Je, mfungo wa Ramadhani au Kwaresma unaelewa kiundani maana yake au unafuata kama desturi tu?

greater than

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
813
1,263
Mwaka huu umekuwa na baraka ya kipekee, Vipindi vikuu vya kusafisha na kutakasa nafsi na roho zetu ,vimeangukia katika mwezi.
Lakini ndugu waumini wa hizi dini kubwa mbili (Ukristo na Uislam),kuna mambo kadha naomba kila mmoja wetu ajiulize na kutafakari.

1.Je, unaelewa kiundani maana ya mfungo,au unafuata kama desturi ?

2.Je,ushakaa na kutafakari juu ya yale maouvu uliyotenda.

3.Je,una timiza sala/swala zote muhimu katika mfungo,bila kutega ama chelewa?

4.Je,umesamehe ndugu,Jirani au rafiki aliyekutendea uovu kwa kukuibia, kukuzushia uongo,kukudhuru, kukusaliti kwenye ndoa,au Mungu akusamehe wewe tu.?

5.Je,umeshiriki kufanya tendo lolote la Huruma ?
-Hata kumpelekea yako chakula

6.Je,kwenye mda wa kula, unajifungia ndani , ?

7. Je,umekaa na kutafakari ni mambo mangapi Mungu alikubariki na alifanya ufanikiwe ?
 
Hizo ni funga za kibinadamu tu. Hamna sehemu yoyote Mungu anasema watu wafunge.
Mungu ni asili, habadiliki badiliki. Ndio maana mwanadamu akizaliwa anapata njaa, ananyonya, anaenda haja. Huo ni mpango wa Mungu.

Mungu haandiki wala hasomi. Hamna kitabu cha Mungu chini ya jua, ni maandishi tu ya wanadamu na hekima zao
 
Nunda
 
Naheshimu imani yako na msimamo wako ...
 
Jomba

Hizo ni Tamaduni za Warumi wa kale na Wakuresh wa kitambo. Fuateni tu mkumbo
 
Back
Top Bottom