Tundu Lissu kuwekwa kizuizini?

Tundu Lissu kuwekwa kizuizini?

Kila mtu na vesion yake mara risasi 38, mara 30 mwenyewe Msaliti anasema 16, basi tu ili mradi muongope!
ata ingekuwa moja bado inaogopesha.
Rais Kennedy aliuawa kwa risasi moja tu.
 
Namshauri asurudi, au inawezekana wakamkatalia kurudi! and this is most likely.
Namshauri aombe ulinzi wa Trump! UK etc. Let him talk to trump (if possible) mshana jr
Lissu atarejea nyumbani na ataendelea na shughuli zake kama kawaida .

Shetani hajawahi kumshinda Mungu .
 
Lissu atarejea nyumbani na ataendelea na shughuli zake kama kawaida .

Shetani hajawahi kumshinda Mungu .
nahofia maisha yake maana huyu mtu wa hapa ni hatari. Alisema "walaze", , hii kauli na inatekelezwa sana. Kila siku mauaji kwa kisingizio cha eti majambazi
 
Hata mngempiga risasi 100 ingekuwa bure tu maana ilipangwa mshindwe. Naona frustrations zenu zitazidi.
Kila mtu na vesion yake mara risasi 38, mara 30 mwenyewe Msaliti anasema 16, basi tu ili mradi muongope!
 
Nani huyo hana woga? kwanza hii ni kaa mbali jiulizeni risasi zote na bado yuko hai? Yule mtingisha makalio ninyi mnamwita eti RC najua hana amani kabisa lazima atajua kwamba binadamu sio kuku
Hujanielewa au umeamua tu kunilisha maneno ?
 
Risasi zilizokusudiwa kumpata Ni 38 lakini 16 zilimpata na moja bado ipo mwilini mwake
Nyie msihangaike na vibwetere hao(yeye na jingalao) kwani wanajua vizuri kila kitu ila wamevaa ngozi za mbwa mwitu
MKUU WEWE KICHWA NGUMU AU? RISASI ZAIDI YA 30 ALIRUSHIWA NAHATA SPIKA ALISEMA (MAANA NDIYE UNAMWAMINI), HALAFU HIZO 16 NDIZO ZILIMFIKA MWILINI NA KUINGIA
 
Kila mtu na vesion yake mara risasi 38, mara 30 mwenyewe Msaliti anasema 16, basi tu ili mradi muongope!
2eb029566d45acaad400688c0de7c47f.jpg
 
Haki haijawahi kushindwa popote tangu zamani za kale za wafalme wenye nguvu za kimamlaka kina Mfalme Daudi.
Kusudi la MUNGU kumponya Lissu lipo; kuna kazi inabidi aifanye.
Mamlaka hizi za duniani (zilizokengeuka) ni za mda mfupi na huwa hazifui dafu mbele ya uso wa Bwana.

Lissu aliyekuponya yupo upande wako atakusimamia, move on ...
 
Mwanasheria wa CHADEMA na Mbunge wa Singida Bwana Tundu Lissu kaondoka Hospital ya Nairobi kuelekea Ubelgiji kwa matibu zaidi baada ya kunusurika kifo kutokana na shambulio la risasi 38 mjini Dodoma mwishoni mwa mwaka uliopita.

Pamoja na mijadala mingi mitandaoni kuwa ni nani kwa hakika alihusika na shambulio lile lakini mhanga mkuu Tundu Lissu hakumung'unya maneno kila alipopata nafasi ya kuongea.

Ameituhumu serikali na mamlaka ya juu kwa kile kinachoitwa 'assassination attempt' jaribio la kutaka kuua....!!!

Kwa serikali zinazojali utawala wa sheria hizi ni tuhuma nzito za aibu na zenye kuitia DOA kubwa serikali kitaifa na kimataifa. Hapa kwetu tunaenda kibongobongo.Fix nyingi siasa nyingi, vitisho na ukatili usio na sababu.

Tangu litokee shambulio lile la Lissu, ambalo aliepuka kifo kwa muujiza tu. Mabadiliko mengi yametokea. Yametokea kwa haraka na kwa muda mfupi ni wazi washambuliaji wake hawakutegemea apone. Kupona kwake ni kihoro na jinamizi kubwa kwao.

Wanamfahamu vema Lissu ni mtukutu, mjanja kwenye siasa na makini kwenye sheria, ana kipawa cha kujenga hoja zikakubalika. Sio mwoga! Haogopi ni msomi mzuri wa sheria na ni mpambanaji asiyeshindwa.

Watesi wake wanatambua vema kuwa risasi zile licha ya kukosa kumnyofoa roho lakini zimeshindwa kabisa kuleta madhara kichwani kwenye injini ya fikra pevu na maarifa.

Wanatambua vema kuwa kwa kipindi chote alichokuwa hospital, licha ya majeraha makubwa aliyopata lakini mwili na akili vimepata mapumziko ya kutosha.

Atarejea kwa nguvu mpya kasi mpya na ari mpya...!!! Na hapa ndio penye kutatiza sana! Sasa hivi jumuiya za kimataifa zinajua fika nini kimempata na nini kimetokea... CV imechafuliwa vibaya kabisa.!!

Mkakati uliopo ni kuanza kutunga sheria za makosa mitandaoni na vyombo vya habari haraka na kuanza kuvichukulia hatua hata kama makosa yenyewe ni mepesi na hayana mashiko.

Kila anachoongea sasa kinarekodiwa na kuhifadhiwa...! Hivi karibuni serikali imesema SI VEMA KUBISHANA NA MGONJWA. ' Anasubiriwa apone...!

Anasubiriwa arudi. Kuna upande hauko tayari kumuona tena anatamalaki jukwaa ni na kwenye vyombo vya habari na mitandaoni..!!

Mashtaka ya uhaini na kukashifu mamlaka yanamsubiri lakini TUTAUKOMBOA WAKATI...!!!!
Sisi tuliokuwepo wakati wa mapinduzi ya kiislam ya Iran tunajua kuwa Mhe. Tundu Lissu hawezi kurudi nchini kirahisi, atarudi kwa nguvu ya umma kushiriki uchaguzi. Kipindi ambacho hataguswa.
 
Kila mtu na vesion yake mara risasi 38, mara 30 mwenyewe Msaliti anasema 16, basi tu ili mradi muongope!
Hata ukijaribu kupindisha ... Ukweli utabaki kuwa Ukweli daima .......... Ingawa unajifanya hujui ngoja nikusaidie!!

Risasi 38 zilipigwa, risasi 30 zilipiga gari na kati ya hizo 16 zilimpata Lissu!!
 
Lissu ameonekana huko anahangaika kutembea Aisee.
Mungu UA hao waliofanya haya na kupanga.
Yani yani yani hakika kisasi kipo tu.

Watanzania daini katiba mpya na tume huru vinginevyo mtapata tabu sana
 
Back
Top Bottom