Tunisia: Waandishi wa Habari waandamana kupinga Sheria za kupambana na ugaidi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Waandishi hao wa Habari wanapinga kile wanachosema kuwa ni Sheria kandamizi dhidi ya ugaidi iliyoundwa kuvitisha vyombo vya habari.

Wameandamana wakiwa na mabango nje ya makao makuu ya muungano wa Wanahabari wa Kitaifa, wakitangaza kuwa uhuru unategemea uhuru wa vyombo vya habari.

Mei 16, 2023 Mahakama ya Rufaa ilimfunga Mwandishi wa Habari wa Redio, Khalifa Guesmi, kwa miaka mitano - na kuongeza kifungo chake cha awali mara tano - kwa kufichua habari kuhusu huduma za usalama za Tunisia.

Afisa wa Polisi aliyepatikana na hatia ya kumpa habari naye amefungwa miaka 10 jela.

Wakosoaji wanamtuhumu Rais Kais Saied kwa kuielekeza Tunisia kuelekea udikteta.

Shirika la kutetea haki za wanahabari, Reporters Without Borders limesema hukumu ya Guesmi ilituma ujumbe "wa kutisha" kwa vyombo vya habari nchini humo.
---

Tunisian journalists rally against anti-terror laws

Dozens of journalists in Tunisia have held a demonstration against what they say are repressive anti-terror laws designed to intimidate the media.

They brandished placards outside the national journalists' union headquarters, declaring that liberty depends on press freedom.

On Tuesday an appeals court jailed a radio journalist, Khalifa Guesmi, for five years - increasing his earlier sentence by five times - for disclosing information about Tunisia's security services.

A police officer convicted of giving him information got 10 years in prison.

Critics accuse President Kais Saied of steering Tunisia towards dictatorship. The media rights group, Reporters Without Borders, said Mr Guesmi's sentence sent a "terrifying" message to the country's media.

Source: BBC
 
Back
Top Bottom