Tuongelee matumizi ya mitandao na athari zake!

Tuongelee matumizi ya mitandao na athari zake!

  • Seduction...
  • Need for attention....
  • Sexual abbcession....
Sasa ndo ukute bibie kamtumia boya mwingine picha ya namna hiyo halafu uso mkavu kabisa anakuambia"si picha ya kawaida tu" kweli?

Sometimes a man must audit his house this includes uwepoji wake kwenye mitandao ya jamii na madhumuni yake!

Usemi wa kusema "ni kutojiamini au unatafuta presha" natupa kule! Kikubwa learn how to deal with it afterwards(baada ya kukuta report ya audit ni mbaya) unafukizia mbali au unaweka mitambo au system ya kisasa ambayo haina urafiki na michepuko? kusuka na kunyoa ndo can be solution!

I hate surprises.....
 
1.Athari za kisaikolojia hasa pale mtu anapokutana na negative comments kutoka kwa marafiki,kukosa "like" na positive comments juu ya "selfie" aliyopost.ikumbukwe kule watu hujuana na si kama hapa.hii inaweza kumuathiri mtu kujiona HAFAI(Self negligence) na kushindwa kujikubali,pia kuweza kuleta msongo wa mawazo,kutojiamin n.k.
2.ni rahisi kupata details za mtu A-Z
3. Utu na ubinaadamu hupungua...siku hizi mtu anakualika harusi fb, ule utaratibu wa kutembeleana na kupeana taarifa kwa kuonesha umuhimu wa mtu unatoweka.mimi ukinialika harusi fb SIJI kabisa kwenye harusi yako!nahisi hujanipa thamani yangu,kama niko mbali ni bora unipigie simu kuliko kupost status na kunitag eti ndo umenialika.
4.Mmomonyoko wa maadili, kule hakuna moderator kama hapa, ni HOLELA tu, sasa si tu vijana huharibika lakini hata watu wazima wamekuwa WATOTO.
5......
Ahsante kwa kufunguka kwako rafiki...Naafiki hili suala la kupata details za mtu ni hatari sana kwasababu mtu hujuani nae,anaweza kukufanyia kitu mbaya na wewe hata usimjue ni nani!!Kwa mtazamo wangu mimi naona hizo social Networks zinadumaza watu na waapoteza hata skills za kusocialize,usishagae hata watu hawaeshi kuanzisha Uzi wakiomba msaada wa kutongoza kwasababu in general hawajui kjiexpress mbele ya mtu/watu.Na hata unaweza kukuta mtu anaiga kitu kwasababu fulani kafanya bila kujua kitu hiko kinaleta tafsiri gani na kimebeba maudhui yepi?!!
 
Globalization... nafikiri mtu achague kinachomfaa ambacho hakitaleta madhara kwake au kwa mtu wake wa karibu

Binafsi siamini saana kwenye hizi social networks kwani mwisho wake si mzuri (ugomvi na hata kuvunjika kwa uhusiano kwa wapenzi na huleta shida kwenye ndoa)

Sipo fb,wtsup,twitter na zingine zifananazo na hizo na hii yote najaribu kuepuka matatizo ambayo mifano hai ninayo ya ndugu na marafiki..sitaki kabisa

Zaidi nipo jf na nina email kwa maswala ya kikaz only.
 
My deep concern ni kwa watoto kwani importantly wao ndo taifa la kesho, ukweli ni kwamba effects zipo nyingi sana in comparison na benefits thus its very vital kwa wazazi/walezi kuwa makini with them on ensuring wanapata the benefits instead of the opposite gorgeousmimi
 
Last edited by a moderator:
My deep concern ni kwa watoto kwani importantly wao ndo taifa la kesho, ukweli ni kwamba effects zipo nyingi sana in comparison na benefits thus its very vital kwa wazazi/walezi kuwa makini with them on ensuring wanapata the benefits instead of the opposite gorgeousmimi
Yaani watoto wa sasa akianza shule tu anakwambia nifungulie facebook account!Tunapaswa tuwe makini sana tena sana rafiki,maana tunakoelekea si kuzuri kabisa!!
 
Kama usiposhinda mtandaoni muda mrefu, je madhara ya matumizi yaliyopitiliza ya mitandao tutayapima vipi?
Kwa output both -ve and +ve anayeipata mtumiaji na iwe judged na mtu mwingine!
 
Cellphones, Facebook and
WhatsApp can bless or break
marriages. Used within the
parameters of marriage these can
greatly enhance communication
between husband and wife.
Unfortunately many marriages
have failed around cellphones,
Facebook and WhatsApp. Protect
your marriage, respect your spouse
and don’t lead yourself into
temptation. Avoid secret
communications and intimate
conversations and private chatting
with people of the opposite sex. Be
accountable to one another. Have
an open cellphone policy with your
spouse. If you must have a
password on your phone or
computer let your spouse know
about it. You and your spouse are
one. There is absolutely no
business or conversation that your
spouse shouldn’t know about.
Openness builds trust. #
 
I was watching a Steve Harvey show episode on this, kuna mama.mmoja anasema lazima awe na simu yake ana soma na ku update social media.
 
Mitandao ya kijamii haina ubaya wowote, kwa sababu maudhui yake hayana ubaya..Lakini pia inategemea mtu kajiunga mtandaoni kwa madhumuni gani, anajihusisha na nani.

Mfano, mitandao kama facebook, skype huwezi kuwa na marafiki usiojuana nao kiuhalisia. Nipo facebook/skype ila 100% ya marafiki zangu nawafahamu na wengi wao ni watu wangu wa karibu. Tatizo linakuja kwa wengi wetu, kwanza kutumia fake IDs (as if tupo jf), pili kuwa na list ya watu hata hatuwajui na tatu kutumia mitandao kama daraja la kutengeneza marafiki. Kuna watu hutumia facebook/skype kutafuta marafiki, mimi nilidhani ukikutana na mtu, baada ya kujenga hali ya kufahamiana hapo ndo unaweza kumfanya awe rafiki wa facebook, ila sivyo wengi tunavyofanya.

Maudhui ya hii mitandao sio mabaya, watumiaji ndo hawajui limits za matumizi.
 
Nakumbuka miaka ya 2000 hivi tulikua tunasema dunia imekua kijiji kwa sababu ya internet lkn sasa hivi dunia ni chumba kwani internet imetuondoa kwenye kijiji na kutuleta chumbani/livingroom. Yote hii ni ktk kufanya mawasiliano kuwa rahisi.

Back to topic. Mitandao kama ilivyo kwa vitu vingine ina faida na hasara kumbuka ktk kila kitu kunapaswa kua na kiasi. Uingi wa faida au hasara unategemea na jinzi mhusika atumiavyo mitandao hiyo. Kwa hapa kwetu Tanzania wanaotumia mitandao ni wachache sana kutoka na mazingira tunayoishi , ingawa kwa kuangalia haraka haraka unaweza kufikiri watumiaji ni wengi kumbe la hasha wenye hiyo access ni wachache sana.

Tunaposema wengi wanatumia vibaya tunaweza kuwa sahihi lkn huenda ni vizuri kujua kuwa kila mtu ana lengo lake na tumetofautiana kama ilivyo mitaani kwetu. Kuna wanaotumia mitandao kwa kuuza miili yao si unajua kidijitali zaidi . Huwezi kukuta mtu mwenye staha kaweka picha anakula sijui nini, tujue tu kuwa wengine wapo kibiashara na inawasaidia wanatimiza malengo yao. Sitaki kuhukumu au kusema vibaya lkn utakuta wengine wanatumiana picha za utupu tena watu usiowatarajia wanafikiri wako salama kwa mfano fb. Hasara zipo kama wengine walivyotangulia kueleza.

Faida za mitandao zipo na ni nyingi kwa kweli , mitandao imesaidia kukutanisha watu tena kama umepotezana na watu miaka mingi unaweza kuwapata kupitia mitandao. Nakumbuka mwaka jana niliweza kukutana na jamaa zangu kupitia fb nilipotezana nao miaka mingi na sikujua wapo wapi. Inakutanisha watu pamoja hasa wale ambao haiwezekani kutembeleana kwa mfano mtu wa dar na mwanza wanaweza kukutana kwa njia ya mtandao na ikawa kama kwamba wapo pamoja na hii inaprove kua dunia imekua room na si kijiji. Pia mitandao inasaidia Kufanya biashara mbali mbali zikiwemo halali na haramu, kujua bidhaa flani zinakopatikana, kupata wachumba, kupata ajira, na mengine mengi kama kuongeza marafiki, kuondoa stress hebu ona mtandao kama jf si stress remover jamani.

Kwa kifupi mitandao ina faida kubwa sna ktk jamii inaelimisha na kuiweka jamii pamoja kwa mfano tumeweza kujua uongo wa baadhi ya taarifa za magazeti kwa njia ya kuangalia chanzo halisi cha taarifa, tumejua tanganyika na historia yake, tumejua kwanini tuliitwa manyani na wazungu, tumefuatilia bunge la katiba kwa karibu n.k. Sijui mitandao mingine inavyofanya kazi naijua michache kama jf,fb, linkedln na skype na hiyo ndio niliyoiongelea hapa. Angalizo kwenye mitandao hakuna privacy hackers wako wengi na wanaingia sana kwenye hiyo mitandao kwa mfano usijuiamini na pm huko bwana kunaingilika tu hasa mtu akihack account yako. Kwa wanaotumia fb huko ndo usiseme hackers wanashinda huko na wanaview mawasiliano yote so be careful mtumiaji.
 
madhumuni ya mitandao ni mazuri tatizo watu wengi wana-abuse matumizi yake. anyway, kila mtu ana access na social networks, swala la matumizi mazuri au mabaya linabaki kuwa responsibility ya mtu binafsi.
Ni upumbavu kuamua social network iharibu mfano mahusiano yako na mwenzako, au ikufanye usifanye kazi na kufikia malengo uliyojiwekea sababu ya kushinda mitandaoni, au upoteze respect mbele za watu kwa sbb ya kupost mambo yasiyokuwa na maana
 
Well said mkuu... Yaan mfano mie nisipoingia JF na kuwa online wozap nahisi nimepungukiwa kitu fulani... But Thanks God sipo kwenye social network nyingine tofauti na JF na Wozap....

:backtotopic:

Social network ni nzuri ikitumiwa vyema as too much of anything is harmful...

Unakuta mtu yuko yuko active social network zaidi ya 7 sasa huyu ana concentrate kwenye shughuli, kazi au masomo yake saa ngapi???
wengine social network ndo shughuli zao. usisahau hilo.jf mimi ndo social network mama kwingine huwa napita tu kuangalia whats going on baaasi.
 
Ahsante kwa kufunguka kwako rafiki...Naafiki hili suala la kupata details za mtu ni hatari sana kwasababu mtu hujuani nae,anaweza kukufanyia kitu mbaya na wewe hata usimjue ni nani!!Kwa mtazamo wangu mimi naona hizo social Networks zinadumaza watu na waapoteza hata skills za kusocialize,usishagae hata watu hawaeshi kuanzisha Uzi wakiomba msaada wa kutongoza kwasababu in general hawajui kjiexpress mbele ya mtu/watu.Na hata unaweza kukuta mtu anaiga kitu kwasababu fulani kafanya bila kujua kitu hiko kinaleta tafsiri gani na kimebeba maudhui yepi?!!

You are very right...BAADHI ya wanaume walio wengi kwa sasa wanapoteza ile confidence na hawawezi kujieleza mbele ya watu na hasa wale wanaowapenda yaani hawajui kutongoza ile ya kuvuta attention ya binti na kuweza kumbadili mtazamo akubaliane nayo. Msaada mkubwa wanapata kwa hizi social networks mana mtu anaweza kuandika bila kuonekana lakini ingekuwa ni uso kwa uso basi duuuh dume ungeona linavyohaha maneno hayatoki kama kameza sound proof mdomoni
 
ATHARI ZA MITANDAO JA KIJAMII

1.Kuwepo kwa watu ambao wako tayari kutetea(justify) kila kitu toka nchi za west bila kujali athari.
2.kuwa na watu wenye poor thinking and reasoning capacities;hakuna mawazo
,fikra mpya zaidi ya mapenzi.Ni nani anaweza sema kawa creative,innovative via s/media?
3.Kushinda kwenye s/media ni ishara ya kutokuwa na majukumu/kutowajibika. Kwa mtu mwenye mipango ya kazi zake,biashara zake,maendeleo yake hana muda na hayo makitu.

FAIDA ZA S/MEDIA NI NYINGI ILA ZA KUFIKIRIKA.
 
mitandao ni mizuri kama unatumia for news,business,learning,refreshing via books,stories,mawasiliano


social networks kama fb zinaathiri watu mf,mtu usipo pewa like you feel you worth nothing hivyo kupoteza mda kutafuta kipi upate like hata kama cha kipuuzi



wastage of time kudiscuss watu badala ya ideas

Pointi ya mwisho inawahusu watumiaji wengi.WENYE AKILI NDOGO WANAFIKIRI NDIO KWENDA NA WAKATI.
 
Yaani watoto wa sasa akianza shule tu anakwambia nifungulie facebook account!Tunapaswa tuwe makini sana tena sana rafiki,maana tunakoelekea si kuzuri kabisa!!

je yawezekana ni mojawapo ya mpango ya new world order.kwamba watu wako so bize na issue za kupenzika kana kwamba mapenzi yameanza mwaka 2014.!
 
Back
Top Bottom