ukibahatisha ukapanda na mtiririko wa mvua utavuna, la sivyo......mikoa yote hali ipo hivyo
 
Back
Top Bottom