Askofu Mndolwa athibitisha kifo cha mke wa Askofu Vithalis Yusuph

Igwe Kingdom

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
266
441
Pole Baba Askofu Vithalis Yusufu wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Biharamulo na familia yako, Poleni nyote wana Kanisa Anglikana Tanzania, Pole kwa Kanisa la Mungu popote Ulimwenguni na wote walioguswa na msiba huu. Ni msiba mzito unaoacha maswali mengi. Faraja ya Mwenyezi Mungu iwe na kila mmoja katika kipindi hiki kigumu sana hasa kwa familia ya Baba Askofu Vithalis Yusufu.

ASKOFU MNDOLWA ATHIBITISHA KIFO CHA MKE WA ASKOFU VITHALIS BIHARAMULO.

Na Maiko Luoga.

Muhashamu Baba Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania na Dayosisi ya Tanga Maimbo Mndolwa ametangaza kifo cha Monica Vithalis Yusuph mke wa Askofu wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Biharamulo Vithalis Yusuph.

Askofu Mndolwa amesema mwili wa Monica mke wa Askofu Vithalis umekutwa leo novemba 08, 2023 ukiwa umetelekezwa kando ya Barabara katika kijiji cha Kasenga wilayani Chato mkoa wa Geita ukiwa na kamba shingoni, chanzo cha kifo hicho hakijafahamika.

Hatahivyo Askofu Mkuu Mndolwa ametoa wito kwa waumini na wahudumu wa Kanisa Anglikana Tanzania kuwa watulivu katika kipindi hiki na kuendelea kuombea familia ya Askofu Vithalis na Dayosisi ya Biharamulo ili Mungu awe faraja kwao wakati kanisa likisubiri taarifa ya uchunguzi kutoka kwa vyombo husika.

Amesema mara baada ya taratibu kukamilika Kanisa litatoa ratiba kamili ya msiba huo sambamba na siku ya ibada ya mazishi, Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe Amin.
 
Duh imekuaje tena hapa??
 
R.I.P mama mchungaji
 
Huu utawala wa nchi hii!! Hali ni mbaya kila kona!
1. Mauaji
2. Ubakaji
3. Ulawiti
4. Wizi
5. Ufisadi
6. Hakuna haki tena mahakamani
 
Stori bado ipo hewani, alifikaje barabani? Alikuwa na ugomvi na jirani, mwenza?
 
Pole nyingi kwa wafiwa. Ingawa kifo chenyewe kinaonekana kuwa na utata mwingi.
 
Back
Top Bottom