Tundu Lissu kuwekwa kizuizini?

Tundu Lissu kuwekwa kizuizini?

Maneno mengiiiii Hanna kitu, utawala umetumia hekima na busara ya kumsubili mgonjwa wetu alone kwanza! Hapo ndipo atatimilika kiakili na si kama mtoa mada, kwa hisia tu anamhukumu mtu
Hanna? Kumsubili? alone? Atatimilika? Kwa mwandiko huu bado tuna safari ndefu sana kwenye mijadala
 
Swali langu kwako mwenyekujua/kuona live tukio ni dereva na Tundu,tundu akili zake bado aziko sawa mpka sasa ila dereva wake hakudhurika kwa maana hiyo yamapasa kuhojiwa ajitokeze na si kujificha
 
Mwanzo mlijua hatoinuka kutoka nje ya nyumba yake aliposhambuliwa akiwa hai,lakini alipotoka akiwa hai mkajipa matumaini kuwa hatotoka Dodoma general hospital akiwa hai.
Mungu mkubwa Lissu akasafirishwa Nairobi mkajipa siku kadhaa kuwa hatoinuka,mlifirahi zaidi kusikia zimempata 16 kwa utaalamu wenu wa silaha mkajihakikisha kuwa hakuna aliyewahi kupigwa risasi 16 akainuka.Siku ziliposonga mkasema hata akipona hatokuwa timamu na itamchukua miaka japo kuongea.Punde picha za Lissu zikaanza kisambaa mkasema ni photoshop,sauti ya Lisu ikasikika mkasema imeigwa,mlikua sahihi kabisa maana hakuna aloyewahi kupigwa risasi 16 akapona mlikuwa sahihi kubisha,hamkujua yupo Mungu mwenye kumiliki uhai wetu.Mliporidhika kuwa picha na sauti ni yeye hakika mkasema hatokuwa na ubavu kumtaja bayana anayemshuku kutaka kumuua,mlomfananisha na Roma mkatoliki,Jana Lissu amenena sasa mnajipa matumaini mapya kuwa hatorejea hakika Lissu atarejea katika aridhi ya baba zake.
Ugumu wa mioyo yenu imefananishwa na ugumu wa moyo wa Farao yule wa nyakati za Mussa.Kilichompata kitawapateni,Ikiwa katika tukio hili hamkiri kwa vinywa kuwa yuko Mungu basi hatanyamaza.
Hii insha yote umemuandikia nani!?
 
Ubelgiji ndiyo makao makuu ya sekta ya madini duniani. Vita alizokuwa anapigana TL ni kubwa na nzito, bahati mbaya hakuwa na watu wenye uelewa, umakini na msimamo thabiti kama wake (wangekuwa wanajua hatari ya vita zile, asingekuwa anatembea bila hata mlinzi).

Namtakia kila la heri huko aendako, Roho wa Mungu amtangulie na kumlinda.
 
Kwani lissu ndio nan? Ni Mkenya? Mbona mie simfahamu?
 
Kila mtu na vesion yake mara risasi 38, mara 30 mwenyewe Msaliti anasema 16, basi tu ili mradi muongope!

Kwa hiyo haki ya msaliti ni kumpiga Risasi mnatumia mwavuli wa usaliti kupiga watu risasi je alisaliti nini unaweza leta ushaidi hata kakobe mtamwita msaliti soon hii Nchi sio mali ya mtu binafsi ya watanzania wote vyeo ni dhamana
 
Unahangaika sana!! Na utaendelea kuhangaika na Lissu... nasikia wewe ni mganga wa dunguli kwa nini usipige dunguli zako apone haraka arudi huyo msaliti??
Umesikia kwa nani?
 
Tatizo sio kusikia ni kuelewa
Mshana unaelewa kuwa mkiwa kwenye chombo cha usafiri baharini mkiwa mnakusudia kufika upande wa pili mkiwa salama buher wa afya, then katikati ya bahari yenye kina kirefu na mkondo hatari, mmoja wenu anaanza kutoboa hicho chombo chenu na mnaona dalili za wazi za mtu huyu kufanikiwa kukitoboa chombo hicho kilicho salama yenu. Pamoja na kumshauri madhara ya kukitoboa hicho chombo lakin yeye akaendelea kufanya hivo.

Mshana Jr unaelewa huyo mtu inampasa kufanywa nn ili nyie mliowengi mpone. Unajua sawasawa nini kinampasa kimpate. Mkiendelea kucheka nae mnajua kitakachowapa nyinyi nyote,

Mshana Jr hebu sema kidogo watu wa aina hiyo huwa wanafanyweje kwenye nchi zingine za magharibi. Tuache siasa hizi za kibongo bongo, tuseme ukweli.

Hii nchi ikipata shida kama huyo mtu wenu anavopiga debe hata akiwa hospitali, siyo yeye atakae teseka, ni sisi na watoto wetu. Yeye atakuwa ameshatoroshewa huko ughaibuni.

Ukitaka kuamin mwambien aweke wazi ni nan wamegharamia matibabu yake. Aseme ni fulan na fulan ili kila mtanzania amjue yeye ni mtu wa aina gan.
Hata vitabu vya dini vimetaja adhabu ambayo mtu hupewa anapojaribu kuiharibu jamii anamoishi. Nabii isah mwenyewe kwa kinywa chake. Nabii isah anakubalika na wakristo na waislam pia. Kwa kinywa chake mwenyewe aliwahi kutamka kuwa yampasa mtu mmoja kufa kwa ajili ya wengi. Huwezi kuacha waliowengi kuangamia kwa ajili ya mtu mmoja.

Tuache kudanganyana. Nyeupe iitwe nyeupe
 
mshana jr,
Lazima serikali imetikisika na kutaharuki zaidi maana mtetezi wetu wa kweli na kaka wa taifa Mh. Tundu Lissu kuelekea Brussels Belgium /Luxembourg kulipo na makao makuu ya Jumuiya ya Ulaya / EU na bunge la ulaya siyo habari nzuri kabisa kwa wana-Lumumba na serikali yao ya CCM.

Habari za ukandamizaji, vitisho, kujaribu kumaliza maisha ya walio na fikra tofauti na utawala huu wa awamu hii zitatinga ktk kamati, bunge na makao makuu ya jumuiya ya ulaya /EU.

Na jumuiya hii ya ulaya hufanya kazi na maazimio kwa umoja wao ikiwemo kusitisha misaada, mikopo, kutenga nchi, vikwazo vya viza kwa viongozi kuingia EU na kuwekea vikwazo vya kiuchumi kwa tawala gandamizi zisizofuata demokrasia, katiba na uhuru wa raia kujumuika/kupashana habari.

Si bure Mshana jr , tunaona comments nyingi zinazoonesha woga, kukata tamaa, kusalimu-amri matamko ya kibabe, kuomba-dua la kuku Tundu Lissu awe mkimbizi nje ya nchi na ku-panick ktk kujibu uzi wako.
[emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116]
He is gone out of this land ...forever and he is not coming back..

Over.

Msiendelee kuwachosha watanzania..

EXILED.
 
Nimefadhaika sana Mshana Jr. kwa tafsiri yako ya alichokisema Lissu. Tukio lililompata Lissu ni la kinyama na kipekee kutokea Tanzania. Mbunge maarufu wa CDM kutaka kuuawa ni kitu cha kusikitisha sana.

Lakini siku zote ilikuwa ni watu wengine waliokuwa na uhakika (sio kushutumu) kuwa serikali na vyombo vya dola vimehusika. Sasa Lissu, kwa kauli yake mwenyewe, ametamka kuwa ana uhakika serikali ndio iliyotaka kumuua

Hii sasa inabadilisha mazungumzo. Sasa tuijadili hii conspiracy theory yake na pia tutoe conspiracy theories mbadala.

1. SERIKALI INAHUSIKA
Sababu kubwa inayotolewa ni kuwa Lissu amekuwa mwiba kwenye serikali ya awamu ya 5. Pia inasemekana alikuwa anafuatiliwa na SUV nyeupe ambazo zinahusishwa na Usalama wa Taifa.

Mimi hili sikubaliani nalo kwa sababu moja ndogo sana. Waliomshambulia Lissu ni limbukeni (armatures). Professional assassins wangeweza kumuua Lissu kwa risasi moja tu. Hawakuhitaji AK47 kummiminia risasi zaidi ya 38. Kwa hiyo hawa sio wauaji wa Serikali.

Sasa nani mwengine, nje ya serikali, alietaka Lissu afe na kuamua kukodi vijambazi uchwara kwenda kumuua, lakini ionekane kana kwamba ni Serikali?

Suala la Lissu kufuatiliwa na SUV nyeupe ilikuwa mbinu ya kuwaandaa wananchi kuamini kuwa serikali ndio iliyomuua Lissu.

CHADEMA KUHUSIKA.
Lazima ikumbukwe kuwa umaarufu wa Lissu ndani na nje ya CDM ulipaa sana hadi kumfunika Mwenyekiti, Katibu Mkuu na hata mgombea Urais wa CDM 2015.

Hawa watu walikuwa hawasikiki kabisa wakati Lissu anaunguruma. Wanachama wengi walikuwa wanasema wazi wangetaka Lissu awe Mwenyekiti wa Chama na wengi pia walitaka Lissu agombee urais ifikapo 2020.

Ni katika mtizamo huu ndipo ninapopata conspiracy theories zangu mbili zifuatazo.

2. KUNDI LINALOMTAKA MBOWE ABAKI KUWA MWENYEKITI LILIHUSUKA
Tukubali, kuna kundi kubwa sana ndani ya CDM ambalo bado wana imani na Mwenyekiti wa sasa Mh. Mbowe. Waliona Lissu anavyokuja vibaya na kuhatarisha kiti cha Mwenyekiti. Waliunda mkakati wa kuiondoa kadhia hiyo, lakini ionekane kana kwamba serikali ilihusika.

3. KUNDI LINALOMTAKA LOWASSA AGOMBEE TENA URAIS UFIKAPO 2020
Kadhalika, kuna kundi kubwa ndani na nje ya CDM ambalo bado wana imani na Lowassa na wangependa apate fursa nyingine kugombea kiti cha Urais ifikapo 2020 na 2025. Lissu alikuwa anavuruga order iliyopangwa kwa kutoa ushawishi wa kufanywa yeye awe mgombea Urais.

Pengine kundi hili na lile la Mbowe walishirikiana au ni moja katika kutekeleza azma yao ya kuindoa kadhia, Lissu.

TAMATI
Tuwe waangalifu sana tunapotoa conspiracy theories. Hakuna mwenye ushahidi kama Magufuli na Makonda (Theory 1) walihusika. Pia mimi sina hata chembe ya ushahidi kama Mbowe au watu wake (Theory 2) au Lowassa na watu wake (Theory 3) walihusika na unyama huu.

Kwahiyo it is not fair kwao kuanza kuzizungumzia hizi conspiracy theories kana kwamba ni kweli. Tunawapaka matope bila ya ushahidi wowote. They deserve better.

Kwa upande wangu ninawaomba wasomaji wapuuzie Theories 2 na 3. Ni tamthilia tu toka kichwani kwangu. Sina ushahidi wowote.

Bali nashangaa kwa watu niliowaheshimu sana humu JF kama wewe mshana jr kuielezea Theory 1 as if ndio ukweli wenyewe.

Very disappointed.
 
Back
Top Bottom