Tundu Lissu: Naipenda Yanga, ila siipendi rangi yao inanikumbusha mabaya

Basi asile mboga za majani, asile fenesi, asile ndizi mbichi/mbivu,asile pilau ya njano,ashindie uji wa ubuyu na ugalii kama alipokuwa mdogo huko isuna.
Nimecheka sana. Ale misosi ya bluu. Na amshauri yule dada Mheshimiwa anayehisiwa kuvuta majani na kuleta timbwili mjengoni aache maana ile kitu ni ya kijani. Yanga mbele kwa mbele
 
Flag_of_TANU.svg.png
1200px-Flag_of_Afro-Shirazi_party.svg.png
Yanga teh.teh
 
Huyu babu uzee unamjia vibaya, unawezaje kuepuka ukijanikijani humu duniani? mboga za majani ni kijani anazila zinakaa tumboni mwake na anazurura nazo mjini, utakuta hata nyumbani kwake kuna maua ambayo ni ya kijani na anaishi nayo, nguvu anayotumia kusema haipendi kijani source yake ni rangi ya kijani kutokana na chlorophill cells kuwezesha mimea kutengeneza chakula kwa photosynthesis na baadae huyu jamaa anapata chakula na kupata nguvu za kwenda kupayuka bungeni.Aache kukariri mambo,kama vipi akusanye mboga za majani azipeleke pale makao makuu ya chama chake zikawekwe rangi ya kaki kama gwanda zao.POINT YANGU NI KWAMBA TUACHE MPIRA UWE MPIRA NA SIASA IWE SIASA. wapo wafia Simba kama kina Haji Manara lakini wakienda chamani kule CCM wanapiga kijani kama kawaida kwa kuwa kila jambo na mahali pake.
 
Jamaa anasema hata kombe la Yanga lilipoenda bungeni hakulikaribia sababu ya rangi ...hahaaa nadhani ilikuwa utani though


Kama ni ugonjwa tunao wengi hiyo rangi siipendagi kisa hilo chama sorry hayo ni maoni na maono yangu hata kama yatakuwa ni ya kijinga kwa kiwango cha mwisho
 
..nilichogundua ktk video hii ni kwamba kwa hapa Tz, TL ndiye mwanasiasa ambaye huwezi kuchoka kumsikiliza.

..kila alipo TL waandishi wa habari wanakanyagana ili mradi kila mmoja apate nafasi ya kuuliza swali.


..waandishi wanajisikia HURU kuongea na TL. Waandishi wako free kumuuliza TL jambo lolote na ndiyo maana umeona wamemuuliza masuala ya mpira ( Yanga vs Simba).
 
Lissu aache Ushamba wa kuleta Siasa zake kila sehemu!

Ina maana huwa hakaribii Mboga za Majani kwa kuwa ni za Kijani?
 
Back
Top Bottom