Umeandika mengi sana lkn ni 'Fiction' tu hizo hamna lolote hapo. Hata waliofanya hicho kitendo roho sio zao hata wenyewe wanafahamu hawako salama.Chadema kisimtumie TL vibaya.
Wamshauri vizuri atulie kama alivyoshauriwa na Nape Nnauye.
Nape bila shaka anazijua vizuri siasa za nchi maskini hasa za Afrika.
Akumbuke wale waliojaribu kumuu bado wapo mitaani na hawajakamatwa. Hatujui kwa hakika walitumwa na nani mpaka sasa.
Hatujui kuwa wale waliomtuma wameshamaliza mission yao au bado!
Na je, Kwa nini matibabu yafanyike Ubeligiji?
Hii nchi sijaona kuwa ni nchi salama kwa mataifa ya Afrika na Demokrasia duniani?
Jambo la kusikitisha ni kwamba Wapinzani wenye afya zao wameufyata na sasa wanamtanguliza mbele mgonjwa.
Na cha ajabu zaidi wanamkatisha tamaa kwa kushindwa kuwa na mbinu za kujenga chama badala yake wanachama na viongozi wa chama wanapukutika kwa kukumbilia kule kule wanakotuhumu kuwa ndipo watesi wa Lisu walipo.
Mbowe ataondoka Chadema na kukiacha kikiwa taabani kifedha ,kisera, kiitikadi,kimwelekeo, kimiundo mbinu, kichama (wanachama) n.k.
Kifupi Mbowe hata kama ataamua kuacha demokrasia imuondoe madarakani au kustaafu uenyekiti lakini atakua ameweka miundo mbinu rahisi kwa CCM kukiua hicho chama kirahisi kwa kuwa ni chama kisicho na mizizi. Ni chama cha matukio tu ndio maana kinang"ang"ana na kampeni za majukwaani zisizoisha ili wapate nafasi za kutuhumu watu na kuwachafua majukwaani bila kuzungumzia nafasi za kujenga chama kimiundo Mbinu.
Mbowe alikua na nafasi kubwa kujenga miundo mbinu ya chama baada ya uchaguzi.
Mh. Rais kabla na baada ya kuingia madarakani aliipenda sana Chadema kwa kuwa ndiyo iliyokua inapambana na ufisadi na ndio maana aliwashauri kuwa wajenge ofisi zao za chama makao makuu Dodoma.
Ushauri ule ulikua ni mzuri sana wa kiungwana.
Wangemwelewa mpaka sasa wangekua na mchakato wa kujenga ofisi nchi nzima badala yake wanatumia pesa nyingi kukodisha majengo.
Ninachoona ni kuwa Mbowe naye yuko mbioni kurudi kule wanaporudi wenzake.
Na kwa hali ilivyo Chadema isipokuwa makini baada ya uchaguzi wa ndani ya chama kitaanguka kama NCCR mageuzi.
Huu hasa ndio woga wa Mbowe kuwa chama kinaweza kusambaratika endapo ataondoka madarakani. Anajua wazi kuwa ameshindwa kujenga chama kitaasisi na kuweka mizizi kuanzia vijijini.
Ni chama kilichoko kwenye briefcase yake mana hakina miundo mbinu maalum.
Kuna watu waliipenda NCCR mageuzi kwa sababu tu mwenyekiti alikua ni Mrema. Hasa watu wa kaskazini kwa maana ya wale wa eneo analotoka Mrema.
Hali hiyo inaonekana ipo pia Chadema. Mbowe amekua na matumaini makubwa kuwa anakubalika sana lakini ukweli ni kuwa alikubalika sana lakini kwa sasa anakubalika kidogo sana tena kwa upanda na eneo analotoka, ambalo nao pia wameanza kumkimbia kwa kasi baada ya kugundua kuwa wanaongozwa na mtu anayejali maslahi yake zaidi kuliko chama kama taasisi.
Maeneo mengine wanakipenda Chama lakini eneo lake wanampenda mwenyekiti na bila shaka watu wa nyumbani kwake watakua wote wamerudi CCM mara tu mwenyekiti huyo atakapoamua kuachia madaraka na kurudi kule madiwani wake wanakorudi kila kukicha ili 2020 awe na uhakika wa kutangazwa mshindi wa jimbo la Hai.
Kwa hiyo wanachama wa chadema wawe makini na waanze kujipanga namna ya kunusuru chama chao wakati wa kumchagua mwenyekiti mwingine. Na ikiwezekana mwenyekiti awe ni Mtu anayefahamika na kukubalika kanda zote.
Chama kijengwe kitaifa na kimfumo sio kimatukio na umaarufu wa mtu mmoja mmoja.
Figures?.......................Its not a big deal. Ila facts bado zinabakia palepaleKila mtu na vesion yake mara risasi 38, mara 30 mwenyewe Msaliti anasema 16, basi tu ili mradi muongope!
Acha kujitoa ufahamu bwana mdogo..!!!Kila mtu na vesion yake mara risasi 38, mara 30 mwenyewe Msaliti anasema 16, basi tu ili mradi muongope!
Huyo ni miongoni ya wale hawakupenda Lissu atamalaki tena.Lakini bado ni risasi
Hahshahahaha..!!!!Lissu ni jabari kwenye siasa weka mbali kabisa na yule mvaa hirizi, niliangalia jana alivyokuwa anaipinduapindua lugha ya malkia nikajiuliza vipi angekuwa kipara ingekuwaje?
Una iq ya mende km raisi wakoKila mtu na vesion yake mara risasi 38, mara 30 mwenyewe Msaliti anasema 16, basi tu ili mradi muongope!
Unata uambiwe hakupigwa risasi ila alipigwa kwa manati?Kila mtu na vesion yake mara risasi 38, mara 30 mwenyewe Msaliti anasema 16, basi tu ili mradi muongope!
Msaliti Magufuli anayefikiri hii nchi ni ya Baba yakeKila mtu na vesion yake mara risasi 38, mara 30 mwenyewe Msaliti anasema 16, basi tu ili mradi muongope!
Moja inatosha lakini Lissu anatoka sifaKila mtu na vesion yake mara risasi 38, mara 30 mwenyewe Msaliti anasema 16, basi tu ili mradi muongope!
Na wewe sema vesion yako, risasi ngapi?Kila mtu na vesion yake mara risasi 38, mara 30 mwenyewe Msaliti anasema 16, basi tu ili mradi muongope!
[HASHTAG]#Atabu[/HASHTAG] anatuharibia nchi yetu. Hana uchungu nayo kabisa, ila yote Tisa kimbembe ni mwaka huu... Tuombe uzima tushuhudie kwa macho yetu.
Mwanasheria wa CHADEMA na Mbunge wa Singida Bwana Tundu Lissu kaondoka Hospital ya Nairobi kuelekea Ubelgiji kwa matibu zaidi baada ya kunusurika kifo kutokana na shambulio la risasi 38 mjini Dodoma mwishoni mwa mwaka uliopita.
Pamoja na mijadala mingi mitandaoni kuwa ni nani kwa hakika alihusika na shambulio lile lakini mhanga mkuu Tundu Lissu hakumung'unya maneno kila alipopata nafasi ya kuongea.
Ameituhumu serikali na mamlaka ya juu kwa kile kinachoitwa 'assassination attempt' jaribio la kutaka kuua....!!!
Kwa serikali zinazojali utawala wa sheria hizi ni tuhuma nzito za aibu na zenye kuitia DOA kubwa serikali kitaifa na kimataifa. Hapa kwetu tunaenda kibongobongo.Fix nyingi siasa nyingi, vitisho na ukatili usio na sababu.
Tangu litokee shambulio lile la Lissu, ambalo aliepuka kifo kwa muujiza tu. Mabadiliko mengi yametokea. Yametokea kwa haraka na kwa muda mfupi ni wazi washambuliaji wake hawakutegemea apone. Kupona kwake ni kihoro na jinamizi kubwa kwao.
Wanamfahamu vema Lissu ni mtukutu, mjanja kwenye siasa na makini kwenye sheria, ana kipawa cha kujenga hoja zikakubalika. Sio mwoga! Haogopi ni msomi mzuri wa sheria na ni mpambanaji asiyeshindwa.
Watesi wake wanatambua vema kuwa risasi zile licha ya kukosa kumnyofoa roho lakini zimeshindwa kabisa kuleta madhara kichwani kwenye injini ya fikra pevu na maarifa.
Wanatambua vema kuwa kwa kipindi chote alichokuwa hospital, licha ya majeraha makubwa aliyopata lakini mwili na akili vimepata mapumziko ya kutosha.
Atarejea kwa nguvu mpya kasi mpya na ari mpya...!!! Na hapa ndio penye kutatiza sana! Sasa hivi jumuiya za kimataifa zinajua fika nini kimempata na nini kimetokea... CV imechafuliwa vibaya kabisa.!!
Mkakati uliopo ni kuanza kutunga sheria za makosa mitandaoni na vyombo vya habari haraka na kuanza kuvichukulia hatua hata kama makosa yenyewe ni mepesi na hayana mashiko.
Kila anachoongea sasa kinarekodiwa na kuhifadhiwa...! Hivi karibuni serikali imesema SI VEMA KUBISHANA NA MGONJWA. ' Anasubiriwa apone...!
Anasubiriwa arudi. Kuna upande hauko tayari kumuona tena anatamalaki jukwaa ni na kwenye vyombo vya habari na mitandaoni..!!
Mashtaka ya uhaini na kukashifu mamlaka yanamsubiri lakini TUTAUKOMBOA WAKATI...!!!!
Hujaelewa lengo langu?"Atabu"?????? au ni haraka ya kutaka kupost