Tuongelee matumizi ya mitandao na athari zake!

Tuongelee matumizi ya mitandao na athari zake!

Gorgeousmimi

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2010
Posts
9,296
Reaction score
7,713
  • Jamani sisi wana wa kizazi hiki tumekuwa digitalized mno,kila mtu anachofanya kwenye maisha yake kipo kwenye mitandao tofauti ya jamii kama ni facebook,twitter,instagram n.k Wenzangu mnalichukuliaje swala hili?
Hata mtu akila apple ata andika na picha atajipiga akilitafuna :confused3:
apple bite.jpg
NAKAA NIKIJIULIZA TUNAPOTEZA SIFA ZA KUSOCIALIZE KIKAWAIDA MPAKA TUMEKUWA WATUMWA WA MITANDAO TOFAUTI?
  • Imekuwa kama fasheni kwa sasa kuweka picha zisizo na maadili pamoja na kuwa na marafiki wengi tusiowafahamu walio katika mabara tofauti ya dunia.Je athari za kuweka picha zetu na personal information kwenye mitandao tofauti tunazipa uzito gani?
  • Kwa wazazi athari za kuweka picha za watoto wetu ambazo tunajua wakija kukua zitawaaibisha na hata kuwaathiri tunalichukuliaje?
  • Nakubali kuna faida nyingi za mitandao hii na imeunganisha watu wengi,lakini je tunaitumia ipasavyo?Kama sasa hali ipo hivi miaka 10 ijayo itakuwaje?sidhani kama hata watu wanasemeshana kwa midomo,kila aina ya mawasiliano itakuwa kwa maandishi,kupitia kwenye simu,computer n.k
  • Athari zake kiafya lipoje?madaktari mnakaribishwa kuliongelea hili,nchini china asilimia kubwa ya watoto wanavaa miwani kutokana na muongezeko wa kutumia vifaa vya kidijitali!Je tunawalemaza watoto na uwezo wao wakujichanganya na watoto wengine kwa matumizi ya vifaa tofauti vya kiteknolojia?Je tunawapunguzia uwezo wao wa kuwa kuunda michezo ya aina tofauti kwa hali hio?
  • Je mitandao hii inajenga au inabomoa?
Cc gfsonwin Mtambuzi Eiyer AshaDii OLESAIDIMU Mr Rocky Kongosho Preta Dr.Mo asakuta same moto2012 ladyfurahia Himidini venine 64Bits Mrs leo Evelyn Salt Smile Ennie Kaizer Asprin Dark City Isumbwile Munkari Eli79 Chocs Viol miss neddy Bantu lady watu8 Mentor christine ibrahim Blessed Ablessed snowhite Kaunga Fixed Point Mndengereko MziziMkavu Karucee Nyani Ngabu FaizaFoxy Kiranga Dr. wasengamila daviey69 TANMO Mearkson na wengineo nilowasahau
 
Last edited by a moderator:
We hulali? Upweke ndo unafanya watu wahamie mitandaoni...wakipata watu wa kuwa keep busy huwaoni...
Nakubali upweke ni sababu mojawapo?Wewe upo fesibuku,insta au twitter mkuu?
 
Nipo jf..wewe Unataka kuni add huko?
hapana,mimi situmii mitandao hio,Naomba nikuulize kwanini hujichanganyi kwenye mitandao hio?Ni kwasababu ya umri au?Kuna tofauti kubwa ya JF na huko nilipokutaja na ni ANONYMOSITY,Huko kwengine information zako au picha zako zinaweza kuwa kwenye internet for decades na zikatumika ovyo kabisaaaaa!
 
It depends na aina ya watu unao jimix nao...usisahau hata kina Obama wapo online..mimi nipo kwa kiasi
 
It depends na aina ya watu unao jimix nao...usisahau hata kina Obama wapo online..mimi nipo kwa kiasi
Sikatai kuhusu watu kuwepo online lakini namaanisha matumizi yasio sahihi,hukuti obama kaweka picha kanyoa kiduku right kwasababu lazima kuna jinsi ambayo anatakiwa ajirepresent!kitu ambacho watu wengi wanajisahau na kujiachia tu!
 
Jamii naombeni mnisaidiemtu anaefahamu wapi wanauza computer mpya tena owe flat screen na warrant 1 year nitashukuru kama kuna mtu anafahamu Duka la karibu hapa dar...
Nahitaji haraka sana lakn ninafahamu haizidi gharama yangu ya mfukoni ila nipe jina la sehemu lkn pia BEI zake...
 
game-mlimani city,bei nimesahau
 
Athari ziko nyingi sana lakini mimi niseme tu kuwa tatizo kubwa ni watumiaji wengi kukosa elimu sahihi juu ya matumizi sahihi ya mitandandao ya kijamii pamoja na vifaa vya teknolojia kama simu,tablets,pc nk. Tukiweza kubaini chanzo cha tatizo basi ni rahisi kupunguza athari!
***naurushweeeeee***
 
Mitandao ya kijamii pia inasababisha watu kushindwa hata kutembeleana,na hapo ndo ubinadam unapoisha,maana kila jambo laishia mitandaon,,,kuna masuala mengi kuhusu social capital na social networks ntayazungumzia kukikucha

Kutembeleana ili iweje? Ujamaa umetuathiri sana waTz
 
Athari ziko nyingi sana lakini mimi niseme tu kuwa tatizo kubwa ni watumiaji wengi kukosa elimu sahihi juu ya matumizi sahihi ya mitandandao ya kijamii pamoja na vifaa vya teknolojia kama simu,tablets,pc nk. Tukiweza kubaini chanzo cha tatizo basi ni rahisi kupunguza athari!
***naurushweeeeee***

Hicho kibwagizo kimenikumbusha mbali wallah

Cc Angel Nylon

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
pia jamii forums ni moja wapo ya mitandao hiyo tajwa!
kwa upande wangu nakubaliana na mabadiliko na mapinduzi ya sayansi na teknolojia lakini siungi mkono matumizi hasi ya mitandao! kikubwa ni kuielimisha jamii na watoto juu ya matumizi chanya pia viwepo vyombo vya kudhibiti uvunjifu wa maadili
 
Mitandao ni mizuri na mibaya ni jinc utakavyoitumia mwenyewe na utajipangaje isikutawale akili ukashindwa kufanya mengine ukweli kwa ss imechukua kasi ya ajabu
 
Basically wabongo sie ni watu wa kuiga blindly, na vijana wengi ndio waathirika wakubwa wa social networks, zimekuja pahala ambapo watu hawafaham matumizi yake sahihi, na uhuru wa kujianika utakavyo,kufanya utakacho ndio umevutia wengi mno.
Athari ni nyingi mno hususan kiuchumi na kijamii.Najua sote twakubali kuwa ndoa na mahusiano mengi mno yamevunjika ama yapo hatarini kwa ajili ya matumiz hasi ya simu na social networks.
Kuporomoka kwa uwajibikaji. Vijana wengi hawajishughulishi badala yake hutumia muda mwingi kufanya chit chat, kuperuzi na ku post ujinga kwenye social networks,ilhali wanajididimiza kiuchumi.
 
Jamii naombeni mnisaidiemtu anaefahamu wapi wanauza computer mpya tena owe flat screen na warrant 1 year nitashukuru kama kuna mtu anafahamu Duka la karibu hapa dar...
Nahitaji haraka sana lakn ninafahamu haizidi gharama yangu ya mfukoni ila nipe jina la sehemu lkn pia BEI zake...

Uhuru computers Kariakoo round about ya uhuru, pia kuna maduka mengine mengi tu mtaa huo.
 
Asante kwa mada nzuri. Mimi wacha niwe nimepitwa ila fb, twiter, instg, huko sipo kabisa. Na haya yanayoendelea kwenye jamii zetu ni hali ya hatari, wazungu wanatuweka busy kila dakika. Ni hatari zaidi kwa watoto wazazi mlione hili
 
Back
Top Bottom