Ahmad Abdurahman
JF-Expert Member
- Mar 5, 2016
- 3,270
- 6,339
Mimi si kwamba namfahamu wala nini.
Ila huwa napenda kujadili hoja kwa kuangalia kina na kiini cha jambo. Sasa ukifanya mjadala kifalsafa hivyo, hawa wazushi wazushi wanaokuja na siasa za majitaka wote lazima washindwe mjadala.
Kwa sababu wataleta habari za double standard ambazo zinaweza kuleta ushawishi kwa watu ambao hawajajikita kujadili hoja kwa kina.
Lakini zikifika kwa watu wanaojadili hoja kwa kina, zinakwama.
Kwa sababu siasa za majitaka hizi hazina misingi mirefu kwenye ukweli, ni sarakasi za kuchafuana tu.
Ndiyo maana namuuliza mtu, habari zako za kwamba mtu asiwekwe juu kama "Mungu" unaziamini kiundani kabisa na hata kwa Magufuli unazikubali?
Aau unazileta kimazingaombwe tu kwa CAG, lakini kwa Magufuli huzikubali?
Aanajiumauma kujibu kitu kinachoeleweka.
Maswali yako hapo ndo yanamtafakarisha mtu na kumfanya akose majibu. Hawezi kutoa majibu ya kueleweka. Atasema A sio sawa na 1 ila atashindwa kusema kama B ni sawa 1.
Tumewaona ndugu zetu wakiwa wanafiki na wa kujipendekeza sana bila hofu na kuiita rangi nyeusi kua ni nyeupe na kutaka watu wote waamini ivo mradi tu kulinda maslahi yake.
Tuna safari ndefu sana, na mtu mnafiki anaujua ukweli lkn ipo siku atakana yote ya nyuma.
Ndo tunarudi kwenye kauli yako " Siasa za majitaka".