Tuondoleeni utata huu wa taarifa za kifo cha mke wa Askofu wa Anglikana Biharamulo

johnmashilatu

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
718
703
Taarifa zinasema kuwa Mke wa Askofu Vitalis Yusuf, wa kanisa la Anglikan Dayosisi ya Biharamulo mkoani Kagera, maziko yake yatafanyika leo Jumamosi nyumbani kwao wilayani Chato mkoani Geita.

Maziko hayo yanafuatia, kifo cha mke huyo Monica Zablon mwenye umri wa miaka 45, kilichotokea usiku wa kuamkia Jumatatu wiki hii katika mazingira ambayo yameibua utata wa pandetatu.

Habari za awali zilizotollewa na Msaidizi wa Askofu Vitalis, kwa vymbo vy habari zinasema mwili wa mwanamke huyo ulikutwa kando ya njia ya kuelekea kwao (na mwanammke) ambako alikuwa amekwenda kuwatenbelea baada ya kupata nafuu kutoka hospitali ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.

Msaidizi huyo wa askofu anassema, mwanamke huyo alitoka nyumbani akidai kwenda kufanya mazoezi akiambatana na mtoto wa kiume mwenye umri unaokadiriwa kuwa miaka 10, na walipofika njiani walikutana na mwanaume ambaye alikuwa akifahamiana na mke wa Askofu Vitalis ambaye alimtaka, mtoto huyo awaachie nafasi wazungumze lakini baadaye walipotelea vichakani.

Mwili wa mwanamke huyo alipatikana sikuya Jumatatu akiiwa amekufa.Na hapa ndio Issue ya polisi inapoingia. Katika taarifa yake ya iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari RPC wa Geita, Sofia Jongo anasema, polisi walikuta mwili umefunikwa nguo, ukakaguliwa na mganga wa zahanati ya jirani na kuthibitisha kuwa mke huyo wa Marehemu "alijinyonga".

Baadaye waliitwa madaktari sita(6) kufanya uchunguzi ambao wao sio tu walibaini alijinyonga bali sababu za kujinyonga kwake ni baada ya kuugua kwa muda mrefu!

Taarifa hiii inanikumbusha Daktari wa serikali ya MOI aliyefanya uchunguzi wa kifo cha Robert Ouko, ambayye alihitimisha kwa kusema "Ouko, alijipiga risasi na baadaye akajichoma moto".

kuna taarifa kuwa baadhi ya viongozi wa Kanisa la Anglikan pamoja na ndugu wa mwanamke huyo hawajaridhishwa na taarifa za polisi kuhusu uchunguzi huo na huenda wakaomba maziko yasitishwe kwa muda ili kutoa nafasi ya uchunguzi.
 
Kuna story Mbili tofauti hapa au?
Mkuu.
Kamanda huyu wa Polisi anayependa kuonekana kwenye vyombo vya habari, anapaswa kufanya kazi kwa weledi. Yule mwanaume aliyekuwa akiongea na mke wa Askofu ni nani?, waliongea nini?, hakuhusika "kunyonga" kwanini Conclusion ya polisi ni " amejinyonga"'?
 
Back
Top Bottom