Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,942
- 19,130
Jamaa anasema hata kombe la Yanga lilipoenda bungeni hakulikaribia sababu ya rangi ...hahaaa nadhani ilikuwa utani though
Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu amesema kuwa hajawahi kwenda uwanjani kuangali mpira tangu mwaka 1993 kwani mara ya mwisho alinusurika kuvuliwa suruali yake ya mashabiki wa Simba.
Tundu Lissu ambaye ni Mwanasheria wa CHADEMA aliyasema hayo alipoulizwa na mwandishi mmoja wa habari kama huwa anakwenda uwanjani kuangalia mpira, ambapo alisema mara yake hiyo ya mwisho alikwenda kuangalia mchezo ilikuwa kati ya Sumba na Stella Club d’Adjamé ya Ivory Coast ambapo alinusurika kuvuliwa suruali, hivyo tangu siku hiyo hajawwahi kwenda tena.
“Sijaenda tangu mwaka 1993. Nilikaribia kuvuliwa suruali na mashabiki wa Simba, baada ya Simba kushindwa na Stella d’Adjamé uwanja wa taifa hapa, sijarudi tena.” alisema Lissu.
Awali Tundu Lissu alisema kuwa yeye ni shabiki wa Yanga tangu utotoni lakini huwa hataki hata kuwakaribia kwa sababu sare zao zinamkumbusha Chama cha Mapinduzi (CCM).
“Mimi ni shabiki wa Yanga lakini sipendi mavazi yao kabisa,.. yananikumbusha CCM. Mi’ ni shabiki wa Yanga tangu utotoni, lakini hicho kivazi chao,.. juzi niliwaambia, mimi nawaunga mkono lakini siwakaribii.”