1.
Kama vile kenya kulivyo na ukabila,
Hawa wa-Kenya nimesema toka jana, kwamba ukweli wanasikitisha sana kwa sababu hii ya ukabila kwao imekuwa ni tatizo kubwa sana ambalo haliwezi kutatulika, that by it self I find it to be insane, siku moja nilihudhuria party nyumbani kwa balozi wa Kenya, I mean total insanity, kwenye party hiyo hiyo moja, ghorofa la juu kuna party ya wa-Kikuyu, na Basement kuna party ya Wa-Jaluo, lakini ni the same party ya balozi wao ambaye ni Mkikuyu, party nzima hakugusa chini kwa wa-Jaluo, at one point nikaamuuliza exactly what was going on? Akacheka tu na kusema hii mambo ya Kenya,
Mpaka leo asubuhi, wamekufa wananchi 125, swali ni for what? Ungetegemea jibu liwe kubakwa kwa Demokrasia, Yes in one way, then comes ukabila and you are lost, maana too many explainations, maana now you have to go kuanzia kwenye foundations za hivi vyama, ambako utakuta too much ishus ambazo hazihusiani kabisa na siasa wala Demokrasia, bali ukabila,
According to the dataz, investment kubwa za Wazungu zipo hasa Nairobi, na hao wawekezaji ndio haa wenye upperhand kwenye ku-influence matokeo ya uchaguzi hasa wa rais, nasikia kabla hata uchaguzi haujafanyika wa-Kikuyu, walishapanga plan A, and B, moja ya kujaribu kushinda kwa kura, na nyingine waliyoitumia jana baada ya kushindwa kura, huku Jeshi na GSU wakiwaonya tume ya uchaguzi kuwa wako tayari kwenda msituni iwapo Kibaki angeshindwa, Mwenyekiti wa tume akawakimbia waandishi chumba kimoja na kukimbilia chumba kingine na kutangaza kuwa Kibaki ndiye mshindi, the next thing US imeitambua serikali ya Kibaki, a big joke!
Kibaki na Odinga, one time walikuwa patners for Ikulu kwenye NARCO, upinzani bongo tuliwakumbatia sana hawa jamaa, lakini the minute tu walipopata power, Odinga akaja bongo na kuzungumza na waandishi pale Maelezo, akasema tena bila aibu kuwa NARCO have nothing to do na upinzani wa Tanzania kwa sababu wao sasa NARCO ni watawala kama CCM, kwa hiyo wako samba samba na CCM not upinzani. Now Odinga anajua fika kuwa njia zote walizozitumia kuingia Ikulu hazikuwa safi, na in one way or another kulikuwa pia na mkono wa Moi, kwenye kuwasaidia, sasa this time arround exactly alitegemea nini kitafanyika tofauti? Hizi political affiliations za dakika za mwisho kabla ya uchaguzi ili kukimbilia Ikulu tu zinaweza vipi kuzaa matunda mema kwa taifa?
Ukweli ni kwamba ishu kama hizi zinatukumbusha moja ya political legacy na ustaarabu wa Mwalimu, kutoruhusu huu upuuuzi bongo, I mean hawa ni watu gani ambao mpaka leo 2007, bado hawawezi kuachana na mizizi ya ukabila? Leo ukienda Nairobi, ni kawaida kusikia wananchi wakiongea kwa lugha zao, hebu jaribu kuongea kwa nguvu lugha yako Dar, uone wananchi watakvyokushangaa, halafu sio wa-Kenya tu, hata wa-Rundi, wa-Zaire, wa-Burundi ni ujinga ule ule tu, sasa kweli eti tunaungana nao kwenye EAC hawa? Wanaotuburuza huko EAC na hawa watu wa kuja kweli wanahitaji kutueleza kwa kirefu kulikoni hasa?
2.
siku za karibuni mambo mengi tanzania yanaangaliwa kwa misingi ya kidini. Majina ya watu (ya kiarabu VS ya kikristo) yanatumika sana siku hizi katika mambo mengi tu Tanzania.
Kwa kweli in general siamini kuwa hii sasa hivi ni ishu kubwa sana bongo, au kwamba tmefikia hatua mbaya sana mpaka ya kupewa our national attention, sasa inaonekana kuwa tuna un-written rule kama taifa ya kupokezana urais kati ya wa-Kristo na wa-Islam, sasa kuna the obvious kuwa rais akiwa dini flani lazima atachagua viongozi wengi wa kumsaidia kutoka dini yake na hata kabila lake, in Mwalimu case aliwatumia sana watu wa kabila lake kwenye nafasi muhimu, Mwinyi aliwatumia watu wa dini yake, Muungwana, ninaweza kusema kuwa angalau amekuwa fair somehow, ingawa onetime na yeye alianza kutumbukia kwenye dini lakini nfikri makelele yalimshitua na akaacha kama sio kupunguza,
Lakini kama kuna dataz ziwekwe tujue ukweli, lakini binafsi bado siwezi kumhukumu Muungwana, kwenye hili na sina uhakika kama bongo tunaelekea au tuko kwenye hali mbaya na hili, kwa kweli labda zitolewe more evidence, maana ya hawa wa-Kenya bado hatujafikia wakuu tena tumshukuru Mungu kwa hili.
Ahsante Wakuu.