Tusipotoshe umma, Tanzania ni Nchi inayofuata mfumo wa vyama vingi, sio lazima Wapinzani kuchaguliwa kuwa Wabunge

Mzee wacha kupotosha tume na TISS pamoja na polisi ndio walioamuwa nani awe mshindi na sio wananchi.
 
CCM ni wezi wa kura period!

Zamani walikuwa wanaiba kiasi kiasi siku hizi wanavomola wanakomba kabisa. Mbunge amejipigia kura na kaenda na familia yake anakuta kapata zero.
 
Wanaoshangaa ya tanzania khs uchaguzi waangalie kinachoendelea USA na uchaguzi wao
 
Kama mmeshinda kwa kishindo why mnalazimisha bado ushindi uonekane au baada ya kuona hauna mvuto?

Pili kusema watanzania wamechagua ccm kutokana na kufanya makubwa je ni chaguzi gani ccm wamekuja na jipya ndani ya miongo yao 4 wasitaje maji na barabara je kuna jipya gani la maana?

CCM mnasemaje mmeshinda kwa kishindo ilhali sijaona mmetatua matatizo yaliyopo zama hizi kama shida kwenye marejesho ya HESLB, malipo ya wastaafu na bima ya NHIF sasa sijajua matatizo hayo makubwa yaliyoletwa na CCM ndio watu waliyachagua tena kwa miaka 5!
 
Upinzani wanataka uchaguzi urudiwe kwa sababu mawakala wa upinzani hawakuruhusiwa kuingia ndani kwenye baadhi ya vituo.

Mawakala wa upinzani walitolewa nje wakati wa kuhesabu kura kwenye baadhi ya vituo, waliwekwa ndani kuamkia siku ya uchaguzi kwenye majimbo kadhaa.

Maafisa usalama pamoja na jeshi walitumika kusimamia uchaguzi kinyume na sheria. Zimekamatwa sandarusi pamoja na viroba vya kura fake mchana kweupe karibia kila mahali kwenye nchi hii.

Baadhi ya vituo kura za Rais zilikuwa nyingi kuliko waliojiandikisha kupiga kura,kuna vituo mfano kwenye jimbo la Temeke kwenye vituo ambavyo wabunge wa upinzani walienda kupiga kura pamoja na familia zao wamepata kura sifuri,etc. Hizi ndizo sababu zinazosababisha upinzani kukataa matokeo ya uchaguzi huu na kutaka uchaguzi urudiwe
Mkuu utamaliza nguvu zako bure
 
Ibara ya 3(1) ya katiba ya JMT inasema wazi kabisa kuwa Tanzania ni nchi isiyo na Dini,bali ni Nchi ya kidemokrasia ambayo inafuata misingi ya vyama vingi.

Tarehe 28 mwezi jana Watanzania walipiga kura,na walifanya maamuzi ya nani awe Mbunge, Diwani au Rais. Na matokeo yametoka na CCM imeibuka kidedea.

Vyama vya upinzani vimeanguka na ni anguko ambalo kila mtu alilitarajia tokea JPM alipoingia madarakani. Hii ni kwa sababu walichokuwa wanakihubiri wapinzani kwa miaka ishirini (ufisadi), kilipatiwa ufumbuzi. Na ufumbuzi wenyewe ni kudhibiti rushwa,ubadhirifu na kuleta uadilifu kwa watumishi wa Umma.

Kwa hiyo wananchi kuchagua wabunge wengi wa CCM na Wapinzani kuambulia wabunge nane sio hoja kuwa sasa tumerudi kwenye mfumo wa chama kimoja. Maana sio lazima tuwachague kama tunaona hamtufai. Mch Mtikila (RIP) hakuwahi kuwa mbunge lakini alikuwa mwanasiasa makini na mwenye hoja zenye mashiko. Hivyo kuingia bungeni sio sifa ya kuwa mpinzani makini.

Namalizia kusema watanzania wamechagua CCM sababu ya mambo makubwa iliyofanya miaka yote iliyopita na pia kwa kusikiliza kwa umakini ahadi zilizopo kwenye ilani ya CCM ya 2020-2025 ambayo wao wanauhakika kuwa itatekelezwa sababu ufisadi umebinywa na fedha za kutekeleza miradi zipo na kiongozi mkuu wa sasa ni msimamizi na mtekelezaji mahiri. Tumuombee kwa Mungu tarehe tano aapishwe ili kazi ziendelee kusonga mbele.
CCM haina jipya zaidi ya miaka 50 ipo madarakani lakini mahitaji ya msingi kama maji bado yapo nchi nzima
 
Kura muibe halafu unasema tulipiga kura,acha ujuha matokeo mlishapanga muda na kura mlikuja nazo kwenye mabegi,mifuko,vikapu...ccm mmejaa wajinga,mafisadi na wachumia tumbo
Hizo ni hisia zenu na visingizio baada ya kichapo cha mbwa mwizi.
 
Back
Top Bottom