Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,503
- 51,098
Mgombea Urais kupitia Chama cha Chadema ndugu Tundu Lissu, amewaasa Wananchi wa Bagamoyo kuwa, Magufuli ana lengo la kubadili ukomo wa vipindi vya utawala na ndiyo maana hilo Suala lilizungumzwa bungeni na Spika Ndugai.
Lissu akawaambia wananchi kuwa, Ndugai asingeweza yeye binafsi kulizungumza hilo bila kufahamu kinachoendelea kwenye mipango ya Magufuli.
Lissu akawaambia wananchi kuwa, wafikirie hali ngumu za maisha, ukatili na uonevu uliotokea katika kipindi hiki cha miaka mitano halafu eti Magufuli aongezewe miaka mingine.
Lissu amesema, serikali ya Chadema itakuwa ni Serikali ya Haki, Uhuru na Maendeleo. Itakuwa serikali itakayoheshimu watu tofauti na hii ya Magufuli yenye kudhalilisha watu hususan wanawake.
Lissu akasema kujenga miundo mbinu siyo hoja ya kunyima haki za watu kama vile nyongeza za mishahara zilizoko kisheria. Akasema kuwa hata mkooni alijenga reli, lakini hiyo haikuwa sababu ya kwa nini Tusimpinge, Akasema kuwa tulimpinga mkoloni kwa sababu hakuwa anatutendea haki.
Lissu akasema kuwa Nyerere alijenga reli ya TAZARA, tena ndefu zaidi lakini hakudhulumu stahiki za wafanyakazi
Kwa taarifa zaidi juu ya hoja nzito za Lissu tazama video hii