Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,708
- 5,711
Ibara ya 3(1) ya katiba ya JMT inasema wazi kabisa kuwa Tanzania ni nchi isiyo na Dini,bali ni Nchi ya kidemokrasia ambayo inafuata misingi ya vyama vingi.
Tarehe 28 mwezi jana Watanzania walipiga kura,na walifanya maamuzi ya nani awe Mbunge, Diwani au Rais. Na matokeo yametoka na CCM imeibuka kidedea.
Vyama vya upinzani vimeanguka na ni anguko ambalo kila mtu alilitarajia tokea JPM alipoingia madarakani. Hii ni kwa sababu walichokuwa wanakihubiri wapinzani kwa miaka ishirini (ufisadi), kilipatiwa ufumbuzi. Na ufumbuzi wenyewe ni kudhibiti rushwa,ubadhirifu na kuleta uadilifu kwa watumishi wa Umma.
Kwa hiyo wananchi kuchagua wabunge wengi wa CCM na Wapinzani kuambulia wabunge nane sio hoja kuwa sasa tumerudi kwenye mfumo wa chama kimoja. Maana sio lazima tuwachague kama tunaona hamtufai. Mch Mtikila (RIP) hakuwahi kuwa mbunge lakini alikuwa mwanasiasa makini na mwenye hoja zenye mashiko. Hivyo kuingia bungeni sio sifa ya kuwa mpinzani makini.
Namalizia kusema watanzania wamechagua CCM sababu ya mambo makubwa iliyofanya miaka yote iliyopita na pia kwa kusikiliza kwa umakini ahadi zilizopo kwenye ilani ya CCM ya 2020-2025 ambayo wao wanauhakika kuwa itatekelezwa sababu ufisadi umebinywa na fedha za kutekeleza miradi zipo na kiongozi mkuu wa sasa ni msimamizi na mtekelezaji mahiri. Tumuombee kwa Mungu tarehe tano aapishwe ili kazi ziendelee kusonga mbele.