Tutakumbushana tena 2025 Magufuli kama atakubali kuachia madaraka basi atalazimisha kutuachia Rais anayependa yeye

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Kuna Vitetesi fulan japo 2025 ni mbali ila kwa uoga wa Rais Magufuli, endapo akikubali kuachia madaraka basi atauingilia Uchaguzi kuanzia mchakato wa Mgombea ndani ya Chama hadi Uchaguzi Mkuu kwa ujumla kuhakikisha anayebaki ni yule atakayefanya yafuatayo

1. Hataruhusu kujadiliwa kwa aliyofanya rais mstaafu.

2. Hataibua hoja au hataruhusu hoja za kuhoji matumizi yasiyofuata taratibu za Manunuzi kama vile ununuzi wa Ndege, na ujenzi wa miradi mbali mbali Ambayo haikufuata utaratibu na hatuoni uwazi.

3. Hataruhusu kuhoji haki za watu zilizopotea na haki za watu waliouwawa au kufichwa kabisa.

4. Hataruhusu kuhojiwa Kwa wafanya biashara Walidhulumiwa na serikali na wengine kufungwa kwa kisingizio cha Uhujumu uchumi na utakatishaji pesa.

5. Hataruhusu kabisa uwazi wa namna yeyote.

KATIKA WATU ANAOWAONA WATAIWEZA KAZI HIYO

1. Bwana Hussein Mwinyi wa Zanzibar, huyu atakuwa ni yule wa Ndiyo mzee wangu mstaafu pumzika usiguswe

2. Paul Makonda, kwa Muda huu anatuzuga kamsahau lakin kwa Mabalaa na Maajabu ya Tanzania ukashangaa 2026 anapigiwa mizinga

3. Kassim Majaliwa, Huyu naye yuko Obedient Sana kwa Magufuli

4. Hamis kigwangalla,


Si lazima jina liwe kwenye hayo ila atapitishwa mwenye sifa za hao

Tukumbushane July 2025

Mungu atuweke na yeye amuweke pia maana ya Mungu Mengi hapa kati kati

Amen

Britannica
 
Sijui kama tutafika 2025 salama, maana kwa ninavyo uona mwelekeo kama dereva gari limesha mshinda na limeshaacha njia. Ameshaamua liwalo na liwe, kama kuchoma kibanda fresh tu.

Sio kwa hali hii ya sasa hivi mpaka kufikia hatua "TRA KUANZISHA KODI ZA VITANDA". Wenyewe kwa lugha ya malkia eti wanaita "BED LEVY".
 
Siwezi puuza huu uzi watu waoga huwa wanaweka kinga ili wasiumizwe ila kuna mawili
1.KUKOMAA MADARAKANI
2.AU KUKIMBIA NCHI/KUISHI UHAMISHONI ILI WATU WASILIPE KISASI
3.KUMCHAGUA SHOSTI MWENYE MAELEKEZO YA KUMLINDA kama mtoa mada asemavyo humu
 
Hii ni sawa na mwanaume ambaye hacheat katika ndoa lakini mwanamke anamshuku mumewe na kumkaripia kila anapochelewa kurudi nyumbani, mwisho wa siku Mwanaume anaamua ku cheat sasa, Ndivyo ilivyo na itakavyokuwa
 
Mbona katiba tayari inawalinda hata watangulizi wake, yeye akifanya hivyo hatakuwa wa kwanza. CCM ikiendelea kutawala huu uozo hautakwisha.
 
Bora Mugalifu wao hana hayo mambo.
Mugafilu anazingatia haki za binadamu
Anazingatia utawala bora
Anazingatia utawala wa sheria
Hana upendeleo
Anazingatia usawa kwa kila mwananchi
Anazingatia ulaji sawa wa keki ya taifa.
Anawapenda sana wapinzani wake ikiwemo Tundu Lissu na CHADEMA kwa ujumla.
Anapenda sana kukubali kukosolewa
Ni msikivu wa kiwango cha rami.
Anazingatia misingi ya ukuzaji uchumi
Anazitumia vizuri pesa mabeberu(wanaume wachapakazi wa Uraya)
Anahakikisha afya za wananchi zinastawi
Ana ruhusu upatikana wa habari hata zile zinazomkosoa.
Anazingatia uwepo wa usalama wa kila mwananchi hata uwe wa CHADEMA.
Amekuwa kiongozi wa mfano ulimwenguni hata serikali za peponi zinajitahidi kumuiga yeye.
Anazingatia kutokuwepo kwa wasaliti duniani kwa kuwapa ulinzi(Tundu Lissu amiminiwa marisasi huko Dodoma)
Mambo ni mengi muda mchache

Kidumu chama chetu chakavu cha mapinduzi kisichojali tena matatizo ya wananchi.

Kigumu chama kinacho impoverish watanzania kwa speed ya mwanga.
 
Siwezi puuza huu uzi watu waoga huwa wanaweka kinga ili wasiumizwe ila kuna mawili
1.KUKOMAA MADARAKANI
2.AU KUKIMBIA NCHI/KUISHI UHAMISHONI ILI WATU WASILIPE KISASI
3.KUMCHAGUA SHOSTI MWENYE MAELEKEZO YA KUMLINDA kama mtoa mada asemavyo humu
Hata akikimbia nchi
Sindano ya sumu ya Doto James inaweza kumfuata huko huko
 
Viongozi wa awamu hii wanaishi kwa woga sana, kama vile hajashinda uchaguzi. Jana Majaliwa alikua anapita, nusu saa kabla bara bara iliachwa wazi na traffic, magari yote yalipack pembeni. Majaliwa alipita kama mwewe.
Ukweli ni kwamba hii mijitu hatuipendi, period
 
Back
Top Bottom