Tundu Lissu: Salamu za sikukuu ya Noeli na Mwaka Mpya kwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Weka siku chaguzi zimefanyika ndani ya cdm kwa mabavu, huenda hujui unaloongea zaidi ya kuwa bendera fuata upepo.
Hili nalo unataka kukataa. Uchaguzi wa ndani wa Chadema ulikua uchaguzi au yalikua maigizo yale. Wapinzani wa mbowe wote waliokua wanagombea kwenye kanda zao wamepigwa chini kwa hila na hujuma.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina tabia ya kukubali sababu dhaifu ili kuridhisha mtu. Huo utetezi kwamba wapinzani wa Mbowe walipigwa chini kimizengwe ni kisingizio cha kijinga. Tunachoangalia ni kuwa siku ya uchaguzi kulikuwa na uchaguzi huru na wa haki? Hayo yote yalifanyika kuanzia kwenye kanda mpaka, uchaguzi wa taifa.

Mimi sio mshabiki kabisa wa kiongozi yoyote yule kukaa madarakani zaidi ya miaka kumi. Na msimamo wangu huo uko wazi kuwa sikuafiki wala siafiki Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm kwa utetezi wowote ule. Lakini kuhusu kushinda, alishinda kihalali na uchaguzi huru na wa haki. Kama ningeona machafuko au wizi wa mabox ya kura siku ya uchaguzi kisha Mbowe atangazwe mshindi, hapo ningeona ni figisu. Kinyume na hapo naona ni sababu za kijinga za hao walioshindwa, sana sana naona wametumia sababu hizo ili kupata uhalali wa kurejea ccm, na kupewa nafasi za mbeleko.
 
Jambazi lililotaka kukuuwa limekata yooooo muda huu lishaoza kitambo Mungu ahimidiwe milele.
Kwa viongozi, wanachama na wafuasi wa Chama chetu na Watanzania wote kwa ujumla,

PEOPLE'S

Naomba nianze kwa kuwapa salamu za msimu huu wa Sikukuu ya Noeli na kuwatakia kila lenye kheri katika Mwaka Mpya unaokuja.

Pili, naomba kuwapongeza kwa kukamilisha Uchaguzi Mkuu wa Chama chetu katika ngazi zote za uongozi kuanzia Ngazi ya Msingi hadi Taifa.

Niwapongeze pia wale waliochaguliwa kuwa viongozi wa ngazi mbali mbali za Chama chetu. Aidha, niwashukuru kwa kunipa imani ya kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama.

Ili muelewe ukubwa na uzito wa kazi mliyoifanya katika Uchaguzi Mkuu huu, naomba niuweke uchaguzi huu katika muktadha (perspective) wake sahihi.

Huu ni mwaka wa 27 tangu kuanzishwa kwa Chama chetu. Katika kipindi chote hicho, CHADEMA haijawahi kuwa na uongozi wa kuchaguliwa na wanachama katika ngazi zote za uongozi wake kuanzia Msingi hadi Taifa.

Kwa kiasi kikubwa na katika maeneo mengi, viongozi wa Chama wa ngazi mbali mbali walikuwa wa kuteuliwa au kuteuana, hata kwa nafasi ambazo, kikatiba, zilikuwa ni nafasi za kuchaguliwa.

Ilibidi iwe hivyo kwa sababu, katika maeneo mengi, hatukuwa na wanachama wenye sifa za, au utayari wa, kuwa viongozi wa Chama. Kama mnavyofahamu, sehemu kubwa sana ya viongozi na watendaji wa Chama chetu wanafanya kazi zao kwa kujitolea, bila kutegemea malipo ya mshahara au posho yoyote.

Sasa, baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa viongozi wa ngazi mbali mbali za kitaifa wiki iliyopita, Chama chetu kimepata viongozi wa kuchaguliwa wa nafasi zote ambazo, kikatiba, ni za kuchaguliwa. Hii inahusu uongozi wa mabaraza ya Chama vile vile.

Sasa tunaweza kusema kwa usahihi kabisa kwamba tuna wanachama na viongozi wa kuchaguliwa katika kila kitongoji, kijiji au mtaa, Kata, Jimbo, Wilaya, Mkoa na katika kila Kanda ya nchi yetu.

Hii ni mara ya kwanza jambo hili limewezekana katika historia yetu ya miaka 27. Ndio maana nilisema, katika salamu zangu kwa Mkutano Mkuu wa Chama wiki iliyopita, hiki ni kipindi cha ", kipekee katika historia ya Chama chetu na katika historia yote ya kisiasa ya nchi yetu."

Kama nilivyosema katika salamu hizo, haijawahi kutokea katika historia yetu yote, kwa chama cha siasa, hasa cha upinzani, kuendesha Uchaguzi Mkuu wake huku uongozi wake wote wa juu ukikabiliwa na mashtaka makubwa ya kisiasa yanayoweza kupelekea wao kufungwa jela kwa muda mrefu.

Aidha, haijawahi kutokea kwa chama cha siasa, hasa cha upinzani katika nchi yetu, kufanya Uchaguzi Mkuu huku mmojawapo wa wagombea nafasi za juu za uongozi zinazogombaniwa akiwa nje ya nchi kwa zaidi ya miaka miwili kwa kuhofia maisha yake baada ya kunusurika katika jaribio baya la mauaji ya kisiasa dhidi yake.

Zaidi ya hayo Uchaguzi Mkuu huu umefanyika katika kipindi ambacho kimeshuhudia mambo ya kutisha yakifanyika dhidi ya viongozi, wanachama na wafuasi wa Chama chetu; na dhidi ya wananchi wa Tanzania kwa ujumla.

Katika kipindi hicho, viongozi na wanachama wetu wameuawa kinyama; na wengine wametekwa nyara na kupotezwa kabisa. Wengi wametekwa nyara, kuteswa vibaya na hata kutiwa vilema vya maisha.

Wengine wamekamatwa, kuteswa katika vituo vya polisi na baadae kushtakiwa kwa makosa ya uongo ya jinai. Wengi wamefungwa jela au wanaandaliwa kufungwa kwa kesi hizi za uongo.

Baadhi, kama Mwenyekiti wetu wa Taifa, wameharibiwa mali na biashara zao; wengine wamefukuzwa kazi na ajira zao ili kuwavunja nguvu za kiuchumi na, ilitegemewa na watesi wetu, za kisiasa.

Tumefanya Uchaguzi Mkuu huu katika kipindi ambacho shughuli halali za kisiasa, mikutano ya hadhara na maandamano, zimepigwa marafuku kwa vyama vya siasa vya upinzani, huku CCM ikiendesha shughuli hizo bila kizuizi chochote na kwa kutumia rasilmali za umma.

Uchaguzi Mkuu huu umefanyika katika kipindi ambacho, kwa mara ya kwanza katika historia yote ya Tanzania,

Watanzania wote wako chini ya uongozi ya Vijiji, Vitongoji na Mitaa ambao hauna uhalali wowote mbele ya macho ya wananchi na mbele ya dunia nzima, kwa sababu hakuna hata mmoja wao nchi nzima aliyechaguliwa na wananchi.

Mateso yote haya yamewafika Watanzania katika ujumla wao.

Wafanyabiashara, wakubwa kwa wadogo, wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka makubwa ya uongo ya uhujumu uchumi au utakatishaji fedha; na wengi kunyang'anywa fedha na mali zao bila uhalali wowote wa kisheria.

Sasa wanaambiwa hadharani kwamba wakitaka wafutiwe mashtaka haya ya kubambikizwa, ni sharti walipe mabilioni ya fedha.

Wakulima wa korosho wa mikoa yote ya Kusini wamedhulumiwa fedha zao baada ya kunyang'anywa korosho zao kwa kutumia nguvu za Jeshi la Wananchi, Usalama wa Taifa na Jeshi la Polisi.

Waandishi habari na wamiliki wa vyombo vya habari wamefungiwa, au kutishiwa kufungiwa, vyombo vyao vya habari; wengine wamekamatwa na kushtakiwa kwa makosa mbali mbali ya uhuru wa fikra, mawazo na mawasiliano.

Na baadhi, kama mwandishi wa habari Azory Gwanda wa gazeti la Mwananchi, wamepotezwa kabisa baada ya kukamatwa na vyombo vya usalama vya Serikali ya Rais Magufuli.

Wafanyakazi wa sekta binafsi na wa umma hawajaongezewa mishahara yao kwa miaka minne kinyume na sheria, huku gharama za maisha zikiongezeka siku hadi siku.

Wananchi wa kawaida wa kote nchini wameshuhudia hali zao za maisha zikianguka kwa sababu ya kuanguka kwa uchumi na ukosefu wa ajira kutokana na mazingira mabaya ya kibiashara yaliyoletwa na kile kinachoitwa sera za kutetea wanyonge za Serikali ya Rais Magufuli.

Wanafunzi wa ngazi zote za elimu kuanzia vyuo vikuu mpaka shule za msingi ambao wanahangaika kwa sababu ya mazingira magumu ya kupatia elimu.

Hata kabla ya Mkutano Mkuu wa Chama chetu kukamilika wiki iliyopita, viongozi kadhaa wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walifukuzwa kwa kosa la kudai wanafunzi walipwe mikopo waliyoahidiwa na Serikali hii hii ili kuwawezesha kuendelea na masomo yao!!!

Wanaharakati wa haki za binadamu wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nao 'wameisoma namba' ya utawala huu wa kidikteta. Ninavyoandika haya, wakili Tito Magoti wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ametekwa nyara na Jeshi la Polisi na anashikiliwa mahali kusikojulikana kwa karibu wiki nzima kinyume na kila sheria ya nchi yetu.

Viongozi, wanachama na wafuasi wa vyama vingine vya siasa, hata ndani ya CCM yenyewe, nao wametishwa au kuumizwa katika kipindi hiki cha miaka minne ya Tanzania ya Magufuli. Ndio kusema hata wale waliotutabiria 'ubatizo wa moto' nao wamebabuliwa na moto huo.

Kwa kifupi, ndugu wanachama, kila sekta ya jamii ya Tanzania imeumizwa. Kama nilivyowahi kusema siku za nyuma, hakuna ambaye amebaki salama. Yale maneno ya kwenye Kitabu cha Mithali, kwamba 'mwovu atawalapo watu huugua', sasa yametimia.

Haya ndio mazingira ya kipekee ya Uchaguzi Mkuu wa Chama chetu ambao tumeukamilisha wiki iliyopita. Kwa hiyo ninaposema huu ni Uchaguzi Mkuu wa kihistoria, hii ndio maana yangu.

Katika salamu zake kwa Mkutano Mkuu wa Chama chetu, Rais wa Chama cha UPDP, Fahmy Dovutwa, alitamka kwamba sasa CHADEMA ndio tegemeo pekee la vyama vya upinzani nchini kwetu.

Kauli hiyo ni ukweli mtupu. Kukamilika kwa Uchaguzi Mkuu wa Chama katika ngazi zote, sambamba na kusajili wanachama zaidi ya milioni 6.7 nchi nzima katika kipindi cha miezi 20; na kuweka zaidi ya 85% ya wagombea katika Uchaguzi wa Vijiji na Mitaa uliovurugwa na Serikali ya Rais Magufuli mwezi uliopita, ni uthibitisho tosha kwamba CHADEMA ndio tegemeo kuu la upinzani katika nchi yetu.

Licha ya jitihada kubwa na kutuumiza sana, Serikali ya Rais Magufuli imeshindwa kuiua CHADEMA. Badala yake, Chama chetu kimekuwa na nguvu kubwa kuliko kipindi kingine chochote katika historia yetu ya miaka 27.

Ni kweli, kama alivyotutabiria Mzee Yusuf Makamba wa CCM, kwamba tumepatiwa 'ubatizo wa moto.' Hata hivyo, ni kweli pia kwamba - kama ilivyokuwa kwa Shadrack, Meshack na Abednego wa kwenye biblia - hatujateketezwa na moto huo.

Kama Phoenix wa kwenye hadithi za Wayunani wa kale, tumetoka kwenye majivu ya moto wa Rais Magufuli tukiwa hai.
Ukweki ni kwamba tumetoka kwenye moto huo tukiwa imara zaidi.

Sasa tunatakiwa kujiweka tayari kutekeleza wajibu wetu wa kihistoria kama tegemeo kuu la upinzani na la wananchi wengine wengi katika nchi yetu.

Hatua ya kwanza katika kujiweka tayari huko ni kupanga safu za uongozi katika ngazi zote za chama. Hii tumeikamilisha wiki iliyopita.

Hatua ya pili inayotakiwa kuanza mara moja ni maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka kesho. Katika hatua hii napendekeza tuelekeze nguvu kubwa na msukumo katika maeneo makubwa matano.

Eneo la kwanza ni kupigania mageuzi makubwa ya Mfumo wa Uchaguzi nchini. Kuvurugwa kwa Uchaguzi wa Vijiji na Mitaa mwezi uliopita kumethibitisha, kama uthibitisho ulikuwa unahitajika, kwamba katika mazingira halisi ya sasa ya kikatiba, kisheria na kitaasisi, hakuna uwezekano wowote wa kuwa na uchaguzi huru na wa haki mwaka ujao.

Tume ya Uchaguzi, kama ilivyoundwa kwa mujibu wa Katiba yetu ya sasa, haiwezi na wala haina haiba na nia ya kuendesha uchaguzi huru na wa haki.

Watu wote 'wanaohusika na uchaguzi', kama walivyoainishwa kwenye Katiba, Sheria ya Uchaguzi wa Taifa na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, hawana uwezo wala haiba pamoja na nia ya kuendesha uchaguzi huru na wa haki.

Mfumo wa Tawala za Mikoa, yaani Wakuu wa Mikoa na Wilaya na watendaji wao, hawana uwezo, haiba wala nia ya kusimamia uchaguzi huru na wa haki.

Na vyombo vya dola, yaani Jeshi la Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa na Ujasusi havina uwezo wala haina na nia ya kusimamia uchaguzi huru na wa haki.

Kwa muundo wao wa kisheria na kitaasisi; kwa historia yao ya kiutendaji; kwa aina ya viongozi na watendaji walio nao, na kwa matendo yao halisi ndani ya hii miaka minne ya Tanzania ya Rais Magufuli, vyombo vyote hivi, ambavyo hutekeleza majukumu mbali mbali wakati wa uchaguzi, haviwezi kuendesha Uchaguzi Mkuu ujao bila ya upendeleo kwa CCM na wagombea wake wa ngazi zote.

Kwa hiyo, nguvu yetu kubwa tuielekeze katika eneo hili. Kauli mbiu yetu kuu iwe: Bila Mfumo Huru wa Uchaguzi Hakuna Uchaguzi Mkuu!!!

Tuieleze Serikali ya Rais Magufuli na watu wake kwamba bila mfumo huru na wa haki wa uchaguzi, hakuna Uchaguzi Mkuu mwakani.

Tuwaeleze wanachama, wafuasi na wananchi wetu wote wa Tanzania kwa ujumla kuwa bila mfumo huru na wa haki wa uchaguzi, hakuna Uchaguzi Mkuu mwakani.

Tuieleze jumuiya ya kimataifa, marafiki na wadau wetu wa maendeleo popote walipo duniani, kwamba bila mfumo huru na wa haki wa uchaguzi, hakuna Uchaguzi Mkuu mwakani.

Na tuamshe harakati na vuguvugu kubwa ya nchi nzima, itakayoshirikisha vyama vingine vya upinzani, taasisi za kijamii na za kidini, vyama vya wafanyakazi na vya kitaaluma na wananchi wa kawaida, ili kuhakikisha kwamba bila mfumo huru na wa haki wa uchaguzi, hakuna Uchaguzi Mkuu mwakani.

Sambamba na kupigania mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi, ni lazima tufanye maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ili tuwe tayari kushiriki uchaguzi pale mazingira huru na ya haki yatakapopatikana.

Tutafute wagombea imara na kuwaandaa kimafunzo na kwa vitendea kazi katika hatua zote za uchaguzi.

Tuepuke magomvi, migongano na makosa ya kujitakia tuyafanyayo kila mara wakati wa uchaguzi.

Yeyote mwenye uzoefu wa chaguzi zetu za nyuma anajua kwamba uchaguzi wowote unaoishirikisha CCM na vyama vya upinzani ni mapambano makali.

Kwa ushahidi wa miaka minne ya Tanzania ya Magufuli, nadiriki kusema kwamba Uchaguzi Mkuu wa mwaka ujao utakuwa wa mapambano makubwa, makali na magumu kuliko yoyote katika historia yetu ya mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Magufuli alishatoa taarifa rasmi ya azma yake ya kufuta vyama vya upinzani nchini ifikapo mwaka ujao. Wote tumeshuhudia utekelezaji wa azma yake hiyo. Waingereza wanasema 'forewarned is forearmed.' Tumetahadharishwa mapema; tunatakiwa kujiandaa mapema.

Eneo la tatu tunalowajibika kulifanyia kazi ni kujenga UKAWA Mpya, imara na bora zaidi kuliko tulivyofanya kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita.

Sisi ndio Chama Kikuu cha Upinzani katika nchi yetu; na, kwa mwelekeo wa miaka kadhaa sasa, tutaendelea kuwa 'tegemeo kuu' la upinzani Tanzania.

Lakini ni lazima tutambue kwamba kuwa chama kikuu cha upinzani sio kuwa chama pekee cha upinzani. Hatuna budi kuelewa kwamba wanachama wetu milioni 6.7 ni sehemu tu ya Watanzania zaidi ya milioni 55; na wapiga kura zaidi ya milioni 20.

Pamoja na nguvu yetu kubwa, peke yetu hatutaweza kuishinda CCM, hasa katika mazingira halisi ya mfumo wetu wa uchaguzi kama ulivyo sasa.

Ni lazima tujenge mahusiano na mashirikiano na vyama vingine vya siasa vya upinzani, taasisi za kijamii na za kidini, vyama vya wafanyakazi na vya kitaaluma, n.k.

Uwezo wetu kujenga mahusiano na mashirikiano hayo utakuwa ni ushahidi muhimu wa kuaminiwa kwetu na makundi mbali mbali ya kijamii nchini na
ndiyo 'guarantee' yetu ya ushindi mwakani.

Katika mahusiano na mashirikiano yoyote ya aina hii, kuna 'give and take.' Kama Chama Kikuu cha Upinzani katika nchi yetu, ni lazima tutakuwa na sehemu kubwa ya 'take.' Kwa mantiki hiyo hiyo, tutakuwa na wajibu mkubwa wa 'give' vile vile.

Kwa sababu hiyo, tusijiangalie sisi na maslahi yetu kama Chama pekee. Tuwaangalie wenzetu na maslahi yao vile vile. Tuwaangalie na wale wote ambao, kwa sababu mbali mbali, sio wanachama wa Chama chetu au wa vyama vingine vya siasa.

Juu ya yote, tuangalie 'the real prize', lengo kuu zaidi: kuiondoa CCM na mfumo wa chama-dola ambao umekuwa madarakani kwa zaidi ya miongo mitano na ambao umeidumaza nchi yetu katika kila sekta ya kiuchumi, kisiasa na kijamii katika kipindi chote cha uhuru wetu.

Kwa bahati au kwa makusudi, sasa kuna mazingira wezeshi ya kisheria ya kutuwezesha kujenga mahusiano na mashirikiano na vyama vingine vya siasa vya upinzani kwa malengo ya kiuchaguzi.

Marekebisho ya mwaka huu ya Sheria ya Vyama vya Siasa yameweka utaratibu unaowezesha vyama vya siasa kuunda 'electoral coalitions' bila kuhitaji kujiua kwanza. Hili halikuwa linawezekana kabla ya marekebisho hayo.

Kwa maoni yangu binafsi, masharti ya kuwa na mashirikiano hayo ya kiuchaguzi yanakubalika, hata kama sipendezwi sana na namna yalivyowekwa kitaalamu.

Tuyaangalie masharti haya kwa umakini wote na tahadhari inayohitajika na tuyafanyie kazi ili tujenge UKAWA imara na bora zaidi. Kwa busara zetu na za viongozi wetu wa vyama vya upinzani, jambo hili linawezekana.

Jambo la nne linahusu mahusiano ya kimataifa. Katika dunia halisi ya leo, hasa katika nchi za Kiafrika, ni vigumu kwa chama cha siasa cha upinzani kushinda Uchaguzi Mkuu na kuchukua madaraka, bila kujenga mahusiano bora na jumuiya ya kimataifa.

Hatuko peke yetu katika dunia hii ya Mwenyezi Mungu. Tuna majirani wenye maslahi na nchi yetu katika pande zote za nchi yetu; kama ambavyo na nchi yetu ina maslahi na majirani zetu wanaotuzunguka.

Nje ya majirani zetu wa kijiografia, tuna majirani wa kiuchumi, kisiasa na kijamii ambao tumekuwa nao kwa muda mrefu. Hawa pia wana maslahi na nchi yetu na sisi pia tuna maslahi na nchi zao.

Kwa sababu hizi zote, kama Chama Kikuu cha Upinzani katika nchi yetu, tuna wajibu wa kujenga mahusiano na mashirikiano na jumuiya ya kimataifa. Tunahitaji marafiki nje ya nchi yetu.

Na hii sio kusaliti nchi yetu, au kuvunja sheria zake, kwani hakuna sheria yoyote ya Tanzania inayokataza vyama vya siasa kujenga mahusiano na nchi na taasisi za nje.

Kufanya hivyo ni kutambua hali halisi ya dunia ya leo. Hakuna nchi iliyo kisiwa; wote ni sehemu ya hiki kijiji cha ulimwengu.

Kwa bahati nzuri, mazingira ya sasa kidiplomasia ni mazuri sana kwa sisi, kama Chama Kikuu cha Upinzani, kujenga mahusiano bora na jumuiya ya kimataifa.

Kwa sababu ya matendo yake, Serikali ya Rais Magufuli imechafuka kila mahali katika ulingo wa kidiplomasia ya kimataifa. Sasa nchi yetu inaangaliwa kwa jicho kali katika medani ya kikanda na kimataifa.

Rais Magufuli ameharibu na anaendelea kuharibu mahusiano yetu na nchi za nje na taasisi za kikanda na za kimataifa. Kwa sababu ya matendo maovu ya Serikali yake, nchi yetu inatengwa au inajitenga na jumuiya ya kimataifa.

Hii ni fursa kubwa kwetu ya kujijenga kidiplomasia. Huu ni wakati muafaka wa kuionyesha dunia kwamba, sisi ni mbadala bora wa CCM na Rais Magufuli katika ulingo wa kimataifa.

Katika kufanikisha jambo hili, tunahitaji kuwekeza nguvu kubwa katika masuala ya kidiplomasia. Tunahitaji kushiriki katika mijadala muhimu inayoendelea duniani. Tunahitaji kusikika katika mabaraza ya kimataifa.

Yote haya yanahitaji watu wenye uwezo wa kuzungumza na wadau mbali mbali wa kimataifa na kueleweka. Tuwatafute watu hao na kuwawezesha kutekeleza jukumu hili muhimu.

Jambo la tano na la mwisho kwa leo linahusu rasilmali za kutekeleza majukumu yote yanayotakiwa kutekelezwa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka ujao.

Uchaguzi wowote ule ni gharama kubwa. Uchaguzi Mkuu wa madiwani, Wabunge na Rais ni gharama kubwa zaidi. Ili tuweze kushinda uchaguzi huo, ni lazima tuwe na rasilmali zinazohitajika.

Sheria yetu ya Gharama za Uchaguzi haikatazi mtu yeyote yule kuchangia gharama za uchaguzi wowote ule. Hivyo basi, tunatakiwa tuchangishane ili kugharamia maandalizi na kampeni za UchaguziMkuu ujao.

Tuwatafute wale wote wenye uwezo wa kuchangia zaidi na kuwaomba wachangie zaidi. Lakini tuhakikishe kila mmoja wetu anachangia kwa kiasi chake kulingana na nafasi yake.

Naomba kumalizia kwa kukopa maneno ya Nelson Mandela katika hotuba yake kwa Mkutano Mkuu wa Chama cha ANC wa Jimbo la Transvaal ya tarehe 21 Septemba 1953: "hakuna njia rahisi ya kuelekea kwenye uhuru, na wengi wetu tutapitia tena na tena katika bonde la uvuli wa mauti kabla ya kufikia kilele cha matazamio yetu."

Chama chetu na viongozi, wanachama na wafuasi wake kimepitia katika bonde la uvuli wa mauti mara kadhaa. Sasa kiko tayari kufikia kwenye kilele cha matazamio ya Watanzania. Basi na tujiandae kikamilifu ili tuweze kukwea kilele hicho.

Nawashukuru sana; Mungu awabariki, na nawatakieni Krismasi ya Furaha na Mwaka Mpya wenye baraka zote.

Tundu AM Lissu, MB
Eindhoven, Uholanzi
Desemba 24, 2019
 
Mbowe na mn
Chuki yako binafsi kwa Raisi kipenzi cha watanzania Dr John Pombe Magufuli, zitakufanya ushindwe kuongoza CHADEMA kama unavyotegemewa. Mbona bosi wako Mbowe hana chuki hiyo? Mbona katibu mkuu wako mpya hana hiyo chuki binafsi?
Baada ya kutoa salaam zinazotuonyesha matumaini mbeleni tuendako, wewe unatiririsha chuki, itakusaidia nini Bw. Lissu? Jenga chama bila ya kuleta chuki yako binafsi. CHADEMA imara itaimarisha CCM mara mia - shime uache chuki. Nakutakia uongozi bora na pia moyo usio na chuki kwa Raisi wetu.
Mbowe na mnyika hawakupigwa risasi 16 wala hawakupoteza ubunge kiuonevu.
 
Huyu Mwamba huyu Mungu amuweke miaka 800
 
Chuki yako binafsi kwa Raisi kipenzi cha watanzania Dr John Pombe Magufuli, zitakufanya ushindwe kuongoza CHADEMA kama unavyotegemewa. Mbona bosi wako Mbowe hana chuki hiyo? Mbona katibu mkuu wako mpya hana hiyo chuki binafsi?
Baada ya kutoa salaam zinazotuonyesha matumaini mbeleni tuendako, wewe unatiririsha chuki, itakusaidia nini Bw. Lissu? Jenga chama bila ya kuleta chuki yako binafsi. CHADEMA imara itaimarisha CCM mara mia - shime uache chuki. Nakutakia uongozi bora na pia moyo usio na chuki kwa Raisi wetu.
Vipi yuko wapi Yule Dubwasha lenu??😅😅😅
 
Sisi ndio Chama Kikuu cha Upinzani katika nchi yetu; na, kwa mwelekeo wa miaka kadhaa sasa, tutaendelea kuwa 'tegemeo kuu' la upinzani Tanzania.

Lakini ni lazima tutambue kwamba kuwa chama kikuu cha upinzani sio kuwa chama pekee cha upinzani. Hatuna budi kuelewa kwamba wanachama wetu milioni 6.7 ni sehemu tu ya Watanzania zaidi ya milioni 55; na wapiga kura zaidi ya milioni 20.
kimataifa.

Nawashukuru sana; Mungu awabariki, na nawatakieni Krismasi ya Furaha na Mwaka Mpya wenye baraka zote.

Tundu AM Lissu, MB
Eindhoven, Uholanzi
Desemba 24, 2019
Merry Christmas.
Nimekuwa nikijiuliza Chadema ni wanaharakati wazuri, wanafeli wapi?.

Kumbe zile kura milioni 6.7 Edward Lowassa alizovuna kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, Chadema ilizihesabu kama ndio idadi ya wanachama wake!.

Kiukweli hiyo sio idadi ya wanachama wa Chadema bali ni idadi ya Watanzania waliompa kura Lowassa, miongoni mwao Chadema wapo, CCM wapo, vyama vingine wako, na hata wasio na vyama pia wapo.

Ili Chadema ipate mafanikio ya ukweli, ni lazima ifanye siasa za ukweli.

I wish you a Merry Christmas.
P
 
CCM anafanya siasa za ukweli? Za kupiga watu risasi? Kupoteza? Kuafungia mikutano ya kutangaza chama Chao etc etc
 
Merry Christmas.
Nimekuwa nikijiuliza Chadema ni wanaharakati wazuri, wanafeli wapi?.

Kumbe zile kura milioni 6.7 Edward Lowassa alizovuna kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, Chadema ilizihesabu kama ndio idadi ya wanachama wake!.

Kiukweli hiyo sio idadi ya wanachama wa Chadema bali ni idadi ya Watanzania waliompa kura Lowassa, miongoni mwao Chadema wapo, CCM wapo, vyama vingine wako, na hata wasio na vyama pia wapo.

Ili Chadema ipate mafanikio ya ukweli, ni lazima ifanye siasa za ukweli.

I wish you a Merry Christmas.
P
Walifanya siasa za kweli na za kistaarabu mkawapa kesi viongozi wap nchi nzima na mkawapiga risasi baadhi yao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom