Tusipotoshe umma, Tanzania ni Nchi inayofuata mfumo wa vyama vingi, sio lazima Wapinzani kuchaguliwa kuwa Wabunge

Kama ni hivyo tusingepiga kura tar 28 oktoba 2020.
Hata DRC enzi za Mobutu walikuwa wakipiga kura hata Iraq enzi za Sadam walikuwa wakipiga kura. Kupiga kura siyo kigezo za Demokrasia bali je maamuzi ya hizo kura yanaheshimiwa? Hilo ndilo la msingi.
 
Hivi Johnthebaptist yuko wapi aanzishe angalau thread zenye maana kuhusu CCM? Wengine mko kama pilipili hoho tu hamna uchungu wala uchachu.
 
Hata DRC enzi za Mobutu walikuwa wakipiga kura hata Iraq enzi za Sadam walikuwa wakipiga kura. Kupiga kura siyo kigezo za Demokrasia bali je maamuzi ya hizo kura yanaheshimiwa? Hilo ndilo la msingi.
Usilinganishe Tanzania na hizo nchi, toa mifano inayolandana. Kama maamuzi ya kura hayaheshimiwi au kukubalika na wanachi ungeona wanaandamana.
 
"Mkichagua upinzani sitawaletea maendeleo"!

"Nikulipe mshahara halafu utangaze mpinzani kashinda"!

Kauli hizo hazijawahi kutolewa na kiongozi yeyote anayeheshimu misingi ya kidemokrasia!

Wananchi wanapaswa kuwa huru kuchagua! Na sio kutishwa kama ilivyotokea!

Mfumo wa Tanzania bado hautoi fursa kwa demokrasia kuchukua mkondo wake!

Sasa angalia ni kamata kamata ya wapinzani ndiko kunakoendelea!
Kweni huyo anayelipwa mshahara si lazima anatekeleza ilani ya chama kinacho mlipa,sasa kwa nini asiwaeleze wananchi kua hiyo ni ilani ya chama kinacho wafanyia kazi,msiwe mnaropoka tu bila kufikiri

Chama chochote kikiwa madarakani mamlaka husika ina uwezo wa kuwaeleza wananchi ni nani anaye tekeleza wanacho kiona,na hiyo siyo kuvunja demokrasia,isitoshe neno demokrasia ni desturi na mila za watu wengine kabisa zilizo lazimishwa kuenziwa na mataifa yasiyo husika na mila hiyo, neno hili demokrasia limesababisha Libya kua watu wanao zama kwenye bahari kila kukicha wakikimbia nchi yao iliyo kua njema sana.

Kama mnataka kuiga kila cha mtu mweupe basi ni afadhari muige kwa wachina,kazi kwanza kwa wote na siasa baadae

Nyie mmekalia demokrasia bila kuitafakafi ina lengo gani huku Afrika wajinga nyie
 
Kwani upinzani mlifungwa midomo kutoa ahadi zenu.. si nanyi mngesema hayo hayo kama wao.. simnajijua mulivyo geza geza..

Mgombea wenu kapata aliyopata.. musherekee.. wabunge waliotanguliza pinga pinga.. tumewapumzisha.. bora wa CCM.. tunajua watasimamiwa vyema..

Miaka nenda rudi.. wengine tumeona upinzani wa TZ.. hauvutii kabisaaaa..

Pongezi kwa
Wapinzani walikuwa wanapenda sana kutoka nje ya Bunge, sasa Watanzania tumeamua tuwatoe nje mazima ili wakavunje miguu vizuri kwa kunywa konyagi.
 
Mkuu uko sawa upstair (hili si tusi), usijitoe ufahamu kwa kiwango kikubwa hivyo. Ingawa tunatumia ID bandia lakini unjidhalilisha sana.
Huna haja ya kuzunguka kama mtoto,jibu swali langu,weka ushahidi wa kura zilizopigwa awali na maeneo gani zilipigwa.
 
Kwa nini Chadema kukosa wabunge mnaona kama kuna kasoro kwenye uchaguzi? Ila mkipata wabunge mnaona hakuna kasoro?
Mkuu hauko sawa mahali fulani, wanacholalamikia si idadi ya wabunge bali mchakato mzima wa uchaguzi. Mbona unakuwa kama roboti yaani kama wamekuprogramu, unasikitisha sana, hata mimi ni CCM lakini siwezi shabikia ushenzi na uzandiki uliofanyika.
 
Mkuu haulo sawa mhala fulani, wanacholalamikia si idadi ya wabunge bali mchakato mzima wa uchaguzi. Mbona unakuwa kama roboti yaani kama wamekuprogramu, unasikitisha sana, hata mimi ni CCM lakini siwezi shabikia ushenzi na uzandiki uliofanyika.
Uzandiki gani? Kila chaguzi malalamiko ya uongo ni haya haya ambayo hayana ushahidi concrete.
 
Mnatumia nguvu sana kujisafisha, ili mjua watanzania wa sasa sio wa enzi hizo wanaelewa kila kitu.
 
Back
Top Bottom