Tunduma: Soko la Manzese lateketea kwa moto

Inatakiwa wafanyabiashara wafunguke na wao wakachome ofisi za halmashauri ndio wanaotekeleza hilo.....pambafu zao
 
Soko la manzese lililopo tunduma mpakani mwa TANZANIA na Zambia limeteketea kwa moto.

---
Tunduma. Soko la Manzese lililoko katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma mkoani Songwe linawaka moto muda huu.

Moto huo ambao chanzo chake bado hakijajulikana umeanza leo Jumanne Novemba 16, 2021 asubuhi ambapo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na wananchi wanaendelea kuuzima.

Soko hilo lina maduka ambayo yanauza bidhaa mbalimbali zikiwamo nguo, vipodozi, vifaa vya magari na viatu

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu wakati akiwa njiani kwenda kwenye soko hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songw, Janeth Magomi amethibitisha tukio hilo akiahidi kutoa taarifa baada ya kufika kwenye soko hilo.

====

UPDATES

====

Zaidi ya Maduka 43 ya Wafanyabiashara katika Soko la Manzese mkoani Songwe yameteketea kwa moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika.

Mkuu wa mkoa wa Songwe, Bw.Omary Mgumbaathibitisha.

Kuna chama cha siasa kitatajwa kuhusika
 
Hilo soko limejengwa ndani ya eneo la mpaka wa kimataifa ambapo hairuhusiwi ujenzi wowote.
Pale unakuta nyumba imejengwa kwenye mpaka sebule ipo TANZANIA vyumba vya kulala vipo zambia.
 
Those arsonist they don't have blood running in their vains? The poor folks are just struggling to make the ends meet.
 
Back
Top Bottom