Tutaangalia mpaka lini?

Fundi Mchundo

Platinum Member
Nov 9, 2007
8,909
6,821
Takhriban miaka 14 iliyopita tulishikwa na butwaa tuliangalia jirani zetu wa Rwanda wakichinjana kwa mapanga.

Tuliangalia tukikosa la kufanya hadi idadi ya waliopoteza maisha yao ilipofika karibu milioni moja!

Kwa miaka zaidi ya mitano tumebaki tukiangalia yanayotokea Dhafur na kwenyewe bila kuwa na jambo la msingi la kufanya. Tunashindwa kuwasaidia ndugu zetu tukisimamia kwenye hiki tunachokiita sovereignty ya serikali ya Sudan. Watu zaidi ya milioni 5 wameuawa magharibi kwetu, kule kulikokuwa kukiitwa Zaire na kwenyewe hatuna la kufanya.

Tumeangalia waMatebele, wazungu na wengine wanaopinga utawala wa Robert Mugabe wakiuawa bila kuwa na la kufanya isipokuwa kusisitiza solidarity yetu na utawala huo. Leo hawa jirani zetu, ndugu zetu wanauana kwa mishale na mapanga na kwenyewe tumeshikwa na butwaa na tunaangalia pasipo na njia ya kufanya.

Itakuja lini siku ambapo viongozi wetu wataelezwa kuwa damu ya muafrika ina thamani kama ya mtu mwingine yeyote na hatutakubali kuwa mashahidi wa genocide nyingine?

Nadhani wakati umefika wa kuwaambia hao wanaojiita viongozi huko Kenya, enough is enough. Tutaingia kunusuru roho za ndugu zetu. Hawa ni wana jumuia wenzetu na machozi yao ni machozi yetu. Tusingojee mpaka hapo itakapobidi wazungu (kama walivyofanya waingereza Sierra Leone, wafaransa Ivory Coast) kuja kuokoa maisha ya ndugu zetu.

Gharama ya procrastination ni ya juu mno na vizazi vijavyo vitatushitaki.
 
Yaani kwa kweli ndugu yangu Mchundo inasikitisha. The best UN na "International community" can do ni kugawa misaada kwa IDPs na wakimbizi!!! Hivi Africa tulilaaniwa? the problem is there for all wanafiki to see, why cant we in a united form tell Kibaki kwamba what he is doing is wrong for Kenyans and humanity? harafu kesho unasikia UN is appealing for humanitarians funds to help displaced Kenyans.......shame on us Africans!

tunahitaji kiasi gani cha watu wafe na kuteketea kusudi tuseme ukweli? Hivi hiyo AU ni club ya wazee kunywa ghahawa au wana mambo ya maana wanayojadili kwa niaba ya wananchi wao? na kama yapo, lipi la zaidi ya damu ya mwananchi wa Nakuru, Darfur na kwingineko linalopashwa kujadiliwa?..na baada ya hapo utasikia wanaunda tume kuchunguza the cause of these deaths in Kenya!!!

Mpaka lini vifo vya waafrika vitakuwa na maana zaidi ya kuwa good source of statistics for academicians and researchers in western countries? Kila nikiwaza sipati jawabu kabisa, how on earth, of all countries, KENYA is just destroying itself voluntarily!! Mchana kweupeeeee!!!!

Thats why I dont use or like the word International community..the word is vague and meaningless! It sounds so huge but in reality halina maana! who is the international community? can you identify him or her?

Who is next after Kenya??
 
Grace Kakai, a police commander in Naivasha, said a large crowd of Kikuyus chased a group of Luos through a slum, trapped them in a house, blocked the doors and set the house afire. Police found 19 bodies huddled in one room, and Ms. Kakai said some of the children’s bodies were so badly burned that they could not be identified.

“All I can say is that they were school age,” she said.

Wanaendelea kuchoma mpaka watoto? Walifanya wakalenjin kwa wakikuyu, leo wakikuyu wamelipiza kwa wajaluo! yataisha lini? Hawa malaika wamekosa nini?

Hao mashujaa wanauana kwa mapanga na mishale halafu hayo majeshi yetu ambayo kila kukicha yananunuliwa silaha za kisasa ati kulinda hadhi ya taifa wanashindwa kuwakabili? Sasa kwa nini wanaoangalia hili wasituhukumu WOTE kuwa ndiyo jadi yetu waafrika maana maisha ya binadamu kwetu hayana thamani yeyote!
 
Mobs set buses ablaze at the main downtown bus station, and one Kikuyu driver was burned alive in his minibus, according to witness Lillian Ocho.

Members of the Kenyan Red Cross went to the morgue in Naivasha to try to figure out how many people were killed in ethnic violence that has injured at least 179 people in the last few days, the agency reported.

The Red Cross is investigating reports that several people were burned alive in the town -- just the latest instance of killing along ethnic lines that has swept Kenya since a disputed presidential election in Kenya.

Wanaendelea kufa! Tik tok tik tok tik tok!
 
Waswahili tunamsemo usemao ukiona mwenzi ananyolewa upara basi na wewe anza kutia maji ,maana ukichelewa basi utanyolewa kavu kavu,hapo ndio mbinde.

Mimi nasikitika sana kuona ya warwanda, waburundi wazaire, wazimbabwe, wasudani,wasomali hata kule mbali kabisa Dafur..nasikitika sana na kuukumbuka ule msemo wa ndugu zetu wa damu waliopo kisiwa jirani cha Pemba ambao wanauliwa kila ukaribiapo Uchaguzi kwa makumi na kufanyiwa vitendo vya ukafiri na mafirauni wa kipolisi wa Tanzania chini ya Mkuu wa Ufisadi Tanzania Mh.Benjamin Nkapa...

Hivyo wandugu mnatia huruma kuona ya mbali wakati chini ya nyayo zenu unapita udikiteta wa kifirauni na hamtoi hata mlio au ndio ule msemo ujulikanao kuwa mpemba si ntu basi Lana wanayoilani wapemba kwa Tanganyika inaitambalia Tanzania na hii kafara lake ni lazima kama kufa Mkapa ashitakiwe kwa mauaji yale la si hivyo waswahili tuna msemo au wapemba wana msemo Ngedere wakimaliza miti huingia mashambani na mashamba ya mafirauni hawa wa polisi na wajeshi waliotua na zana nzito visiwani ni Tanganyika, kaeni mkao wa kuhama kwa miguu.

2010 hii ni 2008 imebaki kama mwaka na miezi kumi.
 
Tanzania inachotakiwa kufanya sasa sio kuingilia migogoro ya watu.

Migogoro mingi ya Afrika chanzo chake ni matatizo ya kiuchumi ambayo kwa miaka mingi viongozi wa nchi hizi wameshindwa kuyatafutia dawa.

Matatizo ya Kenya na nchi nyingine ni kuwa jamii zao zinategemea aliyekuwepo madarakani atawasaidia wao kwa gharama za jamii zingine. Na kwa mtaji Tanzania haiwezi kutoa suruhishi la kudumu.

Tunachoweza kufanya kwa amani tuliyopewa muda mrefu ni kujenga uchumi wetu ambao atakayekuwa madarakani hatakuwa na sababu ya kusaidia watu wa dini yake, watu wa kabila lake au watu wa jimbo lake.

Moja ya sababu kubwa ya Kikwete kuwa na baraza kubwa ni kupata watendaji kutoka kila kona ya Tanzania. Lakini kama tungekuwa ni nchi yenye uchumi wa kutosha tusingejali idadi wa waislamu, wakristo, wazigua, wasukuma, wapare katika baraza lake.
 
Yaani nimekufaamu kama unasema Ufisadi umehusisha makabila yote ya Tanzania ,ukilihumisha hilo baraza la Mawaziri hakuna mkoa unaweza kusema upande wetu ni safi.Bora aje mzungu au vipi ??
 
Naam, Mkuu! Lakini unaamini kweli huo uchumi wetu hautaathirika wakati hali iko hivyo kwa jirani yetu? Tukumbuke kuwa huyu ndiye mshiriki wetu mkuu wa kibiashara. Pamoja na hayo mimi kinachoniuma ni hii apathy yetu ndugu zetu wanapouawa. Unadhani machafuko kama haya yakitokea Mexico, Marekani ataangalia na kushika tama tu? Hatujifunzi na yale yaliyotokea nchi iliyokuwa Yugoslavia? Nchi za ulaya ziliivalia na zinaendelea kuvalia njuga. Mnadhani nani mwenye wajibu wa kuingilia suala la Kenya kama sio sisi jirani na ndugu zao? Tungoje mpaka wazungu watuonee huruma halafu waje TENA kuokoa maisha ya waafrika? Lini tutawajibika wenyewe?
 
A Kenyan opposition MP has been shot dead in Nairobi, police say, adding they could not rule out a connection to disputed presidential elections.
Mugabe Were, a member of the Orange Democratic Movement (ODM) of the defeated candidate, Raila Odinga, was attacked outside his home, police said.

He is the first leading politician to have died amid violence that has gripped Kenya since December's poll.

It comes as nearly 100 people died in fresh bloodshed in the Rift Valley.

Tik tok tik tok tik tok!
 
Mbaya zaidi zimbabwe will be holding an election just arounbd the corner and very likely same mess and shit will roll over! Na SADC, AU, watabaki wanaangalia tu wakisubiri westerners kulta suluhisho, shame on us Africans!!!!!!!!!!!!!!!!! and especially our leaders!
 
Tanzania ifanye nini? Ni swali ambalo naenda nalo kulala kwa sasa kwani nusura na mimi nianzishe mada, ndio uzuri wa kusoma walichoandika wenzako...
 
The trouble in Kisumu began at 8 a.m. on Monday, when young Luo men set fire to a bus believed to have Kikuyu owners. Witnesses said that the passengers escaped and that the attackers had been exacting revenge for what happened the day before, when a Kikuyu mob trapped 19 Luos inside a house in the town of Naivasha and burned them to death.

By 2 p.m., thousands of rioters were sweeping across Kisumu, lighting enormous bonfires and looting shops and even schools. Witnesses said a mob had cleaned out one primary school, taking desks, chairs, books, doors and even windows. Kenyan television stations showed dozens of terrified children running out of the school, some holding hands, as the mob closed in.

Something kuliko hii apathy! Tik tok tik tok tik tok! Tusije tukasema hatukujua ndiyo maana hatukufanya kitu. Tik tok tik tok tik tok.
 
TANZANIA HAIWEZI KUKAA PEMBENI, KUSUBIRI​

Tusipoangalia, yale yaliyotokea Rwanda miaka 14 iliyopita mwezi ule wa Aprili ya kukumbukwa, yako hatarini kutokea tena kwa majirani zetu wa Kenya.

Mauaji ya kiongozi wa upinzani Bw. Mugabe Were mapema asubuhi ya leo yawezekana kuwa ni yale mafuta yanayotumika kuchochea moto wa hasira na kisasi kama yale mauaji pacha ya marais wa Rwanda na Burundi.

Kufuatia uchaguzi mbovu wa Disemba 27 ambapo ulifuatiwa na vurugu na machafuko ya kisiasa, kuna hatari sasa kuwa nchi ya Kenya iko hatarini kuingia katika mauaji ya kimbari na pasipo shaka kuingia katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ambayo kama hayatazuiwa mapema, yataiingiza nchi hiyo kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Pale ambapo vyombo vya usalama vitakapoanza kuchagua upande hasa baada ya kuona watu wa makabila yao au jamaa zao wakikatwa vipande vipande na kuuawa kikatili, basi Kenya tuliyoifahamu kama nguvu ya uchumi katika eneo letu la Maziwa Makuu, itaporomoka na kuvunjika.

Maisha ya wa Kenya yako hatarini na viongozi wao wa kisiasa wameshindwa kabisa kuzuia uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu ambao unatishia siyo tu maisha ya wananchi wa kawaida bali pia unatishia hatima ya Jamhuri hiyo.

Hata hivyo, jambo linalotisha zaidi na bila kukusudiwa litachangia nchi hiyo kuingia katika vita vya wenyewe ni ukimya wa majirani zao na hasa uamuzi wa kuwa watazamaji wa mbali na wahusika wanaosubiri kukaribishwa.

Ukimya huu hasa kwa upande wa Tanzania ambayo ndiyo nchi itakayopoteza vingi na mengi endapo Kenya itakuwa vitani, unatukumbusha ukimya wetu katika siku zile mia moja za mwaka 1994 ambapo zaidi ya watu laki nane waliuawa kufuatia mauaji ya kujaribu kuangamiza jamii moja.

Matokeo ya ukimya ule siyo tu kusambaratika kwa Rwanda lakini pia matatizo ya baadaye ya Burundi na Congo na uhamisho wa wananchi wa nchi hizo kuja Tanzania. Matokeo yake ni Tanzania kupokea wakimbizi zaidi ya milioni moja toka nchi hizo.

Hatuwezi tena kuwa Taifa linalosubiri machafuko na kuanza kuomba misaada ya kuhudumia wakimbizi huku tukiweka mzigo mkubwa katika miundo mbinu yetu na uchumi wetu.

Siyo hayo tu bali pia kuibuka kwa vitendo vya ujambazi na mauaji mipakani mwetu ni matokeo ya vurugu hizo kwenye nchi jirani.

Wakati umefika kwa serikali ya Tanzania kuamua kushiriki moja kwa moja katika kutuliza vurugu za kisiasa nchini Kenya kwani Jeshi la nchi hiyo na vyombo vyao vya usalama vimeshindwa kufanya hivyo na vingi vimeshakosa imani ya wananchi hao.

Huko nyuma tulikuwa na kauli isemayo kuwa Tanzania haiko huru mpaka Afrika yote iwe huru. Leo hii tunaweza kusema kwa uhakika kabisa kuwa Tanzania haiwezi kuwa na amani kama majirani zake wanapigana. Amani ya Tanzania imefumwa na kuungana kwa namna isiyoweza kutenganishwa na amani ya majirani zake.

Ni kwa sababu hiyo basi natoa wito kwa serikali ya Tanzania kufanya mambo yafuatayo mara moja kabla mambo hayajaharibika kabisa.

- Kuandaa vikosi vyetu vya jeshi na Polisi ili kwenda kutuliza amani katika maeneo ya Kenya na hivyo kuviachilia vikosi vya Kenya ambavyo baadhi yao vinadaiwa kushiriki katika umwagikaji damu.

- Vikosi hivyo vyetu viwe tayari kwenda mara moja pindi serikali ya Kenya itakapokubali na baada ya kuleta "Hoja ya Haraka" kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa kutokana na vurugu zinazoendelea Kenya usalama na maslahi ya Tanzania yanatishiwa.

- Rais Jakaya Kikwete aunde timu ya Upatanishi itakayojumuisha viongozi wakongwe na wanaoheshimika wa eneo letu. Timu hiyo inaweza kuongozwa na wanasiasa mashuhuri na kuitisha mkutano wa viongozi wa Kenya mjini Arusha mapema iwezekanavyo.

- Bunge la Tanzania ambalo linakutana sasa hivi liidhinishe nyongeza ya bajeti kwa idara za Usalama ili kuweza kuhudumia vikosi na wapiganaji wetu ili kuweza kukaa nchini Kenya hadi hali itakapotulia na suluhisho la kisiasa kupatikana.

- Vikosi vyetu lazima viende kwa misingi ya kulinda amani na siyo kuchukua upande wowote kati ya pande mbili na kuhakikisha maisha ya Raia wa Kenya yanalindwa na kuleta utulivu. JWTZ inaweza kushikirikiana na Jeshi la Kenya kuhakikisha kuwa Polisi wa Kenya hawasimamii usalama tena hasa kwenye maeneo ya vurugu.

Haya ni baadhi ya mambo ambayo tunaweza kufanya sasa badala ya kusubiri baadaye na kuanza kujiuliza "tulikuwa wapi?" wakati dalili za vita zinaonekana.

Japo hili laweza kuonekana ni jambo kubwa hata hivyo gharama ya kutofanya lolote ni kubwa zaidi. Serikali ya Tanzania na wananchi wa Tanzania hawawezi kukaa kimya wakati ndugu na majirani zao wanachinjana.

Kama kuna somo tulijifunza kutoka Rwanda mwaka 1994 ni kuwa, kisasi huzaa kisasi, na mauaji ya kimbari hayaishi kwa kuzungumza bali kwa kuingilia kati na kulazimisha amani. Tanzania iongoze katika hilo kwani ukimya wetu na kushiriki kwetu kwa mbali kutatugharimu na kumeshagharimu maisha ya watu wengi sasa.
 
The Kenyan police said they had arrested three people in Were's killing. Still, Were's death and the prolonged tension spurred attacks that included the beheading of a doctor in the nearby Kibera slum, an Odinga stronghold, and several reports of forcible circumcision of Luos, who traditionally do not practice that rite. The violence has pitted members of Kibaki's Kikuyu tribe, long accused of being the object of favors from successive Kenyan governments, against Luos, Luhyas and Kalenjin, which had hoped an Odinga victory in the December 27 election would right decades of perceived injustices.

At least seven people were killed on Tuesday in the capital, Nairobi, after Mugabe Were, from Mr Odinga's ODM party, apparently died in the city in violence triggered by last month's disputed elections. There is only one Kenya - we all have multiple identities but I hope you see yourselves as Kenyans first

At least one person died in the Rift Valley town of Naivasha.

Army helicopters fired tear gas and what they said were rubber bullets at a mob of ethnic Kikuyus attacking Luo refugees trying to flee the town.

Inching towards 1000! Tik tok tik tok tik tok....
 
Yaani nimekufaamu kama unasema Ufisadi umehusisha makabila yote ya Tanzania ,ukilihumisha hilo baraza la Mawaziri hakuna mkoa unaweza kusema upande wetu ni safi.Bora aje mzungu au vipi ??

Hiyo ndio porojo yenyewe bongo. Kila mkoa, dini au kabila lina wawakilishi kwenye kuvuta.

Afu rais anachaguliwa kutoka kwenye kikabila kidogo kudumisha amani.
 
Naam, Mkuu! Lakini unaamini kweli huo uchumi wetu hautaathirika wakati hali iko hivyo kwa jirani yetu? Tukumbuke kuwa huyu ndiye mshiriki wetu mkuu wa kibiashara. Pamoja na hayo mimi kinachoniuma ni hii apathy yetu ndugu zetu wanapouawa. Unadhani machafuko kama haya yakitokea Mexico, Marekani ataangalia na kushika tama tu? Hatujifunzi na yale yaliyotokea nchi iliyokuwa Yugoslavia? Nchi za ulaya ziliivalia na zinaendelea kuvalia njuga. Mnadhani nani mwenye wajibu wa kuingilia suala la Kenya kama sio sisi jirani na ndugu zao? Tungoje mpaka wazungu watuonee huruma halafu waje TENA kuokoa maisha ya waafrika? Lini tutawajibika wenyewe?

Uchumi wa Tanzania hauwezi kuwaathirika kabisa na matatizo yanayotokea kule kwa sababu zifuatazo. Sekta kubwa ya uchumi ni misaada na Kenya sio nchi inayotusaidia. Sekta inayofuatia ni madini, migodi iko mbali na Kenya.

Ndio sisi ni ndugu zao. Lakini Tanzania ni ndugu na Zaire vilevile. Na vita vya Zaire vimepoteza watu wengi sana kwanini tusiende kule na twende Kenya?
 
TANZANIA HAIWEZI KUKAA PEMBENI, KUSUBIRI​

Tusipoangalia, yale yaliyotokea Rwanda miaka 14 iliyopita mwezi ule wa Aprili ya kukumbukwa, yako hatarini kutokea tena kwa majirani zetu wa Kenya.

Mauaji ya kiongozi wa upinzani Bw. Mugabe Were mapema asubuhi ya leo yawezekana kuwa ni yale mafuta yanayotumika kuchochea moto wa hasira na kisasi kama yale mauaji pacha ya marais wa Rwanda na Burundi.

Kufuatia uchaguzi mbovu wa Disemba 27 ambapo ulifuatiwa na vurugu na machafuko ya kisiasa, kuna hatari sasa kuwa nchi ya Kenya iko hatarini kuingia katika mauaji ya kimbari na pasipo shaka kuingia katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ambayo kama hayatazuiwa mapema, yataiingiza nchi hiyo kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Pale ambapo vyombo vya usalama vitakapoanza kuchagua upande hasa baada ya kuona watu wa makabila yao au jamaa zao wakikatwa vipande vipande na kuuawa kikatili, basi Kenya tuliyoifahamu kama nguvu ya uchumi katika eneo letu la Maziwa Makuu, itaporomoka na kuvunjika.

Maisha ya wa Kenya yako hatarini na viongozi wao wa kisiasa wameshindwa kabisa kuzuia uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu ambao unatishia siyo tu maisha ya wananchi wa kawaida bali pia unatishia hatima ya Jamhuri hiyo.

Hata hivyo, jambo linalotisha zaidi na bila kukusudiwa litachangia nchi hiyo kuingia katika vita vya wenyewe ni ukimya wa majirani zao na hasa uamuzi wa kuwa watazamaji wa mbali na wahusika wanaosubiri kukaribishwa.

Ukimya huu hasa kwa upande wa Tanzania ambayo ndiyo nchi itakayopoteza vingi na mengi endapo Kenya itakuwa vitani, unatukumbusha ukimya wetu katika siku zile mia moja za mwaka 1994 ambapo zaidi ya watu laki nane waliuawa kufuatia mauaji ya kujaribu kuangamiza jamii moja.

Matokeo ya ukimya ule siyo tu kusambaratika kwa Rwanda lakini pia matatizo ya baadaye ya Burundi na Congo na uhamisho wa wananchi wa nchi hizo kuja Tanzania. Matokeo yake ni Tanzania kupokea wakimbizi zaidi ya milioni moja toka nchi hizo.

Hatuwezi tena kuwa Taifa linalosubiri machafuko na kuanza kuomba misaada ya kuhudumia wakimbizi huku tukiweka mzigo mkubwa katika miundo mbinu yetu na uchumi wetu.

Siyo hayo tu bali pia kuibuka kwa vitendo vya ujambazi na mauaji mipakani mwetu ni matokeo ya vurugu hizo kwenye nchi jirani.

Wakati umefika kwa serikali ya Tanzania kuamua kushiriki moja kwa moja katika kutuliza vurugu za kisiasa nchini Kenya kwani Jeshi la nchi hiyo na vyombo vyao vya usalama vimeshindwa kufanya hivyo na vingi vimeshakosa imani ya wananchi hao.

Huko nyuma tulikuwa na kauli isemayo kuwa Tanzania haiko huru mpaka Afrika yote iwe huru. Leo hii tunaweza kusema kwa uhakika kabisa kuwa Tanzania haiwezi kuwa na amani kama majirani zake wanapigana. Amani ya Tanzania imefumwa na kuungana kwa namna isiyoweza kutenganishwa na amani ya majirani zake.

Ni kwa sababu hiyo basi natoa wito kwa serikali ya Tanzania kufanya mambo yafuatayo mara moja kabla mambo hayajaharibika kabisa.

- Kuandaa vikosi vyetu vya jeshi na Polisi ili kwenda kutuliza amani katika maeneo ya Kenya na hivyo kuviachilia vikosi vya Kenya ambavyo baadhi yao vinadaiwa kushiriki katika umwagikaji damu.

- Vikosi hivyo vyetu viwe tayari kwenda mara moja pindi serikali ya Kenya itakapokubali na baada ya kuleta "Hoja ya Haraka" kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa kutokana na vurugu zinazoendelea Kenya usalama na maslahi ya Tanzania yanatishiwa.

- Rais Jakaya Kikwete aunde timu ya Upatanishi itakayojumuisha viongozi wakongwe na wanaoheshimika wa eneo letu. Timu hiyo inaweza kuongozwa na wanasiasa mashuhuri na kuitisha mkutano wa viongozi wa Kenya mjini Arusha mapema iwezekanavyo.

- Bunge la Tanzania ambalo linakutana sasa hivi liidhinishe nyongeza ya bajeti kwa idara za Usalama ili kuweza kuhudumia vikosi na wapiganaji wetu ili kuweza kukaa nchini Kenya hadi hali itakapotulia na suluhisho la kisiasa kupatikana.

- Vikosi vyetu lazima viende kwa misingi ya kulinda amani na siyo kuchukua upande wowote kati ya pande mbili na kuhakikisha maisha ya Raia wa Kenya yanalindwa na kuleta utulivu. JWTZ inaweza kushikirikiana na Jeshi la Kenya kuhakikisha kuwa Polisi wa Kenya hawasimamii usalama tena hasa kwenye maeneo ya vurugu.

Haya ni baadhi ya mambo ambayo tunaweza kufanya sasa badala ya kusubiri baadaye na kuanza kujiuliza "tulikuwa wapi?" wakati dalili za vita zinaonekana.

Japo hili laweza kuonekana ni jambo kubwa hata hivyo gharama ya kutofanya lolote ni kubwa zaidi. Serikali ya Tanzania na wananchi wa Tanzania hawawezi kukaa kimya wakati ndugu na majirani zao wanachinjana.

Kama kuna somo tulijifunza kutoka Rwanda mwaka 1994 ni kuwa, kisasi huzaa kisasi, na mauaji ya kimbari hayaishi kwa kuzungumza bali kwa kuingilia kati na kulazimisha amani. Tanzania iongoze katika hilo kwani ukimya wetu na kushiriki kwetu kwa mbali kutatugharimu na kumeshagharimu maisha ya watu wengi sasa.

Let's be real. Eneo la Afrika mashariki na kati ni vurugu tupu. Tanzania leo ikingia Kenya, na kesho ikaingia Uganda, na keshokutwa ikaingia zaire, hiyo pesa ya kuwalisha watanzania itapatikana wapi waakati 40% inatoka kwenye misaada?

Acheni mambo ya umasikini jeuri.
 
Uchumi wa Tanzania hauwezi kuwaathirika kabisa na matatizo yanayotokea kule kwa sababu zifuatazo. Sekta kubwa ya uchumi ni misaada na Kenya sio nchi inayotusaidia. Sekta inayofuatia ni madini, migodi iko mbali na Kenya.

Ndio sisi ni ndugu zao. Lakini Tanzania ni ndugu na Zaire vilevile. Na vita vya Zaire vimepoteza watu wengi sana kwanini tusiende kule na twende Kenya?

Mmarekani mtarajiwa! Mwekezaji mkubwa katika haka ka uchumi ketu ni Kenya. Sasa hatutaathirika vipi? Misaada si sehemu ya uchumi wetu.Sehemu kubwa ya bajeti yetu ya serikali ndiyo inayobebwa na misaada wala sio uchumi. Mchangiaji mkubwa katika uchumi wetu ni sekta ya utalii, kuna misaada gani huko? Unadhani hao wanaowekeza kwenye madini na huo utalii wataendelea wakati hali ikiharibika huko Kenya?

Hauwezi kulinganisha DRC na Kenya. DRC, ndiyo tuliwalelea rais wao lakini toka enzi za ukoloni uchumi wetu na utawala ulishirikishwa sana na Kenya. Hii iliendelea hata baada ya uhuru wetu ambapo tulikuwa na East African Community iliyomiliki East African Airways, East African Railways, East African Harbours(?) mpaka customs. Mwalimu Nyerere ameshanukuliwa akisema alishapropose kuvuta subira na uhuru wa Tanganyika ili tupate pamoja na Kenya katika jitihada zake za kutuunganisha. Hawa walionekana ni natural partners kuliko hata Zanzibar ambayo wakati ule ilijulikana kuwa hatimaye itatawaliwa na Sultan mwenye asili ya Oman. Hawa ni ndugu zetu na ni aibu tunavyojikunyata tukikodolea macho. Wewe unadhani vurugu itokee Canada, nchi yako itaangalia tu?

DRC imefika hapo ilipo kwa sababu wakati matatizo yanaanza tuliwaangalia tu, tukitumai watayatatua wenyewe. sasa wamefika mahali ambako hata Umoja wa Mataifa wanashindwa kujamudu. Tusiachie tufike hapo huko Kenya.
 
NAIROBI, Kenya (CNN) -- Opposing sides in a bitter dispute plan to meet Thursday amid an unprecedented wave of violence that has claimed the life of a second opposition member of parliament.

Violence has killed at least 863 people and forced 261,000 others from their homes since a disputed presidential election stirred ethnic tensions around Kenya, a country long known as peaceful and relatively prosperous.

On Thursday, an opposition member of parliament, David Too, was shot dead in the city of Eldoret, Kenyan sources told CNN.

It's unclear whether his death is connected to post-election violence, but his death is the second this week of a legislator from the opposition Orange Democratic Movement. Another member of parliament, Mugabe Were, was shot dead Tuesday.

Mwingine huyo. Tik tok tik tok tik tok! Pretty sooon we will be over the abyss.
Wakubwa wetu wako Addis wakitosa na mheshimiwa Kibaki! Rais gani anaweza kuondoka katika nchi yenye hali kama hii?
 
Mmarekani mtarajiwa! Mwekezaji mkubwa katika haka ka uchumi ketu ni Kenya. Sasa hatutaathirika vipi? Misaada si sehemu ya uchumi wetu.Sehemu kubwa ya bajeti yetu ya serikali ndiyo inayobebwa na misaada wala sio uchumi. Mchangiaji mkubwa katika uchumi wetu ni sekta ya utalii, kuna misaada gani huko? Unadhani hao wanaowekeza kwenye madini na huo utalii wataendelea wakati hali ikiharibika huko Kenya?

Hauwezi kulinganisha DRC na Kenya. DRC, ndiyo tuliwalelea rais wao lakini toka enzi za ukoloni uchumi wetu na utawala ulishirikishwa sana na Kenya. Hii iliendelea hata baada ya uhuru wetu ambapo tulikuwa na East African Community iliyomiliki East African Airways, East African Railways, East African Harbours(?) mpaka customs. Mwalimu Nyerere ameshanukuliwa akisema alishapropose kuvuta subira na uhuru wa Tanganyika ili tupate pamoja na Kenya katika jitihada zake za kutuunganisha. Hawa walionekana ni natural partners kuliko hata Zanzibar ambayo wakati ule ilijulikana kuwa hatimaye itatawaliwa na Sultan mwenye asili ya Oman. Hawa ni ndugu zetu na ni aibu tunavyojikunyata tukikodolea macho. Wewe unadhani vurugu itokee Canada, nchi yako itaangalia tu?

DRC imefika hapo ilipo kwa sababu wakati matatizo yanaanza tuliwaangalia tu, tukitumai watayatatua wenyewe. sasa wamefika mahali ambako hata Umoja wa Mataifa wanashindwa kujamudu. Tusiachie tufike hapo huko Kenya.

Mbona watanzania mnataka kuwa waafrika sana kuliko wengine wakati resource za kutatua matatizo yetu wenyewe hazitoshi?

Kenya ni nchi yenye taasisi za kiserikali na zingine zimeendelea kuliko za Tanzania. Katika kipindi cha sasa, taasisi zao zinatakiwa zionyeshe kuwa ziko tayari kulinda maslahi ya Kenya na sio sisi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom