Ndugu "ukikuta nzi au mende kafia kwenye maziwa usidhani alienda pale ili afe bali anaenda ili ale matokeo yake anafia hapo kabla ya kula" Binafsi sioni sababu ya CDM kujenga ofisi wakati huu,CDM haikurupuki inaenda kwa vipaumbele
Naomba ukiweza jiulize ni chama gani nje ya ccm chenye gazeti la chama,jengo la chama n.k? Nikuulize tena ni gazeti gani la ccm lililoanzishwa baada ya mfumo wa vyama vingi? ikiwa ni pamoja na ujenzi wa majengo au viwanja vya chama ukiacha vile vya serikali ya chama kimoja vilivyobinafsishwa kwa ccm bila idhini ya watanzania tunaolipa kodi.
Wakati huu ni wa kuimarisha chama sio wa kujenga majengo wala kuanzisha magazeti.Kuna faida gani kuanzisha gazeti kwa garama na kesho likafungiwa kwa idhini ya waziri wa serikali ya chama tawala ambao CDM ni wapinzani wao,kama unapitia sheria ya magazeti.
Ni nani anatumia mtaji kujenga duka kisha akakosa fedha ya kununulia bidhaa za kuuza ili apate faida.
Si wote wanaopanga maduka K'koo na kwingineko ni maskini bali wanaangalia vipaumbele.
CDM ikitumia fedha za ruzuku kujenga maofisi na kuanzisha magazeti haitakuwa na faida kwa watanzania hasa wa vijijini.
Pia CDM haitaendelea kwa kutumia movement moja tu yaani M4C,movement ni nyingi hapa unaweza kuuliza,lipi litaendelea baada ya M4C?