Tusikufuru CAG ni binadamu siyo Mungu!

Tusikufuru CAG ni binadamu siyo Mungu!

Natoa tu angalizo maana kuna watu hapa wanatamani Controller and Auditor General asiguswe kwa lolote.

Nasema hilo haliwezekani maana CAG ni cheo kinachobebwa na mtu na wala siyo Mungu kwahiyo yeye mwenyewe anaweza kuwa na mapungufu au wasaidizi wake tena ya kibinaadamu kabisa.

Kwa mfano kuna wizara, idara na taasisi nyingi za serikali ambazo zimepewa bajeti kidogo ukilinganisha na mwaka jana lakini watu wanamuona CAG pekee. Tena wengi wanaona ama ameonewa au anafanyiwa figisu za hujuma.

Watanzania tunaelekea wapi jamani, binafsi namkubali sana CAG wa sasa Alhaj Prof Assad lakini hiyo hainifanyi nimuone ni zaidi ya binadamu wengine.
Ni ukweli anaitendea haki dhamana yake lakini ni lazima tukubali kuwa ofisi yake ni ya kawaida tu kama zilivyo ofisi nyingine za serikali.

Niishie hapo
Maendeleo hayana vyama!
Tukaikague na ofisi ya Rais matumizi yake!!!!Pia na ofisi yake ipigwe panga!

Iko hivi,ofisi ya CAG haifanyi miradi bali bajeti yake ni kwa ajili ya kufanya majukumu yake ya ukaguzi!
Wizara kupunguziwa bajeti ni kutokana na mirado iliyokusudiwa!Mfano,baada ya miradi ya ujenzi ya SGR na umeme kukamilika,bajeti ya wizara ya ujenzi inaweza kupunguziwa bajeti kutokana na uhitaji wa wakati huo!!!

So CAG kupunguziwa Bajeti ina tafsiri moja,amepunguziwa uwezo wa kutekeleza majukumu yake!
 
Back
Top Bottom