Tambwe Hiza si mtu ambaye CCM ingempatia cheo kama hicho, mtu wa propaganda si kufanya kazi ya uropokaji........Makamba hana uwezo mkubwa kuongoza chama hicho kielimu na utashi na amekuwa akikumbatia mambumbu kama akina hiza kwani anaogopa challenges kutoka kwa wenye upeo mkubwa.. Ndugu zangu hali ya kisiasa pale Lumumba si nzuri, watu wananuniana...wanafitiniana....hawasalimiani......Na makamba hata katika mchakato wa Chama mwaka jana alipokea fedha sana kwa wagombea hata wachafu kama kinyesi.... Pale Morogoro kwake alimweka mtoto wake mmoja ndo alikuwa anapokea fedha za rushwa na nasikia kwa kuwa JEYKEY naye anamsikiliza huyu jamaa sijui ni kwa nini lakini inasememekana hata ukuu wa Wilaya na ukuu wa mikoa watu wanapeleka fedha kwa Makamba ili amshawishi Kikwete awateuwe na wengi ni walewaleeeeee ambao hata hawajui la kwenda kufanya.
Ukweli lazima mabadiliko kwa ukombozi wa Taifa hili, tutajutia kwa haya......Mungu atupe nguvu tujitambue....Hata wale majuha walipo humu wanaotumiwa na mafisi wenzao kutafuna nchi yetu tusipoteze muda kulumbana nao wengine ni hao akina RZ1, EL nk ama wafuasi wao......Mabadiliko katika nchi hii ni lazima kama mtu unaitakia mema nchi hii na naamini yanakuja na katika historia ya tanzania kuna watu baada ya uchaguzi wa 2015 watapelekwa the Hague namsii IGP na DGTISS wajue wao ndo watakuwa wakwanza kwani CCM kwa hali ilivyo haitashinda na CCM chini ya rais anayemaliza kipindi chake atataka ailinde CCM isipotee mikononi mwake kama KANU na kwa hivo basi atachakachua vibaya sana na watu wahatakubali wataingia barabarani, wao watatuma FFU na vifaru mtaani kuuwa kama ARUSHA na hapo ndo cha moto watakiona......Tunahitaji taathira njema katika nchi hii.......tunahitaji Tanzania yenye ustawi kwa vizazi vijavyo........Tunahitaji kuutafuta sasa Uhuru wa kweli katikanchi hii....Hii inawezekana kwani nataka niwambie ukijua hata ile siri ya ARUSHA na ukipita katika makambi ya majeshi ukayasikia wanayoyasema na mikakati iliyopo kuunga mkono mabadiliko, inatia moyo kuwa mabadiliko yanakuja........kwa taarifa yenu hata pale ARUSHA polisi walikufa hasa makuruta na Polisi wakatoa taarifa kuwa wamekufa mafunzoni........nawambia itafika siku Polisi na Majeshi watapigana risasi wenyewe kwa kupinga mauaji ya raia wanaotaka kuikomboa nchi hii.......Arusha juzi imetokea, siri kubwa imefichwa ndugu zangu........Nchi sasa si salama na Usalama wa Taifa nusu yao wanataka mabadiliko......Hivi mishahara ya polisi ya 120,000 maisha ya leo wakati IGP na makamishna wenzie wanalipwa mishahara minono, CDF, wakurugenzi na waandamizi TISS na majeshi mengine wanalipwa mishahara na marupurupu manono na rushwa na vibahasha juu.......wakati wafanyakazi wadogo wana wanalipwa 200,000 kwa TISS na 120,000 kwa Polisi hivi maisha ya leo kweli wataunga mkono CCM? Halafu viongozi wanaona wapo salama kwa ulinzi wa watu wenye njaa wanaoponea viposho vya safari ambavyo wakistaafu haviwasaidii kujipatia fedha ya kustaafu inayotosha walau miaka miwili ya maisha ya kustaafu? Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa ujue nchi hii ikiangukia katika matatizo utabeba lawama kubwa kuwa hukutekeleza wajibu wako......Je hamusemi, hamreport au bado tuna usalama wa kizamani wa kulinda maslahi ya Chama na watu badala ya maslahi ya nchi? Acha legacy Tanzania ukumbukwe kama akina Mzema wailiokuwa wanawakata mafisadi na kuwafunga vitambaa usoni na kuwaficha ili wasiendelee kusumbua na kuharibu ama kuhujumu Taifa......nyie mpompo tu......watu wanafanya watakavyo.....Maafisa wengi wanaishi maisha ya shida.....Nchi hii sasa si salama kama unaendelea kukaa kimya ipo siku kama utasoma hii post utaikumbuka..........nakwambia karibu nusu ya Maafisa wako wamechoshwa na hali hii.......wanareport hamchukui hatua kwa nini msimweleze Raisi kuwa atekeleze maagizo yenu kama hataki msusieni nchi kama atajiongoza maana pamoja na kiburi cha viongozi bado tegemeo lipo kwenu, juzi anawambia hatalipa Dowans, leo anageuka kuwa atalipa anawadanganya, nyie mmekuwa watoto? Nimeandika kwa uchungu kama Mzalendo, na mnisamehe kwa kuandika post kubwa inaweza wachosha kusoma lakini mfahamu hii ni nchi yetu, tunataka mstakabari wenye taathira njema kwa vizazi vijzvyo.......Nimesema hata yale ambayo pengine hayakustahiri sana lakini nataka wakuu wa vyombo vya dola wafahamu kuwa nchi hailindwi na vifaru ni amani inayojengwa na uzalendo wa viongozi ambao huwa ni mwelekeo wa wananchi, Tunisia huwezi linganisha na sisi lakini wameshindwa kupeleka vifaru mtaani Raisi akakimbia, hatutaki yatokee hapa kwetu, lakini kama hizo kazi mmezomea mfahamu kuwa yakija haribika hamtazima, mtakuwa mmechelewa.......mtabeba lawama, ujueni ukweli wa Arusha siri hii mnayo, nimesema mno