Tundu Lissu ni ‘mwanakulitafuta, mwanakulipata’. NEC tendeni haki, kama kavuruga mkateni kwa mjibu wa sheria, kanuni na utaratibu bila huruma

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,398
3,907
Tundu lisu ni mwanasheria mzuri sana anajua lipi ni kosa kisheria na lipi si kosa kisheria

Kama anajua kuwa kufanya maandamano ya shangwe na bashasha wakati wa musiba wa Mzee Mkapa si kosa kisheria basi atagombea Urais wa JMT

Kama anajua kuwa kuidanganya mahakama kuwa hawezi kuhudhuria mahakamani kwa sababu amejiweka karantini na wakati huo hakimu na jaji wa kesi yake anamuona anadunda kwenye mikutano ya hadhari changanyikeni basi asiwe na hofu atagombea urais wa JMT

kama anajua kumtukana kumuondolea heshima amiri jeshi mkuu wa ulinzi na usalama ni sawa basi atagombea urais wa JMT

kama kanuni zinaruhusu kuzunguka mikoani kuhutubia ni halali kisheria na kikanuni asiwe na hofu atagombea urais wa JMT

Kama ni sawa kutotanguliza masilahi ya Taifa mbele kwa kuudanganya umma kwamba serikali haijafanya lolote basi ni sawa atagombea urais wa JMT

kama ni sawa kutojaza fomu zenye tamko za Mali na madeni zako si jinai atagombea urais wa JMT

Tume msiomuonee Tundu Lisu kwa kumkata kama hajatenda kosa na msimuoneee huruma pia kama amekiuka utaratibu kwa mjibu wa sheria na kanuni zenu mkateni bila huruma ila msimuonee
 
Mataga woga wa nini?Lissu anawatia hofu sana mpaka mnaona hamumuwezi kwenye sanduku la kura!
 
Sijakuelewa ulichoandika, naomba aliyeelewa mwandishi anamaana gani aliambie.
Viongozi wa ccm kuanzia ngazi za shina hadi ngazi za juu walifanya kampeni kuazia pale tu uchaguzi wa 2015 ulipomalizika wakati vyama vingine wakikatazwa kufanya hata mikutano ya ndani ya vyama.
HILO wewe ulioni, unaona tu lissu anavunja sheria, je hivi sheria za nchi zinaupendeleo kwa vyama fulani na kugandamiza vyama vingine?
 
Hivi nyinyi maccm, hamuoni aibu kutaka kuwa wagombea bila kupata upinzani wowote, kama mlivyofanya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa?

Hivi kama nyinyi CCM mnajinadi siku zote kuwa mmejenga ma-fly overs, mmejenga barabara nyingi za lami, hivi mnaogopa nini kupambana na mgombea ambaye mmekuwa mkidai kuwa chama chake kimekufa?

Hivi kama nyinyi maccm, ndiyo mnahodhi vyombo vyote vya dola, likiwemo Jeshi la Polisi, hivi mnawezaje kumgwaya mtu ambaye hana mabunduki yanayomlinda?

Hakika nyinyi CCM mwaka huu, Tundu Lissu amewashika sehemu zenu za nyeti, na hamna pa kutokea!
 
Tundu lisu ni mwanasheria mzuri sana anajua lipi ni kosa kisheria na lipi si kosa kisheria

Kama anajua kuwa kufanya maandamano ya shangwe na bashasha wakati wa musiba wa Mzee Mkapa si kosa kisheria basi atagombea Urais wa JMT

Kama anajua kuwa kuidanganya mahakama kuwa hawezi kuhudhuria mahakamani kwa sababu amejiweka karantini na wakati huo hakimu na jaji wa kesi yake anamuona anadunda kwenye mikutano ya hadhari changanyikeni basi asiwe na hofu atagombea urais wa JMT

kama anajua kumtukana kumuondolea heshima amiri jeshi mkuu wa ulinzi na usalama ni sawa basi atagombea urais wa JMT

kama kanuni zinaruhusu kuzunguka mikoani kuhutubia ni halali kisheria na kikanuni asiwe na hofu atagombea urais wa JMT

Kama ni sawa kutotanguliza masilahi ya Taifa mbele kwa kuudanganya umma kwamba serikali haijafanya lolote basi ni sawa atagombea urais wa JMT

kama ni sawa kutojaza fomu zenye tamko za Mali na madeni zako si jinai atagombea urais wa JMT

Tume msiomuonee Tundu Lisu kwa kumkata kama hajatenda kosa na msimuoneee huruma pia kama amekiuka utaratibu kwa mjibu wa sheria na kanuni zenu mkateni bila huruma ila msimuonee
MAPINGAMIZI HALALI KISHERIA DHIDI YA MGOMBEA NAFASI YA URAIS.

Wiki ijayo tarehe 26 August, 2020 itakuwa ni siku ya wagombea kuwasilisha mapingamizi dhidi ya wagombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mapingamizi halali kisheria anayoweza kuwekewa mgombea wa nafasi ya Urais kwa mujibu wa masharti ya ya Kifungu cha 35 D na 40 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 yakisomeka kwa pamoja na (read in tendem with) masharti ya Kanuni ya 39 (4) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge, 2020 (Tangazo la Serikali Na. 402 la 2020) ni haya yafuatayo;

(1) Mgombea Urais sio raia wa Tanzania.

(2) Mgombea Urais hajafikisha umri wa miaka 40.

(3) Mgombea Urais hajui kusoma na kuandika Kiswahili au Kiingereza.

(4) Mgombea Urais sio mwanachama wa chama cha siasa.

(5) Mgombea Urais hajadhaminiwa na chama cha siasa kugombea.

(6) Mgombea Urais amekutwa na hatia ya kosa la jinai la kukwepa kodi katika kipindi cha miaka 5 kabla ya siku ya Uchaguzi.

(7) Mgombea Urais hajadhaminiwa na wapiga kura 200 kutoka mikoa 10 ya Tanzania ikiwemo mikoa 2 kutoka Zanzibar.

(8) Mgombea Urais hajadhaminiwa na idadi ya kutosha ya wapiga kura.

(9) Mgombea Urais hakulipa dhamana ya Tshs 1, 000, 000/=

(10) Mgombea Urais hakuwasilisha au hakuambatinisha picha kwenye Fomu ya Uteuzi.

(11) Mgombea Urais ameshindwa kuambatanisha Tangazo la Kisheria (statutory declaration) kwenye Fomu ya uteuzi ambalo limesainiwa na mgombea na limefanywa mbele ya Jaji kudhibitisha kuwa mgombea anayo nia na anazo sifa za kugombea Urais.

(12) Mgombea Urais ameshindwa kuweka wazi pesa ambazo atazitumia katika uchaguzi.

(13) Mgombea Urais hakusaini kukubali kutii Maadili ya Uchaguzi.

(14) Mgombea Urais hakujaza au hakurudisha Fomu ya Uteuzi kwa Tume ya Taifa Uchaguzi kwa mujibu wa matakwa ya sheria.

(15) Mgombea Urais amefanya makosa ambayo yamezuhiwa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi, 2010.

(16) Kutokana na taarifa ambazo ziko kwenye Fomu yake ya Uteuzi, mgombea hana sifa za kuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge au mjumbe wa baraza la wawakilishi la Zanzibar zilizoainishwa na Katiba husika.

(17) Taarifa ambazo mgombea Urais amewasilisha kwa Tume ya Taifa uchaguzi hazijitoshelezi kumtambua mgombea.

(18) Kutokana na taarifa ambazo ziko kwenye Fomu yake ya Uteuzi, hana sifa za kuwa mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizoainishwa na Katiba.

Haya ndo mapingamizi 18 pekee ambayo anaweza kuwekewa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sio vinginevyo.
 
Mkuu mbona tayari jina la lissu lishachinjiliwa mbali(tetesi).

Ningeshangaa Sana Kama NEC wangempitisha huyu mtu wa hovyo kabisa kuwahi kutokea kwenye Taifa letu.
Magufuli amefanya mengi makubwa, yeye ana Tume yake ya Uchaguzi aliyoiweka mfukoni wana hofu ya nini?
 
Tundu lisu ni mwanasheria mzuri sana anajua lipi ni kosa kisheria na lipi si kosa kisheria

Kama anajua kuwa kufanya maandamano ya shangwe na bashasha wakati wa musiba wa Mzee Mkapa si kosa kisheria basi atagombea Urais wa JMT

Kama anajua kuwa kuidanganya mahakama kuwa hawezi kuhudhuria mahakamani kwa sababu amejiweka karantini na wakati huo hakimu na jaji wa kesi yake anamuona anadunda kwenye mikutano ya hadhari changanyikeni basi asiwe na hofu atagombea urais wa JMT

kama anajua kumtukana kumuondolea heshima amiri jeshi mkuu wa ulinzi na usalama ni sawa basi atagombea urais wa JMT

kama kanuni zinaruhusu kuzunguka mikoani kuhutubia ni halali kisheria na kikanuni asiwe na hofu atagombea urais wa JMT

Kama ni sawa kutotanguliza masilahi ya Taifa mbele kwa kuudanganya umma kwamba serikali haijafanya lolote basi ni sawa atagombea urais wa JMT

kama ni sawa kutojaza fomu zenye tamko za Mali na madeni zako si jinai atagombea urais wa JMT

Tume msiomuonee Tundu Lisu kwa kumkata kama hajatenda kosa na msimuoneee huruma pia kama amekiuka utaratibu kwa mjibu wa sheria na kanuni zenu mkateni bila huruma ila msimuonee
Ni maombi yangu mzidi kupoteana
 
Pole yako mkuu, naona mnataka kubadilisha kanuni ili mabeki wasaidie kukaba mpaka penati.
 
Back
Top Bottom