Uncle bright
JF-Expert Member
- Feb 9, 2023
- 1,040
- 4,081
Kuna lawama baadhi ya watu huwa tunapewa kwamba tunataka kufanikiwa wenyewe, hatupendi ndugu wafanikiwe, anataka kuonekana peke yake ndie mwenye mafanikio kwao, n.k. ni kweli kuna baadhi ya watu hufanya hivi maksudi lakini sio wote.
Mtu unakuta ana kampuni yake, biashara yake ama yupo shirika /taasisi flani katika chenye mamlaka ama connection za kuweka watu lakini haweki ndugu zake sehemu aliyopo, anaona ni heri awatafutie kwa wengine ama shirika moja tawi jingine.
1. KUEPUKA DOUBLE STANDARDS - Kuna ndugu wakijua wewe ndie boss WANAVIMBA, yani ubishi na wafanyakazi wengine ni wao, ugomvi ni wao, kiburi na jeuri kwa wafanyakazi wengine ni wao, wana ile fikra kwamba "Hii ni kampuni yetu mimi ni sawa na boss". hapa ili kuepuka kuonekana unapendelea ndugu zako unaamua upige BLOCK.
2. KUEPUKA KUPUNGUZA UFANISI - Ndugu unampa kazi anakuja saa tatu asubuhi anawahi kuondoka kuna ufanisi hapo ? Kazi zinakuwa pending, yote haya anayafanya akijua kwamba hata mkifika mbali mtayamaliza kindugu.
3. KUEPUKA KUTENGWA ZAIDI - Hawa ndugu zetu ukianza kuwawawajibisha kwa makosa wanayofanya wanaanza kukuona unawanyanyasa na habari zinaeneoa ukoo mzima kwamba unaroho mbaya,
4. HOSTILE TAKEOVER - Hii inatokea Ndugu umemweka lakini yeye maelengo yake ni kuja kukuharibia / kukupindua achukue nafasi yako ama kukuondoa kabisa abaki yeye, hapo kuna kusagiwa kunguni mpaka kukuroga, n.k.
Mwisho niseme kuna jamii inakuwa rahisi kuweka hata ndugu kwasababu suala la kumwajibisha ndugu halionekani ni kunyanyasa, ndugu wanajiheshimu hawana mambo ya kuvimbia wafanyakazi wengine kisa wewe bosi, ndugu ni wachapakazi hawapunguzi ufanisi, n.k. hapa inakuwa rahisi sana kumweka ndugu yako.