Chadema kisimtumie TL vibaya.
Wamshauri vizuri atulie kama alivyoshauriwa na Nape Nnauye.
Nape bila shaka anazijua vizuri siasa za nchi maskini hasa za Afrika.
Akumbuke wale waliojaribu kumuu bado wapo mitaani na hawajakamatwa. Hatujui kwa hakika walitumwa na nani mpaka sasa.
Hatujui kuwa wale waliomtuma wameshamaliza mission yao au bado!
Na je, Kwa nini matibabu yafanyike Ubeligiji?
Hii nchi sijaona kuwa ni nchi salama kwa mataifa ya Afrika na Demokrasia duniani?
Jambo la kusikitisha ni kwamba Wapinzani wenye afya zao wameufyata na sasa wanamtanguliza mbele mgonjwa.
Na cha ajabu zaidi wanamkatisha tamaa kwa kushindwa kuwa na mbinu za kujenga chama badala yake wanachama na viongozi wa chama wanapukutika kwa kukumbilia kule kule wanakotuhumu kuwa ndipo watesi wa Lisu walipo.
Mbowe ataondoka Chadema na kukiacha kikiwa taabani kifedha ,kisera, kiitikadi,kimwelekeo, kimiundo mbinu, kichama (wanachama) n.k.
Kifupi Mbowe hata kama ataamua kuacha demokrasia imuondoe madarakani au kustaafu uenyekiti lakini atakua ameweka miundo mbinu rahisi kwa CCM kukiua hicho chama kirahisi kwa kuwa ni chama kisicho na mizizi. Ni chama cha matukio tu ndio maana kinang"ang"ana na kampeni za majukwaani zisizoisha ili wapate nafasi za kutuhumu watu na kuwachafua majukwaani bila kuzungumzia nafasi za kujenga chama kimiundo Mbinu.
Mbowe alikua na nafasi kubwa kujenga miundo mbinu ya chama baada ya uchaguzi.
Mh. Rais kabla na baada ya kuingia madarakani aliipenda sana Chadema kwa kuwa ndiyo iliyokua inapambana na ufisadi na ndio maana aliwashauri kuwa wajenge ofisi zao za chama makao makuu Dodoma.
Ushauri ule ulikua ni mzuri sana wa kiungwana.
Wangemwelewa mpaka sasa wangekua na mchakato wa kujenga ofisi nchi nzima badala yake wanatumia pesa nyingi kukodisha majengo.
Ninachoona ni kuwa Mbowe naye yuko mbioni kurudi kule wanaporudi wenzake.
Na kwa hali ilivyo Chadema isipokuwa makini baada ya uchaguzi wa ndani ya chama kitaanguka kama NCCR mageuzi.
Huu hasa ndio woga wa Mbowe kuwa chama kinaweza kusambaratika endapo ataondoka madarakani. Anajua wazi kuwa ameshindwa kujenga chama kitaasisi na kuweka mizizi kuanzia vijijini.
Ni chama kilichoko kwenye briefcase yake mana hakina miundo mbinu maalum.
Kuna watu waliipenda NCCR mageuzi kwa sababu tu mwenyekiti alikua ni Mrema. Hasa watu wa kaskazini kwa maana ya wale wa eneo analotoka Mrema.
Hali hiyo inaonekana ipo pia Chadema. Mbowe amekua na matumaini makubwa kuwa anakubalika sana lakini ukweli ni kuwa alikubalika sana lakini kwa sasa anakubalika kidogo sana tena kwa upanda na eneo analotoka, ambalo nao pia wameanza kumkimbia kwa kasi baada ya kugundua kuwa wanaongozwa na mtu anayejali maslahi yake zaidi kuliko chama kama taasisi.
Maeneo mengine wanakipenda Chama lakini eneo lake wanampenda mwenyekiti na bila shaka watu wa nyumbani kwake watakua wote wamerudi CCM mara tu mwenyekiti huyo atakapoamua kuachia madaraka na kurudi kule madiwani wake wanakorudi kila kukicha ili 2020 awe na uhakika wa kutangazwa mshindi wa jimbo la Hai.
Kwa hiyo wanachama wa chadema wawe makini na waanze kujipanga namna ya kunusuru chama chao wakati wa kumchagua mwenyekiti mwingine. Na ikiwezekana mwenyekiti awe ni Mtu anayefahamika na kukubalika kanda zote.
Chama kijengwe kitaifa na kimfumo sio kimatukio na umaarufu wa mtu mmoja mmoja.