Tofauti wao wamestaharabika sisi bado sana, labda miaka 1,000 ijayo.
Huku kwetu domo kaya ukiwapa media wataongea uongo asilimia 95 na ukweli 5.
Huku kwetu raia wanaupokea uongo kwa 95% na ukweli kwa 5% tena kwa haraka na kuufanyia kazi chap chap na ndio maana zaidi ya zaidi ya 80% ya Watz wagonjwa wanaenda kwa wachawi badala ya hospitali.
Huku kwetu ukiwaruhusu wanasiasa waongee watasodoa kila jema lililofanyika na linalofanyika.
Huku kwetu ukiwapata pulpit mwanasiasa atawagawa watu kwa misingi ya dini, ukabila na jiografia.
Huku kwetu ukiwapa jukwaa wanasiasa watawaambia watu wasilipe kodi.
Huku kwetu ukiwapa wanasiasa jukwaa watawahamasisha watu wasifanye maendeleo ila wabaki kwenye vigenge kupiga soga za kisiasa za upinzani.
Huku kwetu Tanzania ukiwapa wanasiasa nafasi ya kuongea watawahamasisha watu waache kufanya kazi na waandamane kudai kisichojulikana na hatimaye biashara na mali za raia innocent kuharibiwa na kuibiwa.
Huku kwetu ukiwapa fursa ya kuongea wanasiasa watawahamasisha watu kuchukiana kwa misingi mbalimbali na mwisho wake kupigana
Kikwete aliwapa huo uhuru mliutumiaje?, maandamano kila kona, migomo kila kona, hata kazi watu wengi waligomea, uchumi ulidorora
Mnadai msichokijua, mkipewa uhuru huo mambo yakienda vibaya mnasema Serikali Legelege
Mama Samia Suluhu kaza kamba, hatuhitaji siasa sasa hadi 2025, Watz tuachwe tufanye kazi