Tundu Lissu hakugoma "KUTOKA NJE"

Tundu Lissu hakugoma "KUTOKA NJE"

Anko Sam

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2010
Posts
3,254
Reaction score
908
Wataalamu wa lugha yetu adhimu watuambie maana ya neno "Toka nje"

Mimi nijuavyo "kutoka nje" ni kinyume cha "ingia ndani". Hivyo sikumshangaa Tundu Lissu kumshangaa J. Ndugai alipotamka "...Tundu Lissu toka nje..." Sasa atoke nje aende wapi wakati alikuwa tayari yumo ndani ya ukumbi?Wale askari walivyo ambiwa "Askari mtoeni Tundu Lissu nje" nao bila kuelewa vizuri wakaenda kumshinikiza Lissu aende nje. Wao walitakiwa waulize kama Mh. Lissu anatakiwa atolewe ndani ya ukumbi au la!

Hivyo sioni kosa la Tundu Lissu wala wabunge wa CHADEMA kwenda kuwazuia wale askari wasimtoe ndani na kumpeleka nje, kwani walikuwa wanatekeleza amri ya kiti; Mtoeni nje muingize ndani! Askari walitekeleza kinyume chake! Lol!

Swali: Je kama hatufahamu kiswahili kwa kiasi hiki, kiingereza tutakiweza? Hapa naungana na wale wanaosema kiswahili kiwe ni lugha ya kufundishia mpaka mwisho wa darasa!
 
Yeah, ndugai angesema "toka ndani" au "nenda nje"
 
Umenikumbusha kulikuwa na darasa la HGK katika shule niliyosoma enzi hizo....Mwalimu wa zamu aliwaambia watoke nje "Tokeni nje" wakawa kimya...alirudia kama mara nne watu kimya wanamtazama....
Akaenda kumwambia Headmaster...Headmaster akawauliza kwa nini mmekaidi amri ya Mwalimu...wakajibu "Nadhani hata wewe unaona tuko ndani,na mwalimu alisema tokeni nje...maana yake tuingie ndani...sasa tayari tupo ndani kumsikiliza mwalimu anasemaje"
Lakini nasikitika wengi wao...sijui walipo maana matokeo yao yaliwabishia vivyo hivyo!
 
Wataalamu wa lugha yetu adhimu watuambie maana ya neno "Toka nje"

Mimi nijuavyo "kutoka nje" ni kinyume cha "ingia ndani". Hivyo sikumshangaa Tundu Lissu kumshangaa J. Ndugai alipotamka "...Tundu Lissu toka nje..." Sasa atoke nje aende wapi wakati alikuwa tayari yumo ndani ya ukumbi?Wale askari walivyo ambiwa "Askari mtoeni Tundu Lissu nje" nao bila kuelewa vizuri wakaenda kumshinikiza Lissu aende nje. Wao walitakiwa waulize kama Mh. Lissu anatakiwa atolewe ndani ya ukumbi au la!

Hivyo sioni kosa la Tundu Lissu wala wabunge wa CHADEMA kwenda kuwazuia wale askari wasimtoe ndani na kumpeleka nje, kwani walikuwa wanatekeleza amri ya kiti; Mtoeni nje muingize ndani! Askari walitekeleza kinyume chake! Lol!

Swali: Je kama hatufahamu kiswahili kwa kiasi hiki, kiingereza tutakiweza? Hapa naungana na wale wanaosema kiswahili kiwe ni lugha ya kufundishia mpaka mwisho wa darasa!

Mkuu mbona unakumbatia unyasi wakati jamaa wanakula msoto.
 
Kiswahili lugha ngumu sana Tokeni nje ie ingieni ndani!
Ila ilo neno huwa twalitumia kwa mazoea tuu
 
Jamani sasa hii ya kwetu ya kimatumbi 'toka nje' tayali imekuwa lugha gongana, ndo maana 'impotent' imekuwa issue, tuna tatizo la lugha kama taifa!
 
Alikuwa sahihi, ukanushi mara nyingine kuleta maana chanya. Hapo hakuna ukakasi wowote katika lugha. Hivyo Makinda hakubananga Kiswahili wala matamshi yake.

Mfano neno Sijambo, huonesha buheri, lakini katika muktadha wa matashi, hukanusha ubuheri
 
Hapana
Sijambo imetokana na salamu ya kuuliza
yaani
Jambo = Si jambo
(Problem) = (No problem)
 
kweli mchambuzi umewafusha thithiem na spika.lkn waweza kwenda chuo kuchukua ---- degree ya kiswahi kwani wamechakachua hadi qualifications za kujiunga na chuo.mtu alimayema std 7 sasa ivi ana jiunga chuo kikuu frm TCU gamba kazini! hizi zote ni harakati za kungangani urais mwaka 2015 wale wenzengu amboyo wanautaka uraisi alafu wamemaliza std 7 na sifa za kuingia ikulu hamna
 
watanzania kweli tunaona sana subiri mwaka 2015 mtaona matokeo spika unatakiwa kutenda haki mbona wabunge wa ccm wanatamka matusi bungeni na hukuwachukulia hatua au unaangalia itikadi siyo tunaomba mchango wenu wa mawazo mtusaidie watanzania mungu wabariki wanyonge wetu kuna siku tutapata ukombozi wakatiwa ukombozi ni huu sasa
 
Back
Top Bottom