sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,033
Biashara ntashirikisha familia yangu niliyoijenga (hasa watoto) ama familia niliyotokea (kaka, dada, wadogo zangu, wazazi), nje ya hapo hawa watoto wa mjomba, ma mkubwa, ba mkubwa, ba mdogo, ndugu flani, n.k. sidhani kwakweli, undugu uwepo na ninaweza kuwasaidia mitaji ama kuwasimesha pamoja na kuwa mteja wa biashara zao lakini tusiingiliane kwenye usimamizi wa Biashara zangu
Unakuta wafanyakazi wengine wanafika saa moja asubuhi ndugu anafika saa mbili ama tatu, Ndugu akiumwa hata mafua anaweza asije kazini, hii inanijengea chuki kwa wafanyakazi wengine kwa kuona nina upendeleo wa wazi wazi.
Kuna ndugu wanajikuta wao mabosi kuwa sawa na mimi kisa tu tuna undugu, wanapitiliza kuanza kuwavimbia wafanya kazi wengine, huanza kujiona miungu watu kwa wafanyakazi wengine, hawa ndugu wa kiume baadhi yao huanza kutumia nafasi hii kuwanyanyasa kingono wafanyakazi wa kike
Ndugu hasa wasio na majukumu wanaanza kunichora kwamba naingiza pesa nyingi, maneno yanaanza kupelekwa vijijini kwamba naingiza pesa nyingi lakini siwasaidii kwa uwiano wa kiasi nachoingiza, hapo hawajui kwamba nalipa marejesho ya mkopo, nalipa kodi, nalipa mishahara, nalipia ulinzi, n.k.