Tutarajie Uchaguzi mdogo Jimbo la Buhigwe baada ya Dkt. Philip Mpango kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa JMT

Sasa Huyu Zito atamaliza MajimBo Ya Mkoa Wa Kigoma, Maana Kama akienda Huko Buhigwe Litakuwa Jimbo La Tatu.

Ni haki yake kikatiba mkuu ,hata wewe au mimi tunaweza kugombea maana katiba imeruhusu ili mradi udhaminiwe na chama na ujue kusoma na kuandika tu.
 
Haya sasa, Wezi wa kura pigeni jalamba - wazee wa kuteka wagombea, wazee wa kupiga mitama na kupokonya form za uteuzi, wazee wa kubambikizia wagombea kesi zisizo na dhamana, wazee wa kufunga ofisi za uteuzi mchana na kuzifungua usiku -- hayaaa sasa ubwabwa wa msibani huooo wajaa!!!
 
Nchi yetu ina viongozi Wakuu toka pande zote za Nchi

Rais anatokea Tanzania Visiwani

Makamu wake anatokea Magharibi

PM anatokea Kusini

Spika anatokea katikati mwa nchi

Naibu Spika anatokea Nyanda za juu kusini

Jaji Mkuu anatokea Kaskazin Magharibi

Mkuu wa Usalama wa Taifa anatokea Mashariki mwa nchi

CDF anatokea 'Ukanda wa Ghaza'

Najivunia kuwa Mtanzania Wallahi wabillah wataalah
 
Nchi yetu ina viongozi Wakuu toka pande zote za Nchi

Rais anatokea Tanzania Visiwani

Makamu wake anatokea Magharibi

PM anatokea Kusini

Spika anatokea katikati mwa nchi

Naibu Spika anatokea Nyanda za juu kusini

Jaji Mkuu anatokea Kaskazin Magharibi

Mkuu wa Usalama wa Taifa anatokea Mashariki mwa nchi

CDF anatokea 'Ukanda wa Ghaza'

Najivunia kuwa Mtanzania Wallahi wabillah wataalah
Ukanda wa Ghaza???
 
BAADA YA DK. PHILIP MPANGO KUWA MAKAMU WA RAIS JIMBO LA UCHAGUZI LA BUHINGWE MKOANI KIGOMA LIKO WAZI.

Mbunge akiteuliwa kuwa Makamu wa Rais anakoma kuwa mbunge.

Hivyobasi, Dk. Philip Isidori Mpango atakapo apishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakoma kuwa mbunge wa Jimbo la Uchaguzi la Buhingwe lililopo Mkoani Kigoma, haya ni matakwa ya masharti ya Ibara ya 47 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977.

Hivyobasi, Jimbo la Uchaguzi la Buhingwe lililopo Mkoani Kigoma liko wazi na Uchaguzi Mdogo utaitishwa na Tume ya Uchaguzi kujaza nafasi hiyo kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Uchaguzi.

By Matojo M. Cosatta
Upotevu wa pesa za Umma.Ndio maana ya Vyama vya Upinzani (Opposition Parties)kudai Katiba Mpya.Moja ya masuala ni hili la Mawaziri kutokuwa Wabunge.
 
Back
Top Bottom