Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,366
- 5,994
Takhriban miaka 14 iliyopita tulishikwa na butwaa tuliangalia jirani zetu wa Rwanda wakichinjana kwa mapanga.
Tuliangalia tukikosa la kufanya hadi idadi ya waliopoteza maisha yao ilipofika karibu milioni moja!
Kwa miaka zaidi ya mitano tumebaki tukiangalia yanayotokea Dhafur na kwenyewe bila kuwa na jambo la msingi la kufanya. Tunashindwa kuwasaidia ndugu zetu tukisimamia kwenye hiki tunachokiita sovereignty ya serikali ya Sudan. Watu zaidi ya milioni 5 wameuawa magharibi kwetu, kule kulikokuwa kukiitwa Zaire na kwenyewe hatuna la kufanya.
Tumeangalia waMatebele, wazungu na wengine wanaopinga utawala wa Robert Mugabe wakiuawa bila kuwa na la kufanya isipokuwa kusisitiza solidarity yetu na utawala huo. Leo hawa jirani zetu, ndugu zetu wanauana kwa mishale na mapanga na kwenyewe tumeshikwa na butwaa na tunaangalia pasipo na njia ya kufanya.
Itakuja lini siku ambapo viongozi wetu wataelezwa kuwa damu ya muafrika ina thamani kama ya mtu mwingine yeyote na hatutakubali kuwa mashahidi wa genocide nyingine?
Nadhani wakati umefika wa kuwaambia hao wanaojiita viongozi huko Kenya, enough is enough. Tutaingia kunusuru roho za ndugu zetu. Hawa ni wana jumuia wenzetu na machozi yao ni machozi yetu. Tusingojee mpaka hapo itakapobidi wazungu (kama walivyofanya waingereza Sierra Leone, wafaransa Ivory Coast) kuja kuokoa maisha ya ndugu zetu.
Gharama ya procrastination ni ya juu mno na vizazi vijavyo vitatushitaki.