Salam wanaJF,
Katika nagzi za uatwala bora na uwajibikaji ni pamoja na ushirikishwaji, uwazi na kujali haki kwa wote. Sie wafuasi sugu wa CDM tunaomba tupewe ukweli kwa yanayojiri kwenye vyombo vya habari na pia uchaguzi ujao. Tunahitaji kujua haya:
1. Mipango ya chama kuwa na ofisi yake bila kukodisha kwani kinapokea ruzuku toka serikalini na hakuna sababu ya kukodisha majengo kwani uwezo wa kuwa na ofisi mikoani upo
2. Ukomo wa uongozi kwa mujibu wa katiba ya chama
3.Mapato na matumizi ya chama
4.Mafanikio ya wabunge wa cham kwa umma japo tunafahamu fika kuwa CCM ndio inayotekeleza sera zake kwani ndyo chama kinachounda serikali.
5. Je kwa nini Zitto Zuberi Kabwe hapewi nafasi kama Naibu Katibu Mkuu wa Chama.
Nawasilisha.
Habari ndugu,
upmejitambulisha kama 'wanachama sugu' na mimi nakujibu baadhi kama mmoja kati ya wanachama
Naamini ukiwa mmoja kati ya 'wanachama sugu' utakuwa unafahamu mengi zaidi kama ulijishughulisha kutaka kuyajua,
Umesema Chadema vyema juu ya chama kuwa na ofisi yake hasa ya makao makuu na kuwa na majengo ya ofisi mikoani, sababu chadema inapokea ruzuku kubwa!
Chadema ni chama cha wanachama, ambacho hata bila ya ruzuku kitawategemea wanachama wake, na nyinyi wanachama sugu ndio tunawategemea kwenye kuhamasisha ili tuweze kupata maeneo ya kujengea ofisi
ilipozinduliwa M4C, na nyiny 'wanachama sugu' kupitia matawi yenu mlipaswa kuwaendea wananchi kwenye maeneo yenu na kufanya harambee kwa ajili ya kukusanya pesa kwa ajili ya kununua eneo, matofali nk kwa ajili ya ujenzi wa ofisi
Nakupa mfano:- nenda kimara rombo, ulizia msingi wa Chadema wa Tarime, utaelezwa juhudi zao mpaka kujenga ofisi ya msingi sio Tawi (msingi)
Huu ni mfano wa uwajibikaji wa wanachama kwa chama chao
Kuhusu ukomo wa uongozi, kwa kuwa wewe na wenzako ni wanachama sugu, ina maana mmesoma katiba, kama mmesoma imejieleza vyema, ila jisikie huru kwenda ofisi ya katibu mkuu atakupa maelezo
Na kuhusu mapato na matumizi, kwa mujibu wa sheria ni msajili ndiye mwenye kutangaza kwenye gazeti la serikali, mapato na matumizi ya kila chama, ila hajawahi kutangaza ya chama chochote, sasa hata kama mnataka kuhama chadema, hameni ila nendeni UMD, SAU nk vyama ambavyo havijawahi kupata ruzuku, hivyo labda ni visafi, au undeni chama chenu, ni jambo la ki katiba mnaruhusiwa,.
Jambo jingine, umezungumzia juu ya mafanikio ya wabunge wa chama, nadhani labda wewe sio mfuatiliaji wa Bunge, wabunge wa chama kwa habari ya uwakilishi wao bungeni unaonekana wazi, labda huko majimboni ambapo napo hakuna malalamiko kutoka kwa wananchi wao, wengi wao wanafikia malengo
Na lingine juu ya Zitto, Zitto nafasi yake ya unaibu ni nafasi inayojitegemea na yenye majukumu yake kipekee, Zitto sio katibu mhutasi wa Slaa yeye ni sawa na kusema Katibu wa Chadema Tanganyika, ama Tanzania Bara na Slaa ni Katibu wa Chadema Tanzania, Zitto na Slaa kila mmoja ana majukumu yake sawa sawa na katiba inavyosema, na ofisi zao hazina migongano.
Usiku Mwema
M/Chama ChademaTz
Joash Mussa