masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,621
- 14,577
Mtu anayetapatapa atahalalisha kila uongo uonekane ukweli!Wataalamu wa lugha yetu adhimu watuambie maana ya neno "Toka nje"
Mimi nijuavyo "kutoka nje" ni kinyume cha "ingia ndani". Hivyo sikumshangaa Tundu Lissu kumshangaa J. Ndugai alipotamka "...Tundu Lissu toka nje..." Sasa atoke nje aende wapi wakati alikuwa tayari yumo ndani ya ukumbi?Wale askari walivyo ambiwa "Askari mtoeni Tundu Lissu nje" nao bila kuelewa vizuri wakaenda kumshinikiza Lissu aende nje. Wao walitakiwa waulize kama Mh. Lissu anatakiwa atolewe ndani ya ukumbi au la!
Hivyo sioni kosa la Tundu Lissu wala wabunge wa CHADEMA kwenda kuwazuia wale askari wasimtoe ndani na kumpeleka nje, kwani walikuwa wanatekeleza amri ya kiti; Mtoeni nje muingize ndani! Askari walitekeleza kinyume chake! Lol!
Swali: Je kama hatufahamu kiswahili kwa kiasi hiki, kiingereza tutakiweza? Hapa naungana na wale wanaosema kiswahili kiwe ni lugha ya kufundishia mpaka mwisho wa darasa!
Mwisho wa yote JK atasaini muswada jogoo liwike lisiwike!